St. Francis Mbeya kuna siri gani?

Hiyo shule haina habari za mchujo. Angalia matokeo yao ya form 2. Wanafunzi 91 wote wana div 1 za 7. Na miaka yote idadi yao ni hiyo. Wanacheza 90.
 
Imeanza 98 na walikuwa wa 9.... Kuna mwaka fulani walitaka waitie kibano kwa kuiba matokea ila Rais yule aliingilia kati wakayamaliza
 
Imeanza 98 na walikua wa 9....kuna mwaka fulani walitaka waitie kibano kwa kiiba matokea ila Rais yule aliingilia kati wakayamaliza
Asante kwa marekebisho. Kuhusu kuiba mitihani sina uhakika, maana huyu dogo tangu primary alikuwa smart na huwa anasoma sana so hata anavyofaulu sishangai, na ndio ameingia form four huu mwaka.
Nakumbuka wakati wa interview kulikuwa na wanafunzi wengi sana lakini walichukuliwa 96 tu, na madarasa yao mnapitishwa kuyaona.
 
Ada imefika ngapi? Na ni maswali yapi wanauliza kwenye interview?
 
Mimi binafsi nakataaa hayo matokeo aisee ,hata kama Wana akili huo ufaulu wa kiasi hicho Kuna kitu cha ziada ...hio shule ichunguzwe vzuri kuanzia miezi mitatu kabla ya kufanya mtihani na siku za mitihani
Kwa taarifa yako huwa inachunguzwa sana tu. Siri ya kufaulu kwao ni 1.Walimu wanalipwa vizuri sana, kwahiyo wanafundisha bila stress 2.Walimu wanafundisha sana 3.Motisha kwa Walimu ni nyingi Matharani kila A Ina kiwango chake Cha pesa ambayo Mwalimu analipwa akifaulisha. 4.Watoto wale wakiwa mazingira ya shule ni kuongea kingereza muda wote. 5.Mazingira mazuri na tulivu ya Wanafunzi kujisomea. 6.Screening aka mchujo wa Wanafunzi ni mkubwa Sana. 7.Commitment ya Walimu na Wanafunzi.
 
Leta ushahidi.
 
Kwa hiyo kila mwaka wao wananunua?

Feza schools nao kila mwaka wananunua?
 
Ufaulu hauna mahusiano kabisa na mafanikio kisiasa, kiuchumi na kufahamika. Ukute Wana kazi kubwa na za maana lakini kwasababu kazi zao sio za kuwapa umaarufu ndio maana huwezi kujua.
 
Tuache wivu usio na maana,
Tusiongee tusiyo yajuwa,

Tembelea ile shule uone walivyo makini.

Kuanzia kutunza muda, kazi za ziada pamoja na masomo.

Ni kweli kabla ya kuingia pale lazima mwanafunzi afanye mtihani wao, ambapo waliofaulu vizuri ndio huchaguliwa, hakuna rushwa.

Hivyo siri ya kwanza ni uchaguzi wa wanafunzi.

Siri ya pili ni walimu bora na wanao jituma.

Siri ya tatu ni motisha kwa walimu na wafanyakazi kutoka kwa mwajiri.

Siri ya nne ni nidhamu kali ikiambatana na sheria zao

Siri nyingine ni kumcha Mungu, wana ratiba nzuri ya kumcha Mungu

Siri nyingine ni nidhamu ya ratiba na muda, kwa waliopeleka watoto wao pale waulize hutokea nini wakichelewa hata dakika 5.

Hakika wanastahili pongezi.

Hivyo badala ya kubeza, yafaa kujifunza utaratibu wao wa ulezi na ufundishaji.

Ada yao 2021 ilikuwa around milioni mbili na laki tano kwa mwaka, shule nyingi pia zinatoza hivyo.

Dhana ya kwamba A level hawafaulu sana ni kwa sababu ya ufundishaji tu wa shule waendazo.

Hata huko vyuoni, sababu ni hizo hizo, na uhuru ambao hawajauzoea na hupelekea kujisahau kisha kuharibikiwa, wababa na vijana wengi huwaharibu watoto wa vyuo iwe kwa tamaa au ushawishi. Lakini pia bado wahadhiri wengine wana ile tabia ya kukomoana, ama kutofundisha ipasavyo...

#Kutokufaulu siyo chaguo!

Hongera sana kwa St. Francis Girls.


Wanastahili kwa kweli.

View attachment 2083779
 
Wako vizuri sana. Mtihani wa form wameongoza kitaifa. Wapili Kemebos. Sasa baada ya miaka miwili tutazishutumu wizi.
 
Baraza la mitihani lijitadhini upya. Waepuke mitihani ya multiple choice haraka iwezekanavyo.
 
Chuo wapi wewe? Hata sisi tumesoma na hao pia wanafunzi unamdanganya nani humu? Au kisa hakuna kujuana names humu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…