Staa wa Bongo Muvi, Pastor Myamba apata ajali ya gari

Staa wa Bongo Muvi, Pastor Myamba apata ajali ya gari

Kesho utaambiwa movie mlima wa maombi imetoka.
Pole yao km kweli
 
Huyu jamaa nilikuwa nadhani ni mchungaji kweli.
Kumbe sikukosea.
 
𝐤𝐰𝐚 𝐦𝐚𝐬𝐚𝐧𝐣𝐚 𝐡𝐚𝐤𝐮𝐧𝐚 𝐬𝐚𝐝𝐚𝐤𝐚 𝐤𝐚𝐛𝐢𝐬𝐚
Lazima aache kuigiza kwani si unaona masanja na wengine sadaka sio mzaha
 
Haha..
Shem, kama waoaji wenyewe ndiyo kama hawa wa JF then am doomed..!!
Waoaji wapo, Jf ni zaidi ya mtaa ila walio serious wapo cool.
Nitakufundisha jinsi ya kumjua mtu aliye serious na ambae anakupenda kweli. Wanawake wengi hilo eneo ndio linawapa shida na huishia kuwa na majuto. Bible verses zipo za kila aina kukufundisha Ila wengi hawazijui au hawazielewi ila nitakufundisha na hautakuja kuumia tena au kuwa na mahusiano yasiyo sahihi
 
Emmanuel Myamba almaarufu Pastor Myamba; ni staa mkongwe wa Bongo Movies ambaye alikuwa muigizaji mwenza katika filamu nyingi za marehemu Steven Kanumba.

Pastor Myamba amedhibitisha kupata ajali mbaya wikiendi iliyopita ila wakapona bila majeraha mabaya. Pastor Myamba ambaye wengi wanamfahamu kwa kuigiza kama mchungaji au mhubiri katika filamu za Kanumba kwa sasa ni mhubiri wa Kanisa la House of Victory nchini Tanzania lenye makao yake makuu Dar es Salaam.

Pastor Myamba kama anavyojiita katika huduma ya Injili, huku akiambatanisha na picha ya gari hilo ameandika: "Tunamshukuru sana Mungu atulindaye na kutupa uzima siku zote, siku ya jana tukiwa tunatoka Mlima wa Maombi kuelekea kwenye ibada, mimi pamoja na familia yangu, tulipata ajali hiyo mbaya...

"Kwa jinsi Mungu alivyomwema sana kwetu, alituokoa sote na mauti na wote tu wazima sana hakuna hata aliyechubuka kwa jereha lolote. Tunamtukuza Mungu sana sana. Ungana nami, kumshukuru Mungu kwa ajili yangu na familia yangu."


View attachment 2159283

View attachment 2159314

Chanzo: Tanzaniaweb
Dhibiti...Dhibitisha. Kwahiyo hapo neno thibitisha badala ya Dhibitisha.
 
Back
Top Bottom