Kwa kauli hii sasa tunaanza kuelewana...maana kiburi na majivuno mlizidi mno na hasa baadhi ya viongozi wenu na magazeti yenu...kumbe sasa mnafahamu kuwa mpo hapa Tanzania...maana tambo zilizidi mno..mara sijui simba hii ni ya sayari nyingine, mara simba hii hata waje Barcelona au Man United, mara simba hii ni ya anga nyingine, mara simba hii Yanga mtapiwa nyingi, mara Simba wafanya kufuru Kongo wapangua hujuma zote, mara nyie Yanga saizi yenu sijui Stand United na Mbao na siyo Simba...kumbe wenzenu wakongo wanawasoma tu...in fact kwa maoni yangu hakuna timu rahisi kuifunga kama Simba...ina mafowadi watatu ambao ni wakali ambao ni Bocco, Okwi na Kagere...hawa hufunga mabao kwa kulishwa tu wao hawajui kutafuta...Okwi ni mviziaji hukaa peke yake , Kagere yeye ni mipira ya kutanulizziwa na vichwa, na Bocco ni opportunist kwa mipira inayozagaa...sasa wajanja wanakaba vyanzo vya pasi na Simba kwisha...hakuna cha Okwi, Bocco wala Kagere...