St.Kayumba wote tukutane hapa Wazee wa kidumu na Maji

Mmenimbusha kupiga chabo Yan English jaman Yan nikipewa pepa tu mi najua So.. that,, either... or na neither ... nor.. nimemaliza mtihani hizo ABC sasa mbona zilinikoma nilikuwa nakaa na mtoto mkali alikuwa anaitwa sophia anajua english balaa BAC MI NIKIPIGA JICHO MOJA nashameza abc za swali la 1-7 yan nukigeuka mara mbili tu nishafaulu mtihan RAHA SANA JAMAN CHABO YA PRIMARY TEH TEH[emoji28] [emoji4] [emoji4]
 
Mmenikumbusha nikiwa darasa la tano tulichaguliwa kwenda kusaga mahindi ya shule tukikuwa wavulana na wasichna, baada ya kupeleka mahindi mashine wakati yakisagwa sisi tkaenda mtoni kuogelea bahati mbaya mwalimu wetu wa hesabu akatuona, alochofanya akachukua nguo zetu akaenda nazo shuleni tukarudi na vichupi vyetu sa mwenzetu mmoja visenti sa hizi yupo UK alikuwa hajavaa chupi akarudi kajifunga majani ya mgomba..duu it was so funny ila tulipigwa na kulimishwa shamba la shule mwezi mzima.
 
Soksi za pundamilia zilikuwa maarufu na kibegi chako cha sport. Mimi shule niliyosoma umoja, imezungukwa na kota za jeshi mabibo, sasa usiombee umechelewa alafu umekuta wapo mstarini wanaimba, nyimbo ya taifa, alafu ww unajifanya mjanja unanyata ili usionekane, aiseeeeeeee siku hiyo utaimba aleluya.
 
Darasa la 1 & 2 hiyo, ukimaliza tu ile "Kwaheri Mwalimu kwaheeri, tutaonana keshooo..." hapo mbio huoni mtu, utaona tu mifuko ya Sports ikipepea mgongoni.
 
Hahahaah,kumbe bado yapo haya mambo,duh
yapo bdo yapo.mkuu,, yaan inaboa unakuta umeconcentrate na kusom class anakuja kiongoz kuwatoa mkazbue vyoo,, unatok class umemind utafny nn lkn lazm uend tuu…!!!
 
01.Walimu wa enzi hizo ni walimu
haswa walioshiba namkumbuka mwalimu wa nidhamu CHIEF KASHIKI 1978 leo hii amekuwa mzee sana 02. Ukiwa mtoro unafuatwa mpaka nyumbani kwa nguvu walikuwa wanaitwa LANDROVER 119 03 . Mchakamchaka na nyimbo zenyewe ni hizi
Jembe jembe jembe mama ninapolima nalima mwenyewe ninapovuna walaji wengi nk
walimu wa siku hizi vitoto zamani ni vizee lakini zingua uone utachezea vitasa mpaka ukumbuke viazi nyumbani nakumbuka mengi sana kwa shule hizi nilizosemea KARUMO PRIMARY SCHOOL ILEKANILO PRIMARY SCHOOL nikamishiwa IPANDIKILO PRIMARY SCHOOL 1979 ndiyo nahitimu

Heshima yako mkuu79 umehitimu primary si mchezo
 
Darasa la 1 & 2 hiyo, ukimaliza tu ile "Kwaheri Mwalimu kwaheeri, tutaonana keshooo..." hapo mbio huoni mtu, utaona tu mifuko ya Sports ikipepea mgongoni.

Jmn[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Mkuu daake 1979 ndiyo nahitimu darasa la saba IPANDIKILO PRIMARY SCHOOL MWAKA 1985 Huyu mkuu wa nchi tulikutana naye huko kwao alikuwa anachuuza samaki na dagaa na baiskeli yake aina SWALA NA TENGA sasa nashangaa jamaa kaula kama mzaha tu wakati ananizidi miaka miwili
 
Ndo hivyo ten alopewa kapewa
 
Mkuu daake 1979 ndiyo nahitimu darasa la saba IPANDIKILO PRIMARY SCHOOL MWAKA 1985 Huyu mkuu wa nchi tulikutana naye huko kwao alikuwa anachuuza samaki na dagaa na baiskeli yake aina SWALA NA TENGA sasa nashangaa jamaa kaula kama mzaha tu wakati ananizidi miaka miwili
Mmmh,,,shikamoo BABA……!!!
 
Nakumbuka enzi za darasa la sita, mpaka darasa la saba; kitu cha "tag question" ilikuwa balaa tupu.

"You took my pen"
"________________"
(Malizia mwenyewe)
Msondo ngoma ilikuwa na raha yake asee.
[emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Tooknt it..
 
Mkuu daake 1979 ndiyo nahitimu darasa la saba IPANDIKILO PRIMARY SCHOOL MWAKA 1985 Huyu mkuu wa nchi tulikutana naye huko kwao alikuwa anachuuza samaki na dagaa na baiskeli yake aina SWALA NA TENGA sasa nashangaa jamaa kaula kama mzaha tu wakati ananizidi miaka miwili
Hizo shule ziko maeneo gani. Safi sana mkulu inatakiwa akuite siku moja hapo magogoni angalau mtie story za zamani.
Heshima yako legend.
 
Uwiiiiiiiiiii nimecheka mpka watu wananishangaa [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
da mimi nakumbuka darasa la 2 na la 3... tulikuwa tunaimba table ya kwanza hadi ya 12...
 
Shule niliyosoma ilinifundisha stadi za kazi mapema nikiwa std5, nimebeba sana Matofali na viroba vya mchanga kwa kweli sitasahau imenifundisha kujua maisha mapema sana ingawa imenikomaza mpaka leo sirefuki lakini pesa si haba!
Umedumaa[emoji23] [emoji23]
 
Mmenikumbusha nikiwa darasa la tano tulichaguliwa kwenda kusaga mahindi ya shule tukikuwa wavulana na wasichna, baada ya kupeleka mahindi mashine wakati yakisagwa sisi tkaenda mtoni kuogelea bahati mbaya mwalimu wetu wa hesabu akatuona, alochofanya akachukua nguo zetu akaenda nazo shuleni tukarudi na vichupi vyetu sa mwenzetu mmoja visenti sa hizi yupo UK alikuwa hajavaa chupi akarudi kajifunga majani ya mgomba..duu it was so funny ila tulipigwa na kulimishwa shamba la shule mwezi mzima.
Aisee [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Darasa la 1 & 2 hiyo, ukimaliza tu ile "Kwaheri Mwalimu kwaheeri, tutaonana keshooo..." hapo mbio huoni mtu, utaona tu mifuko ya Sports ikipepea mgongoni.
Tena ukiwa wa asubuhi mkifika mlangoni unawaona wa mchana unawazomea
 
Back
Top Bottom