St. Francis Mbeya kuna siri gani?

Kama una mtoto ni average pale hana nafasi,hakuna blah blah,mtoto Kipanga atapeta,akiwa slow learner wewe tafuta kwingine,St.Francis wala usiifikirie kichwani mwako,nyingine ni Cannosa na Marian,hizo usisogelee pia.
😂😂😂Hafu wanafunzi wao wote unakuta primary kasoma shule ya private ambayo ni nzuri sana, hupati Binti wa kayumba mle
 
Siri ya kwanza ni ubora wao ila pia
Kuna kaujanja ujanja fulani kwa idhini ya refa......

Ngoja niishie hapo.....

Pongezi kwa vijana wote na wale waliokosa wasijione sio kitu maisha hayahitaji kukata tamaa
Kwa idhini ya refa hembu funguka mzee wangu?
 
Muongo
 
Walau kuna watu mnaukubali uhalisia.Hawa wanaobisha,si wapeleke kwanza watoto wao tuone kama hata watapata hiyo nafasi ya kuingia pale
 
Shule za vipaji maalumu za serikali nazo zinachuja wanafunzi.
 
Kuwa na high IQ co lazima uwe presidaa jomba, co lazima uwe ktk position inayoonekana.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kipindi cha magufuli kipi twende ya mwaka 2020 tu hapo. Mbona ilikua na 1 tupu na zote single digit na ilikua ya kwanza kitaifa
Let's kuanzia 2016- 2020 tuone. Sema nimeshagundua hizi shule zinachuja Sana wanafunzi wanachukua Ile cream.
Kuwa huyu mwanafunzi anayeenda hapa pia unakuta akachaguliwa shule zile zenye ufaulu mkubwa aka vipaji.
So alifika huko mwalimu anakuwa na bidii kutaka kumzidi mwanafunzi.ujue Kuna shule ambazo mwalimu Ana bidii kuliko dent.
So ukichanganya kuwa hizi shule both dent and ticha have got bidii na ushirikiano wa Hali juu. Wako committed lazima watoboe.
Mana kwa serikali ni bidii zetu kukomaa.
Binafsi advance physics na maths nimekomaa na washkaji wakanielekeza hata sidhani kuwa nilitegemea walimu kufaulu.
Olevo kidogo baadhi ya subjects yaani unaenda class tayari umeshasoma
 
Binti yangu alisomea pale na kupata div. one na ushindi huo ulimpa msingi mzuri sana wa A level na kufanikiwa kupata pointi 6 A level. St. Francis ni shule nzuri sana.
Asante sana kwa huu ushuhuda,nina Nieces wawili pia,wamepita pale na UDSM,huyo aliemaliza kwa sasa yupo TPDC na mwingine yuko mwaka wa pili ,tunasubiri akimaliza tuone atapata GPA ipi.
 
Unalosema ni kweli, angalia A zao ni za yale masomo ambayo wakipiga past paper za kutosha lazima wapate A. Waangalie katika physics Wana C na B za kutosha. Mwanafunzi akifundishwa vizuri mitihani ya kidato cha 4 ni rahisi sana kwa masomo ya sanaa.
Ndo ivo mkuu sasa nashangaa hawa watu wanaosema eti wananunua mitihani wakati ni ishu ya mipango tu.

Mi mwenyewe kuna dogo apa alikua anasoma kwa bidii somo la computer akijua wazi kua hesabu anaweza kufeli, na kweli hesabu kagonga F lakini hiyo comp ana A. Na hiyo imembeba mpaka ana diviaion 1 kabisa.

Ni mipango tu sio ishu ya kushangaza.
 
Pia aina ya watoto wanaokwenda pale ni top cream kuanzia walikotoka,halafu mtu anatuletea hapa hadithi za Shule kununua mitihani😂
Yani ni vichekesho mkuu, mpaka unashangaa inakuaje mtu ashangae huo ufaulu mpaka unapata shaka yeye alipata ngapi mpaka aone haiwezekani kupata one hizo.

Mtu kama huyu ataona ni sawa mwanae akipata hata 4 au 0 kabisa coz yeye mtihani kwake ni kitu kigumu kichizi.
 
Wanafunzi wanandaliwa vyema sana na zaid Walimu wanapewa motisha sana wanafanya kazi kwa moyo

Mwl kupewa gari kawaida sana nyumba kawaida
Bado mashahara mnono



Sent from my TECNO CX Air using JamiiForums mobile app
 
Nasoma comment nabaki kucheka tu,kama wanajua ni rahisi hivyo,si wapeleke watoto wao wakajaribu mchujo wa pale kama wataweza.
 
Na hiki ndicho inachofanya shule kama Tusiime ile shule naipa big up sana inajua kulea wanafunzi mwanafunzi anakuja hajui kitu ila anatoka na matokeo ya kuridhisha

Siyo shule kama Marian ambazo wanachukua watoto wenye ufaulu mkubwa ili wasihangaike nao kuwalea kutoka kuwa vilaza hadi vipanga ili walinde reputation ya shule yao

Mfano Marian form five mara nyingi huwa wanachukua waliopata division one za single digits tu kwenye matokeo ya form four yaani 1.7 hadi 1.9 tu chini ya hapo hawaenroll
 
😂😂😂Hafu wanafunzi wao wote unakuta primary kasoma shule ya private ambayo ni nzuri sana, hupati Binti wa kayumba mle
Sijui wanadhani hizo Div 1 zinatokea tu kwa bahati mbaya,mtoto kapita Canossa Primary School au Liberman anakwenda St.Francis,uje ushangae kapataje division One😂
😂😂
 
Mkuu hao huwa wanaselect wenye vipaji tuu.Mchujo wao siyo wa kitoto,ni heavy duty.Mtoto wako akichaguliwa st.Francis maana yake yuko vizuri sana kichwani.Halafu wanakutana na mazingira wezeshi sana ya shule.Mimi nawaheshimu sana hao wanaopata point 7 toka government school.huyu angekuwa pale angepata A zote za mia mia
 
Wameset standard yao hivyo,kwanini uwalaumu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…