Huyo bwana ndiye aliyekuwa mhimiri wa kashfa ya Loliondo kabla ya kutolewa Wizara ya Utalii na kupelekwa kuwa RC Singida. Hivi siku hizi yuko wapi huyo Mgumia?
RIP Katabaro.....Namkumbuka sana jinsi alivyokuwa mwandishi mzuri sana na asiye na woga.
Wadau naomba pia mkumbuke jamaa mmoja anaitwa Anthony Ngaiza ambaye aliwahi kuwa editor wa Family Mirror kwenye miaka ya 1992/93 kabla ya kuhamia MCT. Tunahitaji kweli kuwakumbuka hawa jamaa!
Stan Katabaro alikuwa mwandishi mahiri sana, ninaposikia hii sekeseke ya Loliondo sasa hivi huwa namkumbuka. Abubakar Mgumia naye ni marehemu.
Je, mnakumbuka na ile kashfa ya RIO? Kwenye mkutano wa Mazingira Duniani ulifanyika BRAZIL (Rio de Janeiro)
Kwahakika hakuna kama STAN KATABALO.
Kashfa ya LOLIONDO ilimhusu sana sana ABUBAKAR MGUMIA......
Hii digitali ingekuwepo enzi hizo makala zote zingekuwepo lakini sasa hivi uki-google unapata info za above 2000Jamani mwenye nakala za mfanyakazi za issue ya loliondo tunaomba atuwekee
Namkumbuka kwa kuandika kuhusu kashfa ya LOLIONDO(Loliondo gate) kipindi hicho nilikuwa darasa la 3 mkuu.NILIPENDA KUSOMA MAKALA ZAKE NA HATA NILIPOSIKIA KIFO CHAKE SIKWENDA SHULE SIKU 3 KWA HUDHUNI
Hii digitali ingekuwepo enzi hizo makala zote zingekuwepo lakini sasa hivi uki-google unapata info za above 2000
nani anakumbuka issue ya lolionda gate. ukiijua hiyo vema utakuwa unamjua katabaro tunayemzungumza. alikauka ghafla mpaka wa leo watu makini wanasikitika jamani katabaro. where is he We miss him so much. R.I.P
Agoro Anduru (The Temptation) ni Marehemu pia (RIP)
Stan hawezi kulinganishwa na mwandishi yeyote katika hii decade 2000 - 2010! Kubenea, Mbwambo, e.t.c they are no where near - kumbuka kuwa wakati the so called "uhuru wa vyombo vya habari" ulikuwa mdogo sana!
RIP Stan K.
Kweli tumepotea kama Taifa tunahitaji kila mtu na familia yake ajenge uwezo watoto kusoma vitabu maana hizi audio-visual ni nzuri kwa mafunzo ila haziongezi uwezo wa ubongo kufikiria kwa kina kwa kuwa unasikiliza na kuona tofauti na kusoma lazima ita involve na kutafakari kwa kina, siku hizi ukisikia mtu anazungumzia vitabu utasikia ni vya watu wa nje, kweli long time tulikuwa tuna hazina ya waandishi wa simulizi siku hizi tumebaki na waandishi wetu wa story za kwenye magazeti ya rangirangi. Aisee Baba_Enock amenigusa na kitabu cha Temptation cha marehemu Agoro AnduruAgoro Anduru au Aggrey Andrew! This is living and other stories! Jamaa alikuwa mahiri sana. Mungu ampe pumziko la milele.
Makala zake kuzipata ni issue si unajua enzi zile ilikuwa ni analogy, but I think maktaba za taifa magazeti ya enzi hizo yatakuwepo unless kama huwa wanayateketeza baada ya miaka kadhaaKuna sehemu naweza kupata makala zake zote?
Namsikia tu, natamani nisome hizo makala zake