Mkuu upangaji wa bei huwa unazingatia mambo kibao ikiwemo gharama za biashara husika.. Mtu anayeuza pop corn mliman city anakua na gharama kubwa sana za kiuendeshaji kuliko wale wa vitoroli vya barabarani. Mfano mtu aliepanga kijisehemu pale mliman analipa kodi lets say 500,000, analipa umeme 50,000, analipa mfanyakazi 200,000, analipa kodi ya serekali analipa ushuru analipa fire n.k ukijumlisha hapo hizo gharama na sustainability ya bisahara haiwezekani bei ikawa sawa na ya waendesha vitorori barabarani. So kuwa muelewa mkuu azawaizi unataka watu wafunge biashara zao.