St. Francis Mbeya kuna siri gani?

Nyie ndo wachawi wenyewe, ulishawahi kufika shuleni ukaona wanavofundisha?
 
Una matatizo mengi sana
 
Alinikubali tu the way I am.
Ila hawa watu uwezo wanao, nakumbuka chuo nilisoma na kijana mmoja kutoka kibaha ule moto hapana mtu aliyepata division one ya saba ama division one ya tatu muogope hata kama ni ya mchongo, uwezo wao huwa upo juu sana.

Hivyo nakubaliana na wewe kuhusiana na huyo binti uelewa wake ulivyokuwa juu, wakishika kitu hawasahau kabisa.
 
St. Francis ni sawa na vipaji maalum kwa shule za binafsi, kwasababu wanaopita interview karibia wote wamechaguliwa vipaji maalum. Ukiwafundisha kwa spoon feed wanakua moto zaidi.

Hawa watu wako vizuri sana, kinachowafelisha mbeleni ni ujifunzaji mpya. Nakumbuka niko form 4 nafanya mitihani ya jumamosi ya kitaa akaja dogo wa Maua Seminary wa form 3 akawa anafanya mitihani ya form 4. Alitukimbiza mpaka likizo inaisha.
 
Hii hoja yako ni dhaifu coz kama issue ni ada kubwa na wana fedha za kuwawezesha kununua mitihani kwa nini isiwe kwa shule nyingine? Hivi unajua Kuna shule ada ni between milioni 10 - 40? International schools ada mpaka milioni 70... Hebu tujifunze ku appreciate kazi nzuri na commitment kwa hii shule..
 
Wewe mwl unaonekana kilaza.
 
Nina jirani yangu huwa kila mwaka anashiriki kusahihisha mitihani for more than 10 years now, nimemuonyesha hii comment yako amesema hilo haliwezekani.
 
Hakuna Siri yoyote ,wale Wanachaguua watoto wenye vipaji tangu Form One Sasa unategemea nini?
HaO wote wakienda A Level wanakula sambamba na watoto wa Mpiga Miti Sekondari ya Newala
Vipaji wapiiii.. Acheni uzumbukuku na matokeo ya kununua au kuonyesha majibu watoto ktk mitihani
 
Ada yao unaijua? Watoto wanavyopatikana unajua? Mazingira yao unayajua? Kama haujui kaa kimya. Shule ya binafsi kuwa na ada ya 2.3m ni kawaida. Shule ngapi zina ada ya zaidi ya 3.5 zinashindwa kutoa matokeo? Wewe peleka mtoto wako huko unakodhani hawanunui mitihani akuletee makalai na D za kumwaga.
 
Kipindi cha magufuli kipi twende ya mwaka 2020 tu hapo. Mbona ilikua na 1 tupu na zote single digit na ilikua ya kwanza kitaifa
 
Nilitaka nikomenti mkuu naona nlichelewa, SINA CHA KUONGEZA.
 
Shule ya St. Francis's ni nzuri sana...yaani Yale Mazingira mtoto anafelije? Uwezo wa Wanafunzi ni mkubwa sana kwenye ile shule unakutana na katoto kako form II Ila kanajibu maswali Kwa kujiamini
Hata vyuoni uwezo wao ni mkubwa tu wachahe wanajisahau Ila wanauwezoa Sana.
Kuna wawili nawajua wamesoma pale Leo ni Madaktari Bingwa Pale Moi.
 
Kufaulu hiyp mitihani sio kitu cha ajabu kabisa. Nawashangaa hata wanaodhani kua shule inanunua mitiani.

Maswali huwa hayabadili saana, mwalimu akikomaa na past papers ni rahisi kufaulisha namna hiyo.

Mtu unajua kabisa section A inatoa maswali kuhusu hiki na kile, section B ni mada hizi na hizi hivi kweli ushindwe kupasua ukiwa makini.

Wanajituma acha wafaulu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…