St. Francis Mbeya kuna siri gani?

St. Francis Mbeya kuna siri gani?

Hivi pale St. Francis Girls Mbeya pana siri gani wazee? Mwaka huu licha ya kwamba imekuwa ya pili kitaifa lakini ufaulu wake ni wa ajabu na kuogofya sana.

Picha linaanza darasa lina watahiniwa 92 ambao wote wamepata div 1, hii si ajabu sana ajabu ni hili hapa kati ya hizo 1- 92, div 1.7 ambazo ndo ufaulu wa juu kabisa nchi hii kwa upande wa olevel zipo 79 yani 1.7 pale St Francis Girls zipo 79 kama utapata shida kuelewa na maanisha hivi wanafunzi waliopta A saba kwenye jumla la masomo yao wapo 79.

Mwanafunzi wa mwisho pale yani mwenye ufaulu dhaifu au unaweza kuuita goigoi ama kilaza, mmoja ana div 1.14 na mwingine ana div 1.13 na wapo wawili pekee.

Mabinti wamejua kukung'uta aisee div 1.10 ipo moja, 1.9 zipo 6 na 1.8 zipo 4

Kama unadhani maajabu yao mwaka huu ni hayo tu basi Pole mabinti hawa wameendeleza maajabu mpaka kwenye Wanafunzi bora ambapo kumi bora imepambwa na wao.Hatari sana hii mwanafunzi 1-5 kwenye kumi bora anatoka kwao afu wanajichomeka others kwenye 6,kisha namba 7 wanarudi wao afu 8,9 wanajikongoja fedha na ilboru kisha kumi kitabe kabisa wanamaliza wao. Kifupi 10 bora wanafunzi 7 wote wametoka St FRANCIS.

1. Consolata Prosper Luguva - St. Francis Mbeya[emoji837]

2. Butoi Ernest Kangaza - St. Francis[emoji837]

3. Wllhemia Steven - St. Francis [emoji837]

4. Cronel John - St Francis[emoji837]

5. Merry George Ngoso - St Francis[emoji837]

6. Holly Beda Lyimo - Bright Future
Girls[emoji837]

7. Brandina - St. Francis[emoji837]

8. Imamu Suleiman - Feza Boys

9. Mfalme Hamis Madili - Ilboru

10. Clara Straton - St. Francis[emoji837]

Huu ufaulu si wa kitoto, sasa nauliza siri yao hasa ni ipi maana tangu miaka hiyo hawa mabinti wamekuwa moto ina maana shule zingine wameshindwa kabisa kujifunza?

View attachment 2082037

View attachment 2082038

Ushawahi pata wasaa wa kuhudhuria interview zao kwa ajiri ya selection?! Nikutaarifu tu hao 92 wanatokana na watoto zaidi ya 500 katika interview ya mchuzo sasa ! So obviously wanapata watoto cream wao kazi yao kuwasimamia tu! Halafu mwisho wa siku NECTA inakuja toa mtihani sawa na hawa wa Mpelangwasi sec school?! Unfair
 
Kama unataka kuaamini, baada ya kumaliza huo mtihani, wachukue hao watoto watungue paper la standard ya kawaida tu, then wape uone kama hao watoto wote 97 wanaweza kupata one ya point 7.....

Unajua div 1.7 wewe ,yaani watoto wote hao wapate A 7 kwenye masomo yao?????.....

Hao watoto ni weupe mno ,believe me, ni vile tu hata advance wanapelekwa shule za aina hio hio ,Bado vyuoni wanaenda kupotea kwani hawaoneshagi uwezo huo kabisa ,wanaishia gpa za 2.3 na supp juu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Big no
Fuatilia msichana aliyeongoza kwa GPA UDSM mwaka jana.. halafu uje useme alisoma shule gani o level na advance
 
Hayapa ni matokeo yao ya 2003 takribani miaka kumi 19 iliyopita walikuwa wana one za saba Kama tano hapo.
View attachment 2084109
Hayapa ni matokeo yao ya 2006 takribani miaka 15 iliyopita walikuwa na one za saba zipo Kama nane hivi na hichi ni Kipindi ambacho kulikuwa hakuna shule zenu za kata na Elimu ilikuwa bado ngumu

ilibidi nifanye uandakava, nikazama social media kuwatafuta hao wadada waliopiga division one mwaka 2003.

baadhi yao nimewakuta instagram, ni watu wazima kwa sasa na wengine wameolewa.

wote wapo vizuri kimaisha, kurasa zao za social media hazidanganyi, wengine ni wanasheria, wachumi, wahandisi na madaktari wa kutegemewa ktk hospitali wanazofanyia kazi.

jamani tusibeze elimu ya saint francis, hakuna binti anayepita hiyo shule halafu akawa kilaza mtaani.
 
