St George v/s Al Hilal naona Al hilal wanayo quality ya wachezaji lakini hawana timu, washakula 2 bila mpaka sasa

St George v/s Al Hilal naona Al hilal wanayo quality ya wachezaji lakini hawana timu, washakula 2 bila mpaka sasa

Mtanzanias

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2021
Posts
1,747
Reaction score
3,725
Nafikiri kwa timu yoyote itayovuka kati ya hizi kukutana na yanga basi itatakiwa ifanye kazi ya ziada mara 2 kuizuia yanga, naangalia mechi yao hapa inayoendelea sijaona timu ya kuisumbua yanga, Al Hilal wanao wachezaji wazuri lakini wanakosa muunganiko kila mchezaji anacheza kwa uwezo binafsi na sio kitimu, na ndicho kilichowagharimu mpaka sasa wako nyuma kwa goli 2 bila, St George tuliyoiona ikicheza na Simba hapa Tanzania mechi ya kirafiki naiona ni ile ile akuna kilichobadilika wamefanikiwa kuwaduwaza Al hilal kwa kutumia mapungufu waliyonayo ya kutokuwa na muunganiko, Nawaona st george awana washambuliaji hatari aina ya mayele kitu ambacho safu ya ulinzi ya yanga haitokuwa na kazi ngumu ya kufanya, yote kwa yote najua tiyali kuna shushushu wa yanga ndani ya dimba pale ethiopia akifuatilia kwa ukaribu mechi hii na ninamuona kocha Nabi akifanya home work yake vizuri sana kuelekea mechi dhidi ya wapinzani wake hawa
 
Wamefanya uzembe sana kuruhusu goli la away halafu dakika za mwishoni. Yanga wana timu nzuri ila kuna kitu wanakosa labda wajirekebisha. Kocha + wachezaji + uongozi wanatakiwa wayape asilimia kubwa haya mashindano kufika hata robo fainali tu. Waanze kujengwa kisaikolojia ili wajitoe. Jana watu wanapewa madodo na timu pinzani wana mbwela halafu jitu linacheka cheka kwa ujinga alilofanya.
 
Hili goli la ugenini limeongeza mlima kwa joji
Kwa nilivyowaona Al hilal kitachoendelea kuwatesa ni muunganiko ata kwao st george inaweza kupata goli pia wasipojirekebisha
 
Wamefanya uzembe sana kuruhusu goli la away halafu dakika za mwishoni. Yanga wana timu nzuri ila kuna kitu wanakosa labda wajirekebisha. Kocha + wachezaji + uongozi wanatakiwa wayape asilimia kubwa haya mashindano kufika hata robo fainali tu. Waanze kujengwa kisaikolojia ili wajitoe. Jana watu wanapewa madodo na timu pinzani wana mbwela halafu jitu linacheka cheka kwa ujinga alilofanya.
Hivi robo fainali unaijua au unaisikia. Kwa vile simba amefanya hivyo na yanga unaona wanaweza?
 
Kwa nilivyowaona Al hilal kitachoendelea kuwatesa ni muunganiko ata kwao st george inaweza kupata goli pia wasipojirekebisha
Nitafurahi sana timu zetu zote zikifika hatua ya makundi.
 
Hivi robo fainali unaijua au unaisikia. Kwa vile simba amefanya hivyo na yanga unaona wanaweza?
Sasa kama wewe ulifika robo kwa timu yako iyo ya kuungaunga itakuwaje yanga ishindwe inayokuzidi ubora kila eneo!! Ebu leta sababu za msingi hapa zitakazofanya yanga ishindwe kufika alafu wewe na timu yako iyo ya trip shamba trip gereji ndo ifike ebu tueleze
 
Vyovyote itakavyokuwa..mmoja hapo ni mchumba wa mtu..bado ndoa tu.
 
Hata wakipigwa 1 bila biashara imeisha
Kuna mburula mmoja anafikiri kimataifa nikucheza Kama unacheza na Azam fc, kimataifa ni mipango na malengo, kwa akili yake ibenge anaweza tolewa hatua za awali kweli, labda Prof yule aliyekuwa Al merrikh akala 4 kwa mkapa
 
Back
Top Bottom