Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Aiseeee !!
 
Hivi samahani huwa mnafunga kama waislamu mchana kutwa hamli na kunywa au nyinyi mpoje?

Sent using Jamii Forums mobile app

BRO sijawahi kuona mkristo hata mmoja amefunga Toka nizaliwe, nimecheza nao utotoni, nimesoma nao, majirani zangu, nafanya nao kazi, nakula nao Bata...... Narudia Toka nizaliwe sijawahi kuona mkristo amefunga ...iwe pombe, papuchi, mdudu, wali,ugali,nyama,maharage etc. Mwaka Jana niliweka dau ofisini na mtaani kwa kuwaambia hawatafunga na hakuna alofunga lakini jumatano ya majivu kwa mbwembwe zote walijipaka jivu Kama vinyago.DINI SIO MBWEMBWE.
 
Neno kwaresma ni neno la kilatini liitwalo Quadragesima maana yake ni arobaini(40)

mpenzi msomaji, katika maisha ya kikristo kuna kipindi cha siku 40.majira haya ya kwaresma huanza siku ya jumatano ya majivu na kuishia jumapili ya pasaka siku ambayo wakristo wanakumbuka kufufuka kwa yesu kristo kutoka katika wafu.

Kwaresma ni kipindi maalum ambacho wakristo wanakumbuka maisha ya Yesu kristo hapa duniani hususan mateso, kufa na kufufuka kwake.






Ni kipindi cha kutafakari maana na umuhimu wa dhabihu ya YESU kristo katika ukombozi wa dunia na kumrudia Mungu. Aidha ni kipindi ambacho wakristo wanakumbushwa kufanya toba na kumrudia Mungu kwa mujibu wa maandiko matakatifu.

Ingawa kipindi cha kwaresma ni kipindi cha mafungo kwa wakristo, watu wengi na hasa wa dini nyingine hushindwa kutambua funga inayofanywa na wakristo katika kipindi hiki na hasa kwa sababu wakristo wengi huonekana wakiendelea kula na kunywa wakati wa kwaresma. Wakristo walio wengi pamoja na kufuata kielelezo cha Yesu kristo ambae alifunga siku arobaini (usiku na mchana) huzingatia maagizo ya YESU mwenyewe na nabii Isaya ambao kwa kiasi kikubwa hufafanua aina ya funga ambayo wakristo wanapaswa kuizingatia.


Mwenyezi Mungu alitoa maagizo ya namna ya kufunga kupitia kwa nabii isaya akisema hivi
"Walakini wanitafuta kila siku, hupenda kujua njia zangu ; kama vile taifa waliotenda haki, wasioacha sheria ya Mungu wao. Hutaka kwangu sheria za haki, humkaribia Mungu. Husema, mbona tumefunga lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu lakini huangalii? Fahamuni siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu. Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu. Je, kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je, ni siku ya mtu kujitabisha nafsi yake? je ni kuinamisha kichwa kama unyasi na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? je utasema ni siku ya kufunga na ya kukubaliwa na BWANA? Je, saumu niliyoichagua sio ya namna hii? Kufunguo vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaachia huru walio onewa, na kwamba mvunje kila nira? Je, sio kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? umwonapo mtu aliye uchi umvike nguo, wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe? Ndipo nuru yako itakapo pambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia, utukufu wa BWANA (Mungu) utakufuata nyuma ukulinde. Ndipo utaita na BWANA ataitika, utalia nae atasema mimi hapa..." (Isaya 58: 2-9).


Mwenyezi Mungu alitoa maagizo haya baada ya kuona watu wengi wakipoteza muda mwingi na kujitabisha kuacha kula na kujitesa miili yao ili kumpendeza Mungu, huku wakisahau mambo muhimu zaidi ambayo Mungu anawataka wafanye ili kumpendeza. (Katika kipindi hicho wayahudi walikuwa wakifunga kwa kujitesa sana ikiwa ni pamoja na kuacha kula, kuvua nguo zao za thamani na kuvaa magunia, kujipaka majivu na wengine kujipiga na kujikata miili yao ili waone maumivu zaidi.

Aidha, watu walikuwa wakitumia kipindi cha kufunga kuuonesha umma jinsi walivyo wacha Mungu na hivyo kupewa heshima mtaani. Mtu asiyefunga alionekana mjinga, mtenda dhambi na asiyefaa katika jamii. Kufunga ilikuwa sehemu ya maisha na si suala la uhusiano binafsi kati ya mtu na Mungu).

Kwa vile Mwenyezi Mungu wetu ni wa upendo na huruma, alimtuma nabii isaya kuwaambia watu hao kuachana na funga hiyo isiyo na maana na badala yake kuelekeza nguvu zao katika mambo muhimu ambayo Mungu anaangalia katika kutathimini utu wa mtu. Mambo hayo ni upendo, huruma na kujitoa kama ilivyoelezwa hapo juu na kuachana uovu wa aina zote.. Kwa msingi huo, mtu mwenye upendo na anaejitoa kusaidia wengine ana thamani kubwa mbele za Mungu kuliko mtu anaeshinda njaa siku 300 za mwaka pasipo kuonesha upendo wa kweli kwa wengine.


