BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Emmanuel Myamba almaarufu Pastor Myamba; ni staa mkongwe wa Bongo Movies ambaye alikuwa muigizaji mwenza katika filamu nyingi za marehemu Steven Kanumba.
Pastor Myamba amedhibitisha kupata ajali mbaya wikiendi iliyopita ila wakapona bila majeraha mabaya. Pastor Myamba ambaye wengi wanamfahamu kwa kuigiza kama mchungaji au mhubiri katika filamu za Kanumba kwa sasa ni mhubiri wa Kanisa la House of Victory nchini Tanzania lenye makao yake makuu Dar es Salaam.
Pastor Myamba kama anavyojiita katika huduma ya Injili, huku akiambatanisha na picha ya gari hilo ameandika: "Tunamshukuru sana Mungu atulindaye na kutupa uzima siku zote, siku ya jana tukiwa tunatoka Mlima wa Maombi kuelekea kwenye ibada, mimi pamoja na familia yangu, tulipata ajali hiyo mbaya...
"Kwa jinsi Mungu alivyomwema sana kwetu, alituokoa sote na mauti na wote tu wazima sana hakuna hata aliyechubuka kwa jereha lolote. Tunamtukuza Mungu sana sana. Ungana nami, kumshukuru Mungu kwa ajili yangu na familia yangu."
Chanzo: Tanzaniaweb