Stan Katabalo: Tunauhitaji mzimu wako wa habari za Uchunguzi!

Nakubaliana na wewe mkuu. Nakumbuka enzi za gazeti MOTOMOTO!

Jamani kuna mwandishi anhitwa Twaha Khalfani Jenerali Ulimwengu. Kwa kweli huyu naye ametoa mchango mkubwa kwenye tasnia ya habari..Of course kuna akina Ansebert Ngurumo lakini bado bado...Kama si uroho wa pesa akina Dr Shoo na Salva Rwey.. enzi za HCL walitia fora nao...Tunahitaji kizazi kipya cha uhandishi shime akina Ngurumo...
 
Nakubaliana na wewe mkuu. Nakumbuka enzi za gazeti MOTOMOTO!
there you are,but wengi hawalikumbuki hilo gazeti sababu walishalogwa na uhuru mzalendo na mfanyakazi kipindi hicho.naamini kama ni mpenzi wa riwaya unaikumbuka ya george mwakingili ikiitwa''kinywa cha mauti''r.i.p katabalo.wema hawatakuwa na amani katika ulimwengu huu.
 
Mkuu naikumbuka hiyo riwaya. Enzi hizo pia kulikuwepo na akina Charles Charles mwandishi ambaye naye sijui yupo ila makala zake zilikuwa moto wa kuotea mbali.
 
Namkumbuka stan katabalo huyu jamaa aliandika mengi lakini kilichotamba zaidi kipindi anaandikia gazeti la mfanyakazi,ambapo ulikua ukitaka gazeti la mfanyakazi unaambiwa ununue na uhuru(GAZET.)

Nakumbuka alikuwa kama mtabiri haya yanayotokea Loliondo kwa sasa; yeye aliyaona mwaka 1992. Alituahidi kutupa makala kumi mfululizo za kuhusu mkataba wa TBL aliandika MENO YA MAKABURU YAING"ATA TZ maskini baba wa watu akatutoka kabla hajatuelez yaliokuemo kwenye mkataba ule na nina imani kifo chake kikapelekea na kifo cha gazeti la mfanyakazi.

Sijui kuhusu mke wala watoto wala ndugu ila i alway miss him.

RIP KATABALO.
 
Namkumbuka kwa kuandika kuhusu kashfa ya LOLIONDO(Loliondo gate) kipindi hicho nilikuwa darasa la 3 mkuu.NILIPENDA KUSOMA MAKALA ZAKE NA HATA NILIPOSIKIA KIFO CHAKE SIKWENDA SHULE SIKU 3 KWA HUDHUNI

Hongera kwa kupenda kusoma gazeti ukiwa darasa la 3 maana miaka hii kusoma gazeti ni issue hata kwa watu wenye ufahamu wa kutosha, ukiona kanunua gazeti basi ni la udaku wenyewe wanayaita magazeti pendwa
 
Marehemu Stan Katabalo nilipenda sana kusoma makala yake,yeye ndiye mwandishi pekee aliyekua anaandika habari za kiupelelezi,nilisikitika sana kupata taarifa ya msiba wake,nilifunga kwa siku moja kama sehemu ya maombolezo.

Ila yaliyomkuta ni mambo ambayo huwaapata wandishi wengi wa aina yake duniani,na hata wakati wa utoaji wa makala yake siku zote nilikua nahofia sana maisha yake,RIP Shujaa Katabalo
 

Thats was a point ambapo Tasnia ya uandishi wa Habari katika Tanzania ilianza kuacha reli, kwani kila mwandishi alianza kujisafisha, kwa kujifanya 'a;imuonya marehemu ili aachane na suala lile' na walipoona hasikii eti walijitenga naye, walifanya matendo ya kupigania kuishi.

Ghafla Magazeti yakapoteza mwelekeo, Moto moto likapotoea, Shaba likapotea, Mfanyakaza likaanza kusua sua, Ujio wa Majira ukawa kama mkombozi wa Tasnia ya uandishi, Then yakaja mengi, lakini bado mpaka sasa tunaona pengo likiongezeaka japo kuna wachache wanaojaribu kuibuka lakini huhujumiwa na wenzao.

Im really sorry kwa Uandishi wa habar wa Tanzania.
 
 
 

Ninaweza nisiwe sahihi lakini kwa kuliangalia jina lake la pili (Katabalo), ni dhahiri alikuwa anatoka mkoa wa Kagera!!!

Tiba
 
Stan Katabalo alikuwa Mwandishi wa Gazeti la Mfanyakazi lililotolewa kila Jumamosi, na kweli aliuawa na kisa cha Loliondo-gate, na Charles Charles sasa hivi ni Mhariri wa Gazeti la Sauti ambalo lina mwelekeo wa CCM, na kuna wengine wanasema yupo ndani ya Ofisi hizo
R.I.P. Stan Katabalo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…