Starehe za jiji la Dar es salaam linavyoshusha viwango vya wachezaji wa Simba na Yanga

Starehe za jiji la Dar es salaam linavyoshusha viwango vya wachezaji wa Simba na Yanga

Aliulizwa Chirwa tofauti ya Azam na Yanga ni nini?

Alijibu "Yanga ukiwa pale hutumii hela yako ya mshahara kwenye mavazi, chakula na mahitaji mengine.... kwasababu siku ukifunga goli, ukipita kkoo au sehemu yenye maduka unaweza kurudi na begi la nguo na viatu, zawadi za mashabiki au ukapewa hela nyingi tu bila kutarajia,au anaweza kuja boss anayekukubali(mwenye hela) akakupa laki 2 au 5.....ila hapa Azam fc mshahara wako tu na ukipita mtaani hakuna mwenye muda nawewe "
Pia bia unanunuliwa na demu mkali unatafutiwa😀😀
 
Hii Bongo tuendelee kuwaheshimu kina Sammata maana mimi mtu wa kawaida tu pale DSM nimekula maisha pata picha hao wenye majina [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mie nadhan bongo wachezaji wetu hawajitambui kwa njia moja au nyingine

Sisi bado tupo amachure wao wapo professional
 
Hii inaitwa Cheap Popularity ukiiendekeza lazima uharibu career yako

Do it at your own risk
 
Huo mji siutaki ku usikia niliunguza mil 6 kwa sababu ya starehe kuja kustuka Sina kitu .
Kurudi mkoani ilibid nipande Fuso nilikaa kwa nyuma napigwa upepo huku nikiwapungia watu mkono kuiaga Dar .
Ahaaaa dah
 
Hii Bongo tuendelee kuwaheshimu kina Sammata maana mimi mtu wa kawaida tu pale DSM nimekula maisha pata picha hao wenye majina [emoji23][emoji23][emoji23]
Bata hazizoeleki ni vile tu hatuna hela
 
Mie nadhan bongo wachezaji wetu hawajitambui kwa njia moja au nyingine

Sisi bado tupo amachure wao wapo professional
Usiwalaumu,wengi ni wadogo kiumri na hawana management ya kuwaongoza,ulaya kuna wazazi waliamua kuwa ndio mameneja wa watoto wao.mbape ,neyma,ronaldinho ets
 
Mbona wakina Mbappe na Neymar wako Paris (The City Of Love) lakini hawashuki viwango?
😂😂😂😂sijui kafanya utafiti wake wapi Aisee,Mueleze atembee aache ushamba. Watu wako paris, pesa wanazo, umaarufu wanao na viwango havishuki
 
Hili jiji lisikie tu kwenye radio,ila Dar kuna starehe jamani,nimetembelea mikoa mingi nchini na nchi nyingi kidogo si haba,nyingine kwa kwenda phyisically nyingine kwa kusoma,kusikia,movies na mitandao .ila Dar bado ni kinara wa starehe,Jonas Mkude huwa anakula starehe mpaka anazima kesho yake anafungiwa,Chama kuna muda kiwango kilishuka kuja kufuatilia ni starehe za Tabata,
Obrey Chirwa,Amis Tambwe,Chama na wengine ukiwaambia warudi kwao watalia,Kapombe,Ngasa,Ajibu wanajua starehe zilizopo mjini hawawezi kuzipata hata Ibiza.n dio maana waligoma kucheza nje ya nchi
Ukiona mchezaji yupo Simba au Yanga na kiwango hakishuki mpe heshima yake,ujue ameamua kuzipa kisogo starehe za mjini,big up Shabalala na Aishi Manula.
Hawa wachezaji wanalipwa hela nyingi sana kuliko hata maafisa wa TRA stil wananunuliwa pombe na chawa wao na mademu wanaletewa.Mungu akupe nini tena .
Ukija kwenye Derby ya Simba na Yanga ndio usiseme wale first eleven hujiona kama wako mbinguni,nchi nzima inasimama kukuangalia,ikitokea ukafunga goli kwenye derby inabidi uzime simu maana utaishiwa chaji sms za mihamala ya M pesa,pongezi na mademu kujitongozesha...
Inataka moyo
Na wakiendekeza huo ujinga watabaki Tz hapahapa hutawasikia kwenye ligi za maana duniani.
 
Washamba wa Paris viwango vinashuka,Neyma alitakiwa kuwa zaidi ya Messi ila ushamba wa starehe ndio huyo anakufa bila balondor,pia kule wana njia nyingi za kuwadhibiti wachezaji wao kuhusu nidhamu
Ingawa hata bata la kwao Brazil hasa mji wao mkuu Brazilia huaga sio la kitoto mkuu, labda Neyma wakati akiwa kwao hakua na HELA ndio maana hakuwahi ku enjoy.
Mleta UZi kanifungua macho, kumbe wachezaji kung'ang'ani kucheza Tanzania hasa Yanga na Simba hua sio mpira tu, kuna na starehe and this is why Chama karudi? Aiseee. Kumbe ni kweli kwamba Tanzania sio nchi masikini aise
 
Back
Top Bottom