St. Francis Mbeya kuna siri gani?

Mitihani ya siku hizi hamna kitu 1. Rais wa kwanza wa Tanzania ni nyerer......... 2. Binadamu ana macho mawi.......
Sawa mitihani ya siku hizi hamna kitu. Hebu niambie, wale wa kule Pemba na Mtwara ambao shule zao zinakuwa za mwisho kitaifa, WANAFANYA MITIHANI IPI!? Ni hiyo wanayofanya hawa wa Mbeya au mingine.!?? Kwamba ni migumu zaidi ya wanayofanya wenzao.!????
 
ina maana sisi tulosoma kipindi kile hatukuwa na akili kweli?
Unaweza ukawa uko vyema ila kwa hawa wadada achana nano hata mimi nilijitahidi nilipata point kumi na mbili O level ila kawaida tu
 
Yaani umeandika uhalisia. Badala ya kupongeza waliofaulu, tunawalaumu kwanini wanafaulu
 
Hizi shule zina mbinu mbadala sio bure one ya saba wanafunzi wote kwa hiyo wanalingana akili wote ila hongera zao kwa sasa elimu ni biashara,huyo wa ilboru amepiga kazi sana.
Kuna shule ya kata ya kichangachui hapa kgm kuna one za saba kama 7 hawa ndio wanajeshi wa kweli hakuna biashara ni kichwa madogo wameongoza kwa somo la physics kimkoa kitaifa wamekuwa wa 36 kwa somo la physics tena shule ya kata kubaabeki hawa ndio majemedari.
 
Yaani kiongozi wewe ndiye umemaliza kila kitu. Comments nyingine baada ya hii ni za kunogosha tu mazungumzo sebuleni.
 
Wakiingia chuo makarai, masup, macarry-over na madisco ya kufa mtu.
 
So wanaweza kununua miaka yote hiyo, mbona zingine hazinunui na zinalipa ada kubwa lakin matokeo sisimizi
 
Unazungumziaje ilboru yenye 1.7 kama 39 hivi?
 
Mimi binafsi nakataaa hayo matokeo aisee ,hata kama Wana akili huo ufaulu wa kiasi hicho Kuna kitu cha ziada ...hio shule ichunguzwe vzuri kuanzia miezi mitatu kabla ya kufanya mtihani na siku za mitihani
Uliza kwanza kabla hujaandika. Wanafanya mitihani watoto wangapi wa la saba kabla hawajachukua hao 92? Wanafika mpaka 3000 na zaidi. Sasa imagine out of 3000 wanachukua 92. Cream tupu
 
So wanaweza kununua miaka yote hiyo, mbona zingine hazinunui na zinalipa ada kubwa lakin matokeo sisimizi
Sikia nikwambie mkuu maisha ya shule Mimi nayajua Tena zaidi ya unavodhani ...

Shule kubwa kama hizo ,zinawalimu wakubwa Sana wenye uzoefu wa hali ya juu ,na wanakuwa na connection na walimu wengine zaidi ..

Wanaotunga mitihani ni walimu kutoka kanda mbalimbali ,na wabobevu ,hutoa maswali na mwisho wa siku mtihani kitungwa ...

Utake usitake ,upende usipende hizi shule zinamazingira Safi ,walimu Safi ,lakini wananunua mitihani week kadhaa kabla ya pepar ,.....

Fuatilia mitihani wanayofuanya week mbili kabla ya mtihan pre -necta ,ready for necta ,hio ndio mitihan inayotolewa imejaa maswali yanayotoka necta ...

Sio kwamba wanasoviwa siku ya mtihan hapana ,wanafanya maswali yatakayotoka necta week kabla na walimu wanasisitiza kuyakalili ,....

Kama Kuna swali gumu ambalo linasahaulika ,basi mwalimu ataliimba darasana kila siku na mwisho wa siku wanalikuta necta ....

A inaanzia 81-100 ,bro mtihan wa physics , mathematics , biology , chemistry kwa watoto wote 97 wapate A ,???????? Hawa wa kibongo kabisa ? Woteeeee ? ....

Aiseee ,Mimi nakataa hayo matokeo ...hao watoto uwezo wao wa kawaida tu ,sio wa kupata huo ufaulu wote ,kwa kusema sijui walimu Bora ,mazingira Bora ,...
 
Kwa uwongo huu unapaswa utunukiwe PHD katika sector hiyo😂
😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…