St. Francis Mbeya kuna siri gani?

St. Francis Mbeya kuna siri gani?

Kwa taarifa yako huwa inachunguzwa sana tu.Siri ya kufaulu kwao ni 1.Walimu wanalipwa vizuri sana,kwa hiyo wanafundisha bila stress 2.Walimu wanafundisha sana 3.Motisha kwa Walimu ni nyingi Matharani kila A Ina kiwango chake Cha pesa ambayo Mwalimu analipwa akifaulisha. 4.Watoto wale wakiwa mazingira ya shule ni kuongea kingereza muda wote. 5.Mazingira mazuri na tulivu ya Wanafunzi kujisomea. 6.Screening aka mchujo wa Wanafunzi ni mkubwa Sana. 7.Commitment ya Walimu na Wanafunzi.
Ni ngumu sana kuwashawishi "sizitaki mbichi hizi"..
Pengine ni namna ya wao kujisikia faraja mioyoni mwao..


Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Mimi binafsi nakataaa hayo matokeo aisee ,hata kama Wana akili huo ufaulu wa kiasi hicho Kuna kitu cha ziada ...hio shule ichunguzwe vzuri kuanzia miezi mitatu kabla ya kufanya mtihani na siku za mitihani
Ilishachunguzwa Sana mpaka na wasiojulikana walisimamia mtihani na Askari kanzu lakini mabinti wale ni kiboko. Shule Headmistress ni Sr mmoja matata Sana Kwa Elimu. Kifupi shule za Mission ni habari nyingine kabisa.
 
Aliyefaulu kiukweli bila kuiba mtihani ni huyo wa Ilboru, kipindi nimeenda advance level darasa letu lilikuwa na hao waliotoka st Francis na kila mtu aliwaogopa chakushangaza mtihani wa kwanza marks walizopata ni tofauti na hizo one zao. Huko private ni business kwa kwenda mbele na solving za paper kwa ajili ya kupata A za kutosha wakati zikija kitaa inputs yake ni zero kabisa
Maneno ya mkosaji
St Francis chapa fimbo ileile endelea kuburuza paka maji waseme mmma!
 
Elimu ya siku hizi imekuwa mdebwedo sana! Ukitaka kujua hili waulize walimu wa vyuo na waajiri. Binafsi sio Mara moja nimewafanyia interview vijana kwenye mambo ya kazi na naishia kusikitika jinsi uelewa wao ulivo wa mashaka
Vijana wa kileo ni janga
 
Haya mambo ya kusoma kwa kufundishwa kila kitu na walimu yalinilemaza nilivyoenda A-level na kukuta hakuna walimu na kutakiwa kukomaa mwanzo mwisho kupiga msuli....ndo maana wakienda chuo wanapata shida kwenye ufaulu kwani hawajazoea independent learning........
 
Sie Waswahili tumewekeza sana kwny ufaulu na si ueleawa

Hizi division one kalikali zinapoteleaga wapi hadi hazionekani tena?

Tanzania one wa form four walio graduate sambamba na Samia Suluhu miaka hiyo sijui sasa hivi yupo pori gani wakati mwenzie sasa ni Rais?
Kwani Samia alipata div gani form 4?
 
Mimi nimesoma chuo na watoto wanaotoka hizo shule mkuu ...

Siku ya mtihani wanakutana na maswali waliyokuwa wanasolve mwezi mmoja kabla ya necta ...

Sio kwamba siku ya mtihani wanasoviwa hapa ,ila pepar linasoviwa week kadhaa kbala ya necta na hayo maswali ndio yanatoka necta ,mbaya zaidi walimu wanawasisitiza ,.

Usiwe mjinga kuelewa mambo yanayoendelea huko ...

Wananunua mtihani ,pamoja na kuwa na mazingira mazuri ya kusomea ,walimu wazuri ,malazi ,na ufundishaji mzuri ....wananunua mtihani mkuu ....
Mkuu si kweli...naweza kukupa mfano....somo la History nimelifundisha sana na kila nikifundisha natoa sample questions mwaka uliopita 2021 nilitunga maswali kumi cha ajabu maswali matatu ya essay yalikuja kama nilivyotunga..
Je,nami nimeiba mtihani?
 
Mimi nimesoma chuo na watoto wanaotoka hizo shule mkuu ...

Siku ya mtihani wanakutana na maswali waliyokuwa wanasolve mwezi mmoja kabla ya necta ...

Sio kwamba siku ya mtihani wanasoviwa hapa ,ila pepar linasoviwa week kadhaa kbala ya necta na hayo maswali ndio yanatoka necta ,mbaya zaidi walimu wanawasisitiza ,.

