Nimefanikiwa kuona clip ya mkutano wa Makonda katika Wilaya ya Longido kwenye Shule ya Wasichana wa Mama Samia. Kwanza nimpongeze Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo kwa taarifa nzuri na matumizi mazuri ya fedha katika ujenzi wa shule hiyo. Staili ya Makonda katika ziara yake inatakiwa kukemewa. Kwanza, mtalaam anapoeleza mradi au suala linaloulizwa anatakiwa akae kimya mpaka mwisho wa maelezo ya suala husika. Kila mtalaam akiendelea kueleza yeye anaingilia kati kwa maswali yasiyokuwa na tija. Pili, udhalilishaji anoufanya kwa Wataalam unatakiwa kukemewa. Ziara zake nyingi anawadhalilisha watalaam mfano Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha, Meneja wa TARURA Mkoa wa Arusha na yule Dada aliyekuwa anatoa maelezo mazuri na kumueleza kuwa ana mke mzuri kuliko yeye. Hivi ni vitendo vinavyodhalilisha sana. Mpe nafasi mtalaam aeleze mpaka mwisho ndo uanze kumuuliza maswali na siyo kila mara kuingilia kati katika maelezo yake. Anayeteua tunakupa angalizo hili.