Yesu kristo alipokuja ulimwenguni, alisisitiza maneno ya nabii Isaya kwa kutaka watu waache tabia ya funga za kujionesha kwa watu, na badala yake wajitahidi kumpendeza Mugu. Yesu alisema"Tena mfungapo msiwe kama wanafiki wenye nyuso za kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amini nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na baba yako (Mungu) aliye sirini; na baba yako aonae sirini atakujazi" (Mathayo 6:16)

Kumbe tabia ya kujionesha mbele za watu kwamba tumefunga inamuudhi Mungu na kutufanya tukose thawabu. Mtu anaejionesha au kujisifu kwamba anafunga huambulia kusifiwa na watu wa kidunia ambao wanadhani mtu huyo ni mtakatifu sana, lakini kwa mujibu wa maandiko matakatifu mtu huyo anajisumbua na kupoteza muda wake bure kwani hakuna thawabu anayo pata kwa Mwenyezi Mungu.


Tumuombe Mungu sana atuongoze na kutusaidia katika kipindi hiki cha Kwaresma na baada ya hapo.Ni wajibu wetu kujitahidi kuachana na maovu yote, kufanya toba ya kweli na kumpokea Yesu katika mioyo yetu badala ya kumuabudu kwa midomo tu. Tunapaswa kukumbuka kuwa Mungu wetu ni yule yule kabla, wakati na baada ya kipindi cha Kwaresma na hivyo kipindi hiki kiwe kipindi cha kutukumbusha na kutuandaa kwa ajili ya wakati mrefu ujao baada ya Kwaresma.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eeee bhana eeee !!
 
nitarudi kusoma comment ili nipate pa kubishia



Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
kweli dini ni ngumu kama ukisoma kitabu kimoja,utabaki kusikiliza maneno ya watu,lakini dini nyepesi kama utasoma vitabu vyote vya Mwenyezi mungu pasipo kuchagua,ndio maana Leo watu wanafwata yaliyoanzishwa na mwanadamu yasiyokuwa na historian yoyote ile pole sana ndugu yangu.

Unaijua miezi mitakatifu ya mwenyezi mungu aliyowaamulu mitume wake na manabii wafunge?
 
mfungo unaotambulika na Mungu ni ramadhani tu . kwaresma mpaka wakristo wenyewe hawaitambui ndio maana hawafungi
 
Ukristo ufutwe.Tubaki waislamu tu
 
Mumuma tusaidie kuijua miezi hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi zote ni drama za kipumbavu!

Kitendo cha Mungu kukosa options zingine hadi mwanae wa pekee ateseke kiasi kile huku bado wanadamu wengine wakiwa wangali katika Lindi la mateso hakipatani na akili za mtu mwenye akili timamu.

Chukulia wewe ndio Mungu mwenye uwezo wote, upendo na mjuzi wa yote, je? Ungefanya mauzauza kama hayo?

Au ungeweza kuendelea kujikalia tu ilihali mambo yamezidi kuwa mabaya humu duniani?

Wewe waweza kumwacha mwanao ateseke muda mrefu mpaka afe kwa visingizio vya kipumbavu namna hii?

Kama ndio hivi, kwanini basi mwanadamu aliyeumbwa na huyo Mungu aweze kuwaza vyema kuliko huyo Mungu?

Acheni kuendeshwa na upepo enyi wanadamu mliokosa akili.
 
mfungo unaotambulika na Mungu ni ramadhani tu . kwaresma mpaka wakristo wenyewe hawaitambui ndio maana hawafungi
Hakuna cha Ramadhani, Kwaresima wala Juma hapa! Nyinyi wote mmepotosha akili zenu makusudi.

Hebu eleza mambo hayo yana faida gani katika jamii ya mwanadamu?
 
Fact kabisaa yani..
 
Ndugu yangu mungu yupo,na wapo watu waliyokuwepo wabishi kabla yako,na historia zao zipo
 
Katika eneo ambalo wazungu walitukamata ni hapo kwenye dini. Yaani kila nikisoma mijadala ya aina hii hua nahuzunika sana. Waafrika itatuchukua miaka mingi sana kutoka katika vifungo vya ukoloni na kujitambua!

Wakati sisi tunabishana na kutiana vidole vya macho huku kuhusu kupakana majivu kama vichaa, mara kuvaa magunia, sijui amri zipi ni bora kati ya Roma na Uyahudi, wao wanapeleka vyombo sayari ya Mars.. wakati mwingine hua nawaza hivi sisi ni binadamu kweli..??🤔
 
Aiseee !!!
 
Maelezo na mafundisho kuhusu Jumatano ya Majivu ni mengi, marefu ma ya kina. Nayafupisha kama ifiatavyo:-

Jumatano ya Majivu ni Mwanzo wa kipindi cha dini cha Kwaresima (siku 40) ambapo mambo matatu makuu matatu huzingatiwa katika maisha ya waumini wa dini Katoliki ya Mitume, Nayo ni Upendo, Huruma, Kusamehe.

Inaitwa Jumatano ya majivu kama ishara ya toba ikizingatiwa kuwa binadamu ni mavumbi na mavumbini atarudi. Ukumbusho wa maisha baada ya kifo binadamu akiwa msafi kimwili na kiroho. Majivu hayo yanatokana na kuchomwa kwa matawi ya mchikichi ya mwaka uliopita yaliyobarikiwa.

Misingi ya Siku 40 za mfungo ni Kusali, Kufunga, na Kutoa Msaada kwa wenye mahitaji.
 
Kwani unatumia Biblia gani isiyo na Kitabu cha Yeremia 6:26, Acha kumeza mafunzo ya Lesson tumia Biblia mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…