St.Kayumba wote tukutane hapa Wazee wa kidumu na Maji

Dah mi kuwahi namba kulinitesa Sana aisee kilichokua kinanisave nisichapwe kwa vile nlikua mtoto wa mwalimu lol
Halaf nilikua natembea umbali mrefu kidogo kutoka home mpaka shule bila wasiwasi ,nashangaa sasa hivi eneo fupi tu mpaka nipande gari[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Na ile ya kuwa mtoro shule halafu wababe wa darasa wanatumwa kukufwata na kukuleta kwa nguvu, jamaa walikuwa na sifa sana, kwanza wana mbio balaa wakikuona utakamatika tu hata ifike jioni, ukifikishwa shule hizo bakora zake sasa...
 
Mimi huko nakumbuka tu kutongoza kwa tubarua, mwenye mwandiko mzuri ndio anapewa jibu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Sijui kwa hiki kizazi zikirudi hizi zama, itakuaje
 
Daaah kubebana na vidumu na ufagio kila siku za shule aisee
 
Darasa la NNE hyo.tupo darasani.sasa nje ya madarasa.kuna njia.wakapita wadada wawili wamevaa suruali.si. unajua tena tukaanza kupiga miruzi.oyaaaa nyie wadada wazurii.tumewapenda.n.k.Yukawa kama wapiga debe wa mansese kipindi kileeee.hamadi!wale wadada si wakageuza.wakaenda mpaka ofisini kutusemea kwa walimu.tulitamani ardhi ipasuke.siku hyo nakaa kwenye daladala kwenye bansen bana.makalio yanawaka motoo kwa bakora.za mwalimu aloyce.wa ukombozi mansese.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ,,, Mungu nae anaona aiseee……'!!!
 
Aisee umenikumbusha mbali. Mr chambo popote alipo Mungu ambariki..
Ile ni namba nyingine
Yupo Kinondoni hii hii, sasa hivi ni afisa elimu. Anaishi Mapinga, juzi kati nilikutana naye kwenye daladala wote tukiwa tunarudi kujipumzisha jioni.
JF raha sana mkuu kajojo
 
Uwiiiiiiiiiii nimecheka mpka watu wananishangaa [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
01.Walimu wa enzi hizo ni walimu
haswa walioshiba namkumbuka mwalimu wa nidhamu CHIEF KASHIKI 1978 leo hii amekuwa mzee sana 02. Ukiwa mtoro unafuatwa mpaka nyumbani kwa nguvu walikuwa wanaitwa LANDROVER 119 03 . Mchakamchaka na nyimbo zenyewe ni hizi
Jembe jembe jembe mama ninapolima nalima mwenyewe ninapovuna walaji wengi nk
walimu wa siku hizi vitoto zamani ni vizee lakini zingua uone utachezea vitasa mpaka ukumbuke viazi nyumbani nakumbuka mengi sana kwa shule hizi nilizosemea KARUMO PRIMARY SCHOOL ILEKANILO PRIMARY SCHOOL nikamishiwa IPANDIKILO PRIMARY SCHOOL 1979 ndiyo nahitimu
 
Tukiwa boarding school, mtoto wa form one amepokea bakuli la maharage kuangalia kuna wale wadudu wadogo dogo weusi wanaelea juu na mafuta, akayamwaga, tulimcheka sana, alilia wakati huo bado alikuwa na buscuit zake. Alipozoea alikua mtaalamu kweli wa kutoa wale wadudu kwa kijiko.
 
Tuna wazeee humu
 
Halafu kuna Ile Mnasubiria kengele ya kutoka darasan saa8 mnachungulia madirishan TImE kupa apige kengele halaf anakuwa na manjonjo huyo ILE AKIPIGA tu kengele kelele zake huzo Kunasiku Tulichalazwa stik siji sahau kisa kelele zile za saa8
…Acha hiyo ya kushangilia kengele, nakumbuk nlkua darasa la, tano sas muda wa mapumziko km kawaida kengel imegongw tukaanz kuishangilia,, kikapit kitot cha darasa la kwanza nyuma ya darasa letu kikapanda dirishani kikasema "yaani na nyie wakbwa ivo mnashangilia mapumziko?" ckuwai kuifikiria,kaul ya huyo mtot lkn nkiifkiria saiz najion mjinga hatari yan……!!!
 
Hahahahaah eti ili msishtukiwe kwamba mmeegezana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…