Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Nyinyi tangu mlipoondoa Seria A tu nikawahama,sasa je nilete kisimbusi mnipe hela yangu japo nusu?
 
Hili ndiyo anguko la Startimes? Chanel za fox,tv1,cloudtv,national geographic wild,n.k zote mmefuta. Maana ya nini? Kama si ndiyo hatima yenu?
Mimi nashàuri wote tunaotumia ving'amuzi vya hawa wapumbavu startimes tuvitumie kwa local channel tu, lakini ni bora kujibana kununuwa dstv tu. Kwa sasa kulipia king'amuzi cha stattimes ni sawa na uwendawazimu.

Watanzania ifike wakati tuamke na tusikubali kudharauliwa.

Boycott Startimes now.
 
Wengi Sana Wanatumia Local Channels
Kwasasa Mapato Yao Yanasua Nadhani Wataanza Kupunguza Bei
Hawana Mvuto Hawa
 
Hivi startimes kwanini mmekuwa mnaondoa baadhi ya chanels bila hata kuwataarifu wateja wenu? Kwakweli mnaharibu soko lenu sana. Net Geo wild, mmeondoa Emanuel tv hakuna sauti nk. Hivi mnajua kuna watu tunalipia king'amuzi ili kuona hizo chanel tu ? halafu analipa anangalia leo kesho mmeshaondoa!! kwakweli hili linaboa sana.
Binafsi mimi nimeamua kubaki na local chanels tu nimehamia Dstv kabisa. Huu uzalendo umenishinda. madakimasanja@yahoo.com
 
Umefanya uamuzi wa busara sana, hata Mimi Niko mbioni kununuwa dstv, hawa startimes kitabaki kuwa king'amuzi kwa ajili ya free local channel tu, siwezi kurecharge tena airtime over my dead body.
 
Hivi kwa nini mvua ikinyesha kwa wingi Sisi wenye decorder za dishi ghafra matangazo ukatika nini ttzo au dish alipo Sawa?
 
Asee startimes mnazingua sana sana , ukizima decoda mara channel zibadilike, halafu kuna siku nililipa 12k channel mlizoweka asee poa tuu
 
Mie cha kwangu hata Local channels hakisomi soon pesa ikikata!

Nishatupaga ving'amuzi viwili Kwa upuuzi wa namna hii

Guess what is next!!!!
 
Hiki kisimbuzi cha Startimes nauza 40,000 bila dishi, anayekitaka anicheck PM. Nimekitumia 3 months only.

Hapa nahamia 1. Azam au 2. DSTV
 
Mnanichanganya sana. Nimeweka kifurushi hata mwezi haujaisha mnaondoka hewani. Rudisheni pesa zangu fasta!
 
Mna mambo ya kitapeli tapeli sana.Kesho nauza hili dishi na kin'gamuzi then nafungua kesi mahakamani ya wizi wa