St.Kayumba wote tukutane hapa Wazee wa kidumu na Maji

St.Kayumba wote tukutane hapa Wazee wa kidumu na Maji

Wakuu nYie seMen yote MsalA kucHelewa MstaliN haLaf walimu wanachapa namba we ndo unafika unavohaha kwa kujificha KilA sehemU hUwa HaIkalikI Mbaya zaid ufumwe Na MatICha WaNoko wanaozunGuka kutaFuta wanafunz waliojificha Mbona Utaisoma namba ukifumwa[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tulikuwa tunaagizwa nyanya au machungwa darasa zima za kufundishiwa sehemu halafu anatumia nyanya moja tu zingine anaondoka nazo halafu tulikuwa fea sana hatuulizi wala nn
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hahaaa dah nimekumbuka form two somo la english kuna kitu kinaitwa tag questions nikikumbuka nacheka san shenti shiiiii?
Hizo hadi leo hii Niko chuo kikuu lakini bado naona hizo tag question ni kama mazingaombwe na miujiza[emoji2] [emoji2]
 
ilikuwa kila nikinunua fagio lazma niibiwe , basi nami nikaanza tabia ya kuchomoa chelewa kwa lola fagio la mtu anayezubaaa mpaka napata fagio kabisa.
Nakumbuka mvua ilkua ikinyesha kila nikipewa mwamvuli nyumban lazma nkaibiw so ikabd MAMA aache kunipa miamvul hata mvua inyeshe vip yan…!!
 
Kuhusu suala la viboko asee, acha tu! Nakumbuka kuna mwalimu mmoja alihamia shuleni kwetu tukiwa darasa la sita, akawa mwalimu mkuu. Huyu mwalimu kabla hajaamia alipewa sifa shule yetu ina "manunda sana" sasa akaja na fimbo zake mbili.

1. Inaitwa "zima kibatari", wakuu hii ukitwishwa huamki mpk hata dakika moja ipite, au zaidi.
Hafu huyu "ticha" alikuwa kashiba, mbavu, na kaenda hewani. Na hii hata kama alikuwa amekasirika sana, atapiga mwisho mbili tu, akizidisha lazima unye[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji24] [emoji24] [emoji85] [emoji85] [emoji85] [emoji119] [emoji119] [emoji119]

2.Iliitwa "tamba uone boko kuna nini". Hii ilikuwa ni ya mkanda mithili ya ile mikanda inayozungushiwa mitambo ile ya mashine za kusagia mawe. Hii ukitwishwa maumivu yake yalikuwa hayasimuliki. Na hii alikuwa anaitumia mara chache sana. Hii ilikuwa inachana mpaka makalio.

Halafu akimaliza kugawa "doso" anawafolenisha na kuanza kuwaimbisha nyimbo za dhihaka, mkizunguka shule nzima. Kwa mfano kosa likiwa ni kutokana na kupiga kelele, atawaimbisha "Boko ina wenyewe, kelele si jadi yetu[emoji445] [emoji445] [emoji444] [emoji445] [emoji444] .
Heshima sana kwako
mwl. Chambo, (sasa hivi ni afisa elimu wilaya x)

[emoji23] [emoji23] [emoji23] duh we jamaa umesoma boko nini, aisee jf ni kijiji
 
Halafu kuna Ile Mnasubiria kengele ya kutoka darasan saa8 mnachungulia madirishan TImE kupa apige kengele halaf anakuwa na manjonjo huyo ILE AKIPIGA tu kengele kelele zake huzo Kunasiku Tulichalazwa stik siji sahau kisa kelele zile za saa8
 
Kitu pekee nachokumbuka ni kwambaaaa..kubebeshwa kote kuni,mbolea,jembe,fagio,kwenda kafanya kazi om kwa mwalimu nk. Nlitoka kama nlivyoingia yan ckuambulia chochote akilini..cjui walikua wanafundisha kikorea
[emoji23] [emoji23] [emoji23] we umetisha ulikua unasindikiza wenzako
 
Hizo hadi leo hii Niko chuo kikuu lakini bado naona hizo tag question ni kama mazingaombwe na miujiza[emoji2] [emoji2]
Ukienda UDSM kuna jamaa mmoja anafundisha lile somo DS.
Yeye kila akiongea sentensi mbili lazima atupie Question tag. Isn't?
Umekuwa ugojwa wake kwa mara ya kwanza watu wanacheka balaa. Maana bila hiyo hawz kuongea
 
Hapo nipo darasa la sita, mimi ndo huyo niliejizungushia duara jekundu...nilikuwa na vituko Hatari, fkiria kwa hako kamwili nilikuwa navaa viatu vya mzee wangu huku nikijaradia nguo zaidi ya 4 kwa ajili ya kujikinga na fimbo..watu tumetoka mbali.
Kitambo iyo
 
St kayumba za dar earl2000 darasa la sita kwenda la saba kulikua na utaratibu wa kushindana kwenye mitihani inashirikisha shule nyingi,bwana ulikua ukifeli hizo stick zake balaa[emoji2][emoji2]mda wa kwenda mnashangilia makelele mpk mnafika

We unaongelea ya st kayumba za juzi tu mkuu
 
Nakumbka mkuu wa shule alikuwa mkali hujui kiinglish kaa kimya, ma monitor wanapewa vibao vimeandikwa " speak English " sasa jamaa mmoja akakerwa na mwenzake akaona hakuna namna inabidi ajibu mashambulizi akamwambia "you have population" akimaanisha unamasifa[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ukienda UDSM kuna jamaa mmoja anafundisha lile somo DS.
Yeye kila akiongea sentensi mbili lazima atupie Question tag. Isn'i it?
Umekuwa ugojwa wake kwa mara ya kwanza watu wanacheka balaa. Maana bila hiyo hawz kuongea
He is right, question tag is added at the end of the sentence or statement, 1.to see if the sentence is correct 2. It is used to ask guestion
 
Shule niliyosoma ilinifundisha stadi za kazi mapema nikiwa std5, nimebeba sana Matofali na viroba vya mchanga kwa kweli sitasahau imenifundisha kujua maisha mapema sana ingawa imenikomaza mpaka leo sirefuki lakini pesa si haba!
 
Back
Top Bottom