Usiwe mjinga kuelewa mambo yanayoendelea huko ...

Wananunua mtihani ,pamoja na kuwa na mazingira mazuri ya kusomea ,walimu wazuri ,malazi ,na ufundishaji mzuri ....wananunua mtihani mkuu ....
Wananunua kwa nani na wengine wanunue
 
Mimi binafsi nakataaa hayo matokeo aisee ,hata kama Wana akili huo ufaulu wa kiasi hicho Kuna kitu cha ziada ...hio shule ichunguzwe vzuri kuanzia miezi mitatu kabla ya kufanya mtihani na siku za mitihani
Hahahh.mkuu hvo vtu vya kawaida..sis wenyew darasa letu form 4 kulikua na 1 zote halaf 2 zilkua mbili...its a seminary..ni hivi...kutoka darasa la saba kwenda form 1 tulipigwa mchujo mkali haijawai tokea..wanafunz wa interview walikua kamaa 4000..halaf tukachkuliwa 35 pekee..sasa lile darasa letu ilikua ukiangalia kila mtu alifaulu darasa la saba shule za vipaj karib weng yaan kat ya hao 35 tuliochaguliwa...sasa unategemea nin mkuu hapo form 4...tena hzo two hao jamaa walipigwgwa suspension miez miwil kabla ya nekta...hahah..mkuu..hyo ni form 4 ya 2006
 
Imagine wa kwanza sijui nan itakua labda ana 1.7 zote🤣🤣🤣🤣
Yaani hapo inatakiwa kuangalia maksi zao,unaangalia wote waliopata 100 kwa100,ukikosa unashuka 99.9 ivyo ivyo ila mwisho wa siku wakigongana wengi na unahitaji kumpata mmoja basi wanaishia kuangalia nani mwenye hati nzuri,ama nani kwenye njia alikosea alitumia njia nyepesi....mfano wa ivyo labda
 
Hivi pale St Francis Girls Mbeya, pana siri gani wazee? Mwaka huu licha ya kwamba imekua ya pili kitaifa lakini ufaulu wake ni wa ajabu na kuogofya sana.

Picha linaanza darasa lina watahiniwa 92 ambao wote wamepata div 1, hii si ajabu sana ajabu ni hili hapa kati ya hizo 1- 92, div 1.7 ambazo ndo ufaulu wa juu kabisa nchi hii kwa upande wa olevel zipo 79 yani 1.7 pale St Francis Girls zipo 79 kama utapata shida kuelewa na maanisha hivi wanafunzi waliopta A saba kwenye jumla la masomo yao wapo 79.

Mwanafunzi wa mwisho pale yani mwenye ufaulu dhaifu au unaweza kuuita goigoi ama kilaza, mmoja ana div 1.14 na mwingine ana div 1.13 na wapo wawili pekee.


Mabinti wamejua kukung'uta aisee div 1.10 ipo moja, 1.9 zipo 6 na 1.8 zipo 4


Kama unadhani maajabu yao mwaka huu ni hayo tu basi Pole mabinti hawa wameendeleza maajabu mpaka kwenye Wanafunzi bora ambapo kumi bora imepambwa na wao.Hatari sana hii mwanafunzi 1-5 kwenye kumi bora anatoka kwao afu wanajichomeka others kwenye 6,kisha namba 7 wanarudi wao afu 8,9 wanajikongoja fedha na ilboru kisha kumi kitabe kabisa wanamaliza wao.Kifupi 10 bora wanafunzi 7 wote wametoka St FRANCIS.

1. Consolata Prosper Luguva - St. Francis Mbeya🔴

2. Butoi Ernest Kangaza - St. Francis🔴

3. Wllhemia Steven - St. Francis 🔴

4. Cronel John - St Francis🔴

5. Merry George Ngoso - St Francis🔴

6. Holly Beda Lyimo - Bright Future
Girls🔴

7. Brandina - St. Francis🔴

8. Imamu Suleiman - Feza Boys

9. Mfalme Hamis Madili - Ilboru

10. Clara Straton - St. Francis🔴


Huu ufauru si wa kitoto sasa nauliza siri yao hasa ni ipi maana tangu miaka hiyo hawa mabinti wamekua moto ina maana shule zingine wameshindwa kabisa kujifunza?

View attachment 2082037

View attachment 2082038
Namkumbuka girlfriend wangu, alikua anasoma hii shule. Alikua na akili za kuelewa haraka mpaka nikawa namshangaa. Alipoenda kusoma University Ulaya ukawa ndiyo mwisho wa mahuasiano yetu.
 
Back
Top Bottom