Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Nimependa sana .mulichofanya startimes, kitendo cha kuja humu haraka na kujibu malalamiko ya mteja.

Jitahidini kufanya hivyo kwa kila mteja.
Mulifanya kosa kubwa kutokutoa majibu/taarifa ya haraka kipindi cha tatizo la itv na eatv...

Tafakari...
 


habari yako tunaomba ututajie unaishi maeneo gani! tutamtuma fundi wetu aje aku saidie upate huduma zetu vizuri!
 
habari yako

tafadhari tujulishe uko Arusha sehemu gani, huduma yetu arusha inapatikana vizuri wala haina matatizo. kuscratch kwa decoder kunasababishwa na upokeaji hafifu wa mawimbi ambao unaatokana na matatizo katika antena yako

Natumia antenna ya nje. Mwanzo ilikuwa poa lakini sasa ni shida. Naishi along old Moshi road karibu na chuo cha Nelson Mandela
View attachment 226589
 
habri yako

kwa maeneo ya Tukuyu mbeya tunakushauri utumie huduma yetu ya SATELITE DISH, ambayo inaonekana vizuri huko, hii huduma ni ving'amuzi vya startimes vinavyotumia DISH

Ahsante, je ntakipata king'amzi kwa bei gani ? Napenda startimes
 
habari...mimi niko kibaha mwendapole, namba ya akaunti ya king'amuzi changu cha startimes ni 02035111864 nina malalamiko yafuatayo🙁1) hii ni wiki ya 3 sasa steshen za tv zifuatazo hazipo kabisa kwenye menu list.....itv,eatv,mlimani tv,star tv,e star tv,nimekuwa nikikosa mambo mengi ya kielimu,kiuchumi,kijamii,burudani na kiutamaduni kwa muda mrefu sasa.(2)sielewi hiki kifurushi kipya nakipataje? karibu wiki 3 sasa tangu nimelipa tshs 4000/ sikukipata na hela yangu haukurudishwa,sasa mbona hatuwaelewi startimes?(3)tafadhalini naomba utatuzi wa masuala hayo yanayonitatiza ili niendelee kufurahia king'amuzi chetu cha startimez.asanteni kazi njema.
 
Habari,kwa singida ile ofa yenu ya king"amuzi vyemu vya ofa,yaani tsh 34,000,kifurushi cha nyota na king"amuzi kwa miezi saba na nusu inapatikana wapi?
 
Big up star times kwa kunijibu kwa haraka. Leo nitabadilisha na kuweka kifushi cha nyota then nitalipia tena 4000 ili nione.
Asante sana kwa majibu
 
kwanini usifunge free TV channel zilizopo Amos5@17e mbona kuna channel kibao za Bure bila malipo za ndani na nnje ya nchi.

Hii makitu inapatikana wapi aiseee niiwahi fasta nishaibiwa sana na hivi vishumbushi mtu chanel za bure tunalipishwa yaani wanatuibia mchana kweupee.
 

Si kweli mimi nina ving`amuzi viwili baada ya hili tangazo la Nyota kimoja nimekilipia shs 4000 hakuna channel yoyote ya mambo iliyofunguliwa acheni wizi au ndio mnataka kuwaiga Voda?
 

umeengia choo cha wanawake
 
Nahitaji kununua Startimes ni sh: ngapi decoder pamoja na dish 2 je kuna free chanel ngapi na nizipi na zipi? 3 malipo kwa chanel zingine ni Tsh:ngapi kwa mwezi? ni hayo tu. Chacha wa marwa niko Tarime Mara.
 
Week ya 2 sasa.. li ng'amuz lenu halionyeshi star tv. Ndo nn sasa??
 
Mimi nimenunua king'amuzi cha tshs 59000 kama siku sita zilizopita. nimeunganisha kila kitu sawa na maelezo yaliyopo katika "user's guide" lakini hakuna kinachoonekana. Nikienda ktk signal status inasoma zero. Nifanyeje au tatizo ni nini? Naishi Tandika.
 
kuna watu wana moyo wa chuma,yaani hawa startimes ni bure,yan nna miezi 6 ckitumii,yan nmeachana nacho.yan za bure pia nlipie tena za bongo,km kuna mtu anataka ata bure ntampa,uchafu tuh.bora nlipie dstv.nienjoy movies.
 
mbona sijibiwi?
Kama sistahili kujibiwa mniambie nikadai pesa yangu ninunue king'amuzi kingine.
 
Huduma zenu bado zinahitaji kuboreshwa huwez ukalinganisha na huduma za vingamuz vingine kama azam nk.
 
Napenda kujua vifurushi mbali mbali na gharama zake na jinsi ya kuvipata vifurushi hivyo Bila kuja ofisini kwenu
 
nimekuwa nikinunua kifurushi cha nyota bila mafanikio. ujumbe naoupata ni huu "smart kadi hiyo 02035..... imefanikiwa kupata4. subiri kwa dakika15 kisha kuhakikisha chaneli zako". lakini baada ya muda huo kupita hakuna mabadiliko yoyote. baada ya shida hiyo ndani ya siku tatu nikajaribu kulipia kupia menu ya m-pesa, napo hadi leo ni siku ya pili hakuna chochote! ujumbe wa kuthibitisha malipo nimeupata toka selcom. nipo dom
 

nimekuwa nikinunua kifurushi cha nyota bila mafanikio. ujumbe naoupata ni huu "smart kadi hiyo 02035..... imefanikiwa kupata4. subiri kwa dakika15 kisha kuhakikisha chaneli zako". lakini baada ya muda huo kupita hakuna mabadiliko yoyote. baada ya shida hiyo ndani ya siku tatu nikajaribu kulipia kupia menu ya m-pesa, napo hadi leo ni siku ya pili hakuna chochote! ujumbe wa kuthibitisha malipo nimeupata toka selcom. nipo dom
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…