St.Kayumba wote tukutane hapa Wazee wa kidumu na Maji

hahahahaa bakora vipi mkuu enzi hizo, Sisi wengine wa 90s niliwahi kula bakora ya mgongo hadi mkono na mgongo vikaganda kwa muda nikajua nakufa. Hujo Mwalimu alihamia kutoka International akakuta watoto wa uswazi kelele ndio ilikuwa chanzo....
Kuhusu suala la viboko asee, acha tu! Nakumbuka kuna mwalimu mmoja alihamia shuleni kwetu tukiwa darasa la sita, akawa mwalimu mkuu. Huyu mwalimu kabla hajaamia alipewa sifa shule yetu ina "manunda sana" sasa akaja na fimbo zake mbili.

1. Inaitwa "zima kibatari", wakuu hii ukitwishwa huamki mpk hata dakika moja ipite, au zaidi.
Hafu huyu "ticha" alikuwa kashiba, mbavu, na kaenda hewani. Na hii hata kama alikuwa amekasirika sana, atapiga mwisho mbili tu, akizidisha lazima unye[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji24] [emoji24] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji119] [emoji119] [emoji119]

2.Iliitwa "tamba uone boko kuna nini". Hii ilikuwa ni ya mkanda mithili ya ile mikanda inayozungushiwa mitambo ile ya mashine za kusagia mawe. Hii ukitwishwa maumivu yake yalikuwa hayasimuliki. Na hii alikuwa anaitumia mara chache sana. Hii ilikuwa inachana mpaka makalio.

Halafu akimaliza kugawa "doso" anawafolenisha na kuanza kuwaimbisha nyimbo za dhihaka, mkizunguka shule nzima. Kwa mfano kosa likiwa ni kutokana na kupiga kelele, atawaimbisha "Boko ina wenyewe, kelele si jadi yetu[emoji445] [emoji445] [emoji444] [emoji445] [emoji444] .
Heshima sana kwako
mwl. Chambo, (sasa hivi ni afisa elimu wilaya x)
 
ninacho kumbuka sikuwahi kudeki vyooni kwa muda wote niliokuws shule ya msingi! ila nilikuwa mkuu wa bustani za maua na mbogamboga!
ila pamoja na cheo hicho pia sikuwahi pewa au onja chochote cha kwenye bustani hizo!
 
Hahahahaa Mwal noma sana huyo...
Mimi nakumbuka darasa la tano nilikuwa nadaiwa ADA 3000. Mwal mkuu tena tulikuwa tunakaa nae mtaa mmoja. alikuja na fimbo nene kama bomba la nchi tatu ili atukomoe wadaiwa sugu. Sasa sisi tukawa tunamwambia akamdai mzazi sisi hatuusiki. Hapo ilikuwa ni Moja ya nguvu unaunga hadi nyumbani.
Nimegundua wale walimu tulikuwa tunawachosha sana...
 
Tulikuwa tunawachosha mno, na ndio maana hata wakati mwingine walikuwa wanaomba "collabo"
 
Hapo nipo darasa la sita, mimi ndo huyo niliejizungushia duara jekundu...nilikuwa na vituko Hatari, fkiria kwa hako kamwili nilikuwa navaa viatu vya mzee wangu huku nikijaradia nguo zaidi ya 4 kwa ajili ya kujikinga na fimbo..watu tumetoka mbali.
 

Attachments

  • 20170417_171625.jpg
    22.8 KB · Views: 28
Hapo nipo darasa la sita, mimi ndo huyo niliejizungushia duara jekundu...nilikuwa na vituko Hatari, fkiria kwa hako kamwili nilikuwa navaa viatu vya mzee wangu huku nikijaradia nguo zaidi ya 4 kwa ajili ya kujikinga na fimbo..watu tumetoka mbali.
Du aseee
 
St kayumba raha san kweli nimeamin wakati haurudi nyuma lait ningeambiwa kitu gani ungependa kijirudie maishan mwangu hakika ningejibu nirudie shule ya msingi ilikuwa rah san

Kwakweli[emoji2][emoji2]nakumbuka st kayumba kpnd cha kufunga shule lazma mzichapekuwahi namba na kidumu&fagio kunyolewa msalaba [emoji2][emoji2][emoji2]uwiiii now tumekua
 
Hapo nipo darasa la sita, mimi ndo huyo niliejizungushia duara jekundu...nilikuwa na vituko Hatari, fkiria kwa hako kamwili nilikuwa navaa viatu vya mzee wangu huku nikijaradia nguo zaidi ya 4 kwa ajili ya kujikinga na fimbo..watu tumetoka mbali.
mbona mlikuwa mmekomaa sana nyie,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…