St. Francis Mbeya kuna siri gani?

St. Francis Mbeya kuna siri gani?

Mimi binafsi nakataaa hayo matokeo aisee ,hata kama Wana akili huo ufaulu wa kiasi hicho Kuna kitu cha ziada ...hio shule ichunguzwe vzuri kuanzia miezi mitatu kabla ya kufanya mtihani na siku za mitihani
Mimi nadhani ingekua bora zaidi kwenda kujifunza wanafanyaje wanafunzi wao wanafaulu vizuri. Fatilia historia, hawajaanza kufaulu leo. Wengine waende kujifunza watoto wetu pia wafanye vizuri SIO Kuanza kutafuta kasoro.
 
Kama unataka kuaamini, baada ya kumaliza huo mtihani, wachukue hao watoto watungue paper la standard ya kawaida tu, then wape uone kama hao watoto wote 97 wanaweza kupata one ya point 7.....

Unajua div 1.7 wewe ,yaani watoto wote hao wapate A 7 kwenye masomo yao?????.....

Hao watoto ni weupe mno ,believe me, ni vile tu hata advance wanapelekwa shule za aina hio hio ,Bado vyuoni wanaenda kupotea kwani hawaoneshagi uwezo huo kabisa ,wanaishia gpa za 2.3 na supp juu😂😂😂😂

Big no
 
Mitihani ya siku hizi hamna kitu 1. Rais wa kwanza wa Tanzania ni nyerer......... 2. Binadamu ana macho mawi.......
Maswali mepesi lakini mbona wanafunzi wengine kule Kazulamimba wanafeli? Hawa watoe strategies tujue wengine waige vipi. Inaniuma kuona karne hii wanafunzi wanashindwa kufaulu hata kidato cha nne. Kuna jamaa yangu alifeli form 2 nilisoma name shule moja ya ajabu ajabu uko. Juzi akanambia eti daktari alivyompima akamwambia anaumwa ugonjwa unaitwa "INFECTIONS", nikamuuliza mara mbili na akasisitiza sana.

Sasa taifa linakuwa na watu wa hivi hata kutumia mbolea shambani hawataweza, lishe kwa watoto hawawezi, uzalishaji wao kitaifa ni duni. Shule walienda kuishi, kuvaa sweta na kunywa uji. Elimu ya bongo hasa uswahilini uko ni ile wazazi wanawaambia watoto wao wakiwa wamefunga eti "mmetuchosha hebu shule zifunguliwe wazazi tupumzike". Hapo usitegemee maajabu ya kufaulu. Sasa hawa waliofaulu wangetoa strategies imekuwaje ingesaidia wengine
 
Mimi nadhani ingekua bora zaidi kwenda kujifunza wanafanyaje wanafunzi wao wanafaulu vizuri. Fatilia historia, hawajaanza kufaulu leo. Wengine waende kujifunza watoto wetu pia wafanye vizuri SIO Kuanza kutafuta kasoro.

Mkuu hakuna ufaulu wa namna hio ,kwa hio ratio ....

Hapo ni wazi kabisa wamenunua mtihani na kusolve ...

Hakuna kitu kama hicho ,watoto wa kitanzania Mimi nawajua ,kuapata div 1.7 kaa watoto wote sio kwa uwezo wao ,japo wenye uwezo wapo lakin sio kwa hio idadi kabisa ...


Mimi nakataa kabisa 🤣
 
Wameongoza KEMEBOS huyu muhaya anakuja juu si mchezo, Bwire naona kwa ALLIANCE alishindwa kabisa kumaintain
Mwaka huu tu ndio wametolewa hapo na shule ambayo inamilikiwa na JK, all in all hiyo shule bado iko njema angalia hata idadi ya walioingia 10 bora ni hatari tupu.
 
St. Francis Mbeya ni kawaida yao. Ufaulu wao haujaanza jana wala leo.

Kwanza unakuta topic za form 4 walishazimaliza wakiwa form 3. Wakiingia form 4 ni kujifunza jinsi ya kujibu mitihani kwa kufanya past papers. Likizo hamna kwenda na madaftari wala hamna kusoma tuition.
 
Mkuu shule za kata ....ni mbaya...hebu fikiria mwanafunzi hajui kingereza lugha rasmi ya kufundishia ataelewa ya kwenye vitabu kweli?
Mwalimu hajui hata anafundisha nini. Mwalimu wangu wa fizikia alikuwa hajui vitu mpaka nikawa najiuliza unakuwaje mwalimu hujui unachofundisha?

Sasa kwa hali hii ukiwa kata utachomoa kweli?
 
Sio kwamba hawafundishi ila naomba kujua data kama tatu:-

Wote walioingia walikuwa na Passmark kiasi gani (creme de la cream)
Michujo ilifanyika kiasi gani (yaani potential failures wote kuondolewa)
Ufundishaji mzuri na kulenga mitihani (sijajua uelewa wa hawa vijana wala thinking capacity yao ila Mitihani hii ilivyo unaweza ulenga mitihani kwa kukariri hata kama thinking capacity yako ni ndogo)

Kwahio binafsi ubora wa shule naupima kwa mtu kumtoa point A kwenda B; bila mchujo wala kuchagua wanaojiweza pekee..., kama mtu amekuja hajui kitu na after four years akapata hata three huenda shule hio imefanya kazi kuliko kuchukua the best na katika hao best wale wote ambao ni better kuwabakisha madarasa (hio haijengi sababu hata Div 1 mpaka Three kwa form four bado ni ufaulu na kuna a long way forward na kuna a room for improvement
 
Back
Top Bottom