St. Francis Mbeya ni kawaida yao. Ufaulu wao haujaanza jana wala leo.

Kwanza unakuta topic za form 4 walishazimaliza wakiwa form 3. Wakiingia form 4 ni kujifunza jinsi ya kujibu mitihani kwa kufanya past papers. Likizo hamna kwenda na madaftari wala hamna kusoma tuition.
Hii ya likizo hamna kwenda na daftari nimeisikia,lengo au fairs yake ni nini?
 
Ila msisahau maisha yanaegemea Sana kwenye bahati kuliko juhudi
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]nimesoma hapo funny thing toka enzi zetu wa mwisho alikuwa na 2 ya mwanzo
Hatukuwahi kuletewa mtihani wala majibu
Ila niwashauri tu Kama mnataka shule nyingine ziperform kama hivyo nendeni mkae week moja tu mtajifunza kitu
Hakuna uchawi wowote ni kitabu na sala kwa sana
Nilikuwa nasali jamani nusu niwe sister na mimi [emoji2]
Kweli usome St Francis usijue uandishi wa sentensi ?!. Huna cha herufi kubwa, koma wala nukta !!. Halafu lugha upate 'A'

Acha kutafuta misifa
 
Hio shule inanunua mitihani na kufanya mwezi mmoja kabla ya mitihani ya taifa na huwa maswali yanarudiwa kwa msisitizo mkubwa Sana ......

Hao watoto wanaomaliza huko hawana uwezo kabisa wa kufaulu hivyo, never ever....

Hapa bongo ukishakuwa na pesa hakuna kinachoshindikana, paper za NECTA zinanunuliwa na watoto Wana solve mapema kabisa ...

Hio shule ada yake tu unaweza kula mwaka mzima ,kununua pepar wizaran kupitia kwa mamuruki ni kitu rahisi Sana .....mbaya zaidi wafanyakazi wengi wa serikali dawa yao ni pesa ,kwa million 20 anakuletea pepar la necta lotee mwezi mmoja kabla .....


Niamaini Mimi haya nayoyasema

unaijua Ada ya St. Francis au unaongea tu? ni sh ngapi? eti unaweza kula mwaka mzima usiongee kitu usichokijua ada yao ya kawaida sana ndiyo maana watu huwa wanaikimbilia sema wanakosa sababu mtoto lazima awe vizuri kichwani.


Watanzania tuna roho mbaya sana hatupendi kuona mtu anafanikiwa wala kufanya vizuri!!! umekomaliiia kuongea uongo, jistukie na ona aibu!!!
 
unaijua Ada ya St. Francis au unaongea tu? ni sh ngapi? eti unaweza kula mwaka mzima usiongee kitu usichokijua ada yao ya kawaida sana ndiyo maana watu huwa wanaikimbilia sema wanakosa sababu mtoto lazima awe vizuri kichwani.


Watanzania tuna roho mbaya sana hatupendi kuona mtu anafanikiwa wala kufanya vizuri!!! umekomaliiia kuongea uongo, jistukie na ona aibu!!!
Hahaaa hizo ni division one za michongo tu ....
 
Hebu check wakati wa jpm matokeo Yao yalikuwaje Mana jamaa Alibana Sana wizi wa mitihani.
Shule za serikali zikaenda juu Sana.
Nimeshawahi kupiga tempo shule moja private nayo inawika hivyo2.
Nilikuwa nawafundisha advance physics jinsi ambavyo nilikuwa napitia Pepa zao za shule ni vilaza ama ni kawaida Ila mtihani ukija wanakuwa na maksi nzuri.
Ila jinsi unavyotoa quiz ubaoni wanavyosovu hata Ile interaction wanavyo respond unawacheck uwezo wao mkuu. So Kama mtu mzima unajijumlisha
Wewe Mbona muongo hivyo??. Rekodi si zipo Mzee??.Leta ushahidi hapa.
 
Sikusoma hapo. Nilisoma na wanafunzi wa Alevel waliosoma hapo. Walikuwa na div 1 za 14 lakini wote walikuwa weupeee ndani. Sijawahi kuona mtu anatoka shule inafaulu wakawa weupe kichwani kiasi hicho. Walituelezea shule yao kwa undani na tulishangaa sana.
Hapo kabla kuna ndugu yetu alianza kusoma hapo. Alichotuelezea mhmmm. Alihamishwa fastaa.
Ulisoma nao shule ipi huko A-level??.
 
Maandalizi ndio kila kitu wabongo wengi kwa bahati mbaya hupenda zimamoto na kutegemea matokeo yawe mazuri.
 
Back
Top Bottom