Stand ya daladala Mbezi Louis imegeuzwa soko?

Stand ya daladala Mbezi Louis imegeuzwa soko?

DALALI MKUU

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2022
Posts
2,011
Reaction score
4,705
Ni jambo la kusikitisha sana Stand ya daladala Mbezi luis kugeuzwa soko, hasa nyakati za Jioni kuanzia saa 12 Jion na kuendelea.

Ukipita stand ya Mbezi luis kuanzia barabara ya kwenda Kinyerezi kunakuwa na foleni kubwa sana daldala haziingii ndani ya stand zinapaki na kushusha abiria njiani kwa sababu Wfanyabiashara wadogo wa Vyakula, matunda,nguo,viatu n.k hupanga bidhaa zako katiaka maeneo ambayo magari hutakiwa kusimama na kwenye vibanda vya kupumzikia abiria.

Watu hawana hata wasiwasi wanawasha Jiko la mkaa na kuni wanapikia kule stand, wakati kuna vyombo vya Moto vinavyotumia Petrol hii ni hatari mno.

Hili ni Jambo la ajabu na kushangaza sana kwa Viongozi wa Manispaa, LATRA NA TANROAD wanashindwa vipi kusimamia au kuwaondoa kabisa wale wafanyabiashara kule ndani ya stand, au wapangwe vizuri watengewe maeneo maalum kule stand lakini sio kule katikati Ile ni hatari sana.

Wale wafanyabiashara hawafanyi usafi ukipita asubuhi kule stand ni kuchafu, vyakula vimemwagwa, uchafu wa matunda na wale wamama wenye watoto wanajisaidia kule kule ndani lakini hakuna kiongozi anayejali.

Hii ni kero Kubwa kwetu wakazi wa Mbezi Luis tunaiomba Serikali ifanye jambo kuinusuru stand ya mbezi luis ambayo kwa sasa imegeuzwa kuwa soko.
 
Wabongo ni wabishi sana inabidi mjerumani arudi kutu tawala kwa Viboko.

Nadhani mjerumani ange tutawala walau mpaka 1980 hivi, Akili zetu zingekuwa zime staarabika.

Waafrika tulipewa uhuru mapema mno bila ya sisi wenyewe kujitambua na kujielewa.
 
Nilishangaa sana last Week nilipoona Dereva wa DalaDala anamuomba Mfanyabiashara apaki Gari lake ili ajaze Wateja baada ya Kumkuta ametandika Bidhaa zake Njegere, Mchicha, Maembe na Maparachichi barabarani kabisa pasipotakiwa.
 
Wabongo ni wabishi sana inabidi mjerumani arudi kutu tawala kwa Viboko.

Nadhani mjerumani ange tutawala walau mpaka 1980 hivi, Akili zetu zingekuwa zime staarabika.

Waafrika tulipewa uhuru mapema mno bila ya sisi wenyewe kujitambua na kujielewa.
hahah kwa hiyo tutawaliwe tena kwanza ili akili zitukae sawa?
 
Back
Top Bottom