Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Kiongozi, kuna mambo huwa tunawalaumu hawa service providers kwa 'ignorance' yetu. Baada ya wewe kuunga kifurushi then kikaisha baada ya nusu mwezi uslichukua hatua gani?

Sasa fanya hivi, Inawezekana kabisa hata hujui upo kifurushi gani, Inawezekana unaweka bundle la 'nyota' kumbe umejiunga bundle la 'mambo'. Dial *150*63# ili ujuwe upo kifurushi gani, then baada ya hapo unaweza kuhama kifurushi kimoja kwenda kingine bila tatizo na ukatumia pesa yako hadi mwisho wa mwezi.

Unaweza; Kuangalia salio na aina ya kifurushi, Kubadilisha kifurushi hnachohitaji etc.

Tusiwaite wezi kwa kuwa tu tupo ignorant na hatutaki kujifunza. Dial 0764 700 800 wakusaidie.

CC StarTimes Tanzania.
 
Nimewasiliana noa wameniambia eti niko kwenye kifurushi cha mambo na sibuka ambacho ni 15,000. Na mimi sijawahi kujiunga na hicho kifurushi cha sibuka na mambo, niko mambo tu after all kuna kipindi walikuwa wanatangaza kifurushi cha mambo 12,000.

Hiyo na mambo na sibuka wala sijui ni nini? Inamaana waliniunga wenyewe. Maana mimi niko mambo toka 2012. Huu ndiyo ninasema wizi
 
Uliungwa by default, hilo sio tatizo. Kila kitu kipo wazi sana, dial *150*60# utajua kila kitu. Hakuna sababu ya kuogopa kuwa unaibiwa.

Mfano, mimi mwezi huu nimejiunga "mambo", mwezi ujao mambo yakiwa vizuri najiunga "uhuru" kwa kutumia hiyo USSD hapo.
 
Wizi mwingine bhana ivi hiyo SIBUKA ina nini cha maana mpaka ikifanye kifurushi kiwe 15,000?. Ni moja kati ya channel mbovu hapa bongo. Meneja masoko wa Sibuka ni kipofu....
 
Hivi remote za king'amuzi chenu mnauzaje?

Jamii Forums mobile app
 
Yan najuta kuingia mkenge nikanunua ichi kishumbusi tangu jana nimelipia lakini bado akioneshi television yoyote ata zile radio zao za wapi uko aziongei yani ni msalaba mtupu kila mda ni kuscrach tuu yani ni matatizo matupu

Mwenye namba zao za huduma kwa wateja naomba anisaidie tafadhali ili niwapigie wakinizingua narudi dukani kuchukua azam

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina ushauri kuna SMS nililetewa kutoka startimes ilikuwa inasema unaweza klipia king,amuzi kwa siku 1000 shilling au kwa mwezi elfu kumi na mbili vipi kuhusu kile kifurushi cha wiki mbili ambacho kilikuwa ndo at least
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…