Stars iliyolipwa posho zote na Rais Samia imefungwa, Tujipange zaidi

Stars iliyolipwa posho zote na Rais Samia imefungwa, Tujipange zaidi

Jamani nauliza tu , Je walipewe booster? Walipata Jani?
Kama hawakupata tusilaumu
Maandalizi ya muda mrefu na yenye umakini wa hali ya juu, bora tukajifunze wenzetu wamewezaje yale mataifa ambayo yapo mbele kimpira
 
Bocco
Manura
Shomari wote
MHuseni
Samata
Msuva

Hawa wote hawatakiwi kwenye timu yetu ya Taifa
 
Tanzania ni sawa na likulima limoja livivu vivu haswa, wakati wenzake wanadamka alfajiri lenyewe saa nne ndo linaingia shambani, halitunzi shamba Wala kupanda mbegu Bora.

Subiri Sasa wakati wa mavuno, linaandaa ghala kubwa kuliko wote wakati mazao yenyewe hata bajaji hayajai, na kwa vile Lina mdomo litaishia kulalama majirani wanalifanyia ndumba kwenye mazao[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Yaani ligi imeahirishwa muda mrefu afu ujinga unafanyika
 
CCM wana nuksi, walivyoweka mkono wao tu sisi tukajua kipigo na mbwa mwizi kinafuata.

Mambo ya michezo hayataki siasa, CCM wana usafi gani kuipa baraka Taifa stars kama si kuipaka nuksi.
Ni kweli kabisa hata simba waliopochukua tu slogan yao ya mama ya "kazi iendelee" tayari wakaweka unajisi au unuksi juu yake, simba ikafungwa.

Nazani ni wakati wa ccm na serikali yake wakaaa pembeni na mpira maana wanahamishia nuksi au unajisi wao kwenye mpira na kitu chochote watakachogusa, tutawalaumu wachezaji wetu bure tu wakati chanzo ni nuksi au unajisi wa ccm na serikali yake maana pale wanaposhiriki tu katika mpira au kitu chochote kile Ile nuksi au unajisi wao unahamia huko.
 
Wale wazee wote kwenye ile timu wastaafishwe kwa manufaa ya umma, nasisitiza wazee wote, hata hayo majina yanayotokea ulaya yote hayana maana, watafutwe vijana wapya toka timu za ndani.
Bado hiyo sio dawa kwa soka letu jama! Vijana tu baasi, kweli?
 
Cousin wako ametuchomesha we demu..mwambie watanganyika wanapasuka huku mtaani wakifikiria zile bilioni walizochangiwa ni bora tugawane hata jero jero nchi nzima kuliko kuwapa vichwa vya wendawazimu.
 
Hela ya Rais ama hela yako kupitia kodi.
mkuu hiyo ni ya rais kwakuwa ipo kwake
Pic%20Layer_20211111131418277.jpg
 
Cousin yangu anayechezea timu ya Taifa, alinieleza kwamba juzi baada ya kutembelewa na Waziri Mkuu, walilipwa posho zao zote ikiwemo malimbikizo ya nyuma.

Posho ambazo walikuwa hawajalipwa zilikuwa zinashusha Morali kwenye kambi, lakini Waziri Mkuu aliyeagizwa na Rais Samia Suluhu kuitembelea timu hiyo, alifahamu jambo hilo akalitatua.

Stars imetendewa haki na Serikali ya Rais Samia, ikiwa ni moja kati ya mipango yake ya kuzisaidia timu zote za Taifa (Rejea hatua alizochukua tangu aingie madarakani katika kuendeleza michezo ikiwemo Kuhuisha Mfuko wa Taifa wa michezo, kuanza ujenzi wa viwanja, kuondoa kodi kwenye nyasi bandia na hatua nyingine njema)

Matokeo ya leo yanahusu mpira wenyewe, Tumezidiwa wa DRC.

HATA HIVYO : Tuna safari ndefu bado. Tujenge timu zetu za Taifa.

View attachment 2007208
CCM na Serikali yake walivyotia mkono tu kwenye Taifa Stars ndiyo nuksi ilipoingia. Mnambenepesha ng'ombe siku ya mnada.
 
Hiv unafikir kila kitu kinaletwa na hela unafikir hao Benin wamepewa hela ndo wafanye vizur wew unasubir mtoto aingie form four amekaribia Siku ya mtihan wa mwisho unaanza kuleta presha lazima atafeli mpira n uwekezaji wajenge viwanja vya michezo na wajenge academy za watoto wadogo
 
Kwa hiyo walilewa na posho pamoja na malimbikizo,, Jamani walikuwa wanawaza pesa zao walizopewa
 
Cousin yangu anayechezea timu ya Taifa, alinieleza kwamba juzi baada ya kutembelewa na Waziri Mkuu, walilipwa posho zao zote ikiwemo malimbikizo ya nyuma.

Posho ambazo walikuwa hawajalipwa zilikuwa zinashusha Morali kwenye kambi, lakini Waziri Mkuu aliyeagizwa na Rais Samia Suluhu kuitembelea timu hiyo, alifahamu jambo hilo akalitatua.

Stars imetendewa haki na Serikali ya Rais Samia, ikiwa ni moja kati ya mipango yake ya kuzisaidia timu zote za Taifa (Rejea hatua alizochukua tangu aingie madarakani katika kuendeleza michezo ikiwemo Kuhuisha Mfuko wa Taifa wa michezo, kuanza ujenzi wa viwanja, kuondoa kodi kwenye nyasi bandia na hatua nyingine njema)

Matokeo ya leo yanahusu mpira wenyewe, Tumezidiwa wa DRC.

HATA HIVYO : Tuna safari ndefu bado. Tujenge timu zetu za Taifa.

View attachment 2007208
Chawa kazini

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom