Stand up comedy: Comedian Deogratius ana kipaji hasa atafika mbali sana

Stand up comedy: Comedian Deogratius ana kipaji hasa atafika mbali sana

Yuko vizuri sana "in my book " halafu anajua kuimba
Hahahaha hiyo intro yake kwanza anaanza kwa kuimba kwanza, halafu anapenda nyimbo za Bongoflava na reggae

In my book
 
MC Jessey, Captain nani yule sijui, Chemutai, Eric Ormond hahahaaa hawa jamaa ni next level aisee..
Nikiwa na stress naingia zangu YouTube Churchill show, siku imeisha hiyo but comedians wa bongo ni kama wanatumia nguvu kubwa sana kuchekesha
 
MC Jessey, Captain nani yule sijui, Chemutai, Eric Ormond hahahaaa hawa jamaa ni next level aisee..
MC jessey? Mkuu hongera sana kama anakuhekesha.

Erick alianza vzr then akaanza kurudia ikaboa. Mdogo wake nae alipopata nafasi akawa anarudia ya kaka ake, sikufuatilia tena.

Prof Hammo anajua sana, Mca trick yuko good, kuna Njoroge pia nae si haba. Pia kuna creative generation, kuna jamaa ana jicho moja lina ulemavu na wale walevi wawili. Mwisho yupo sleepy David hawa ni miamba.

All in all Erick Omond ndiye alinifanya nikaijua churchill show. Mc pilipili enzi hizo ndiye nilikua namsifia kumbe hamna kitu.
 
M pia nilikua siwaelewagi wabongo ila kuna cheka tu audition iko poa wanajitahidi kwa mtazamo wangu....my favorite comedian n mc jessy jamaaa anajua.
 
Last week ilikua "Mbele za mademu" school ilikua ukiazibiwa mbele za mademu unakaza unajifanya stick haziumi unaonyesha umwamba, ukiadhibiwa mbele ya masela wenzio unalia kishenzi na kulalamika. Hata yesu alipoadhibiwa na pilato kwa kua kulikua na mademu alikaza, akabeba msalaba alipokua njiani akawaona wanawake akakaza akawaambia msinililie mimi lilieni vizazi vyenu na watoto ila alipotokea Simon Yesu akaanguka oyaaa simoni nisaidie msalaba mzito hahahahahahahahahah
Jamaa alinichekesha sana yani deo uwa ananichekesha sana jinsi anavyounga mambo yake na yakamake sense
 
Dunia ipo kwenye hali mbaya sana upande wa furaha. Watu hawana furaha kabisa. Kumeibuka wachekeshaji wengi mno ambao kwa hapa Bongo wanaboa kupitiliza. Idris Sultan ni mfano hai wa mchekeshaji anayelazimisha mambo ili tucheke.
 
Mkuu tumkazie, hamna kucheka!
 
Back
Top Bottom