Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimelipia kifurushi cha mambo yapata week sasa lakini channel zinazo onyesha vizuri ni tatu tu nyingine zina katakata sana na zingine hazionyeshi kabisaa yani pesa yangu imekwenda bure najuta hata kwanini nimekilipia bora ningebaki naangalia free channel hizo mlizo tuachia kama nibomba nimeshazungusha sana nimelipandisha na kulishusha lakini hakuna mabadiliko
habari yako
tafadhari tujulishe uko Arusha sehemu gani, huduma yetu arusha inapatikana vizuri wala haina matatizo. kuscratch kwa decoder kunasababishwa na upokeaji hafifu wa mawimbi ambao unaatokana na matatizo katika antena yako
habri yako
kwa maeneo ya Tukuyu mbeya tunakushauri utumie huduma yetu ya SATELITE DISH, ambayo inaonekana vizuri huko, hii huduma ni ving'amuzi vya startimes vinavyotumia DISH
Ahsante, je ntakipata king'amzi kwa bei gani ? Napenda startimes
kwanini usifunge free TV channel zilizopo Amos5@17e mbona kuna channel kibao za Bure bila malipo za ndani na nnje ya nchi.
Habari yako
ndugu mteja, sio kweli kuwa kifurushi cha NYOTA kina matatizo kama unavyofikiri, kama unataka kuhama kifurushi kutoka kifurushi ulichokuwa unalipia awali, ni lazima ubadilishe kifurushi chako, kama awali ulikuwa unatumia kifurushi cha mambo 10000@mwezi alafu ukalipia 4000 bila kubadilisha kufurushi basi fedha yako 4000 itatumika katika kifurushi cha mambo, yaani utaangalia kwa muda wasiku 12 chanel za mambo.
hivyo basi kama awali ulikuwa unatumia kifurushi cha mambo, utakapolipia kifurushi cha NYOTA 4000 ni lazima ubadilishe kifurushi. unaweza kubadilisha kifurushi kwa kupiga namba yetu ya huduma kwa wateja, au kwa kutembelea ofisi zetu au kwa kutumia simu yako ya mkononi kwa kupiga *150*63# kisha ufuate maelekezo utayopewa
ahsante
mimi naitwa lupakisyo mwaisumo, nimefanya miamala mitatu, kulipia kifurushi cha dstv lakini kwa bahati mbaya namba niliyokuwa nalipia ilikosewa, badala ya 42793676695, nilikuwa naweka 4279367669 , yaani namba 5 ya mwiso sikuiweka, hivyo tarehe 1/1/2015 mnamo saa 1:07 nilipoteza sh. 7,000/=, tarehe 2/1/2015 saa 11:55 asubuhi nikaipoteza tena sh 10,000/=. Nimekuja kugundua tena nilipofanya muamala tarehe 2/2/2015 wa sh. 17,500/= saa 2:09 usiku. Nimewapigia watu wa tigo pesa kunirudishia hizo fedha zangu, wakanielekeza kuwanapaswa kuongea na nyie watu wa startimes. Hivyo naomba kusaidiwa katika tatizo hili. Namba niliyoitumia kulipia king'amuzi hiki ni 0713874005, na smartcard inamilikiwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya kilolo, mkoani iringa.
Habari zenu wanaJamiiForums
Je una tatizo lolote unapotumia huduma zetu? Unaushauri wowote ili kuboresha huduma zetu?
Tafadhali tunaomba utumie thread hii, ili tukusaidie? Tafadhali tunaomba unapokuwa na tatizo ili tukusaidie kirahisi
1. Utaje tatizo lako
2. Taja sehemu unayoishi?
3. Pia kama unaweza tunaomba ututumie na namba yako ya smartcard!
STARTIMES tutajibu maoni, malalamiko na ushauri ule tu ambao utakuwa umejitosheleza na wenye nia ya kutusaidia kuboresha huduma zetu.
Ahsanteni sana na karibuni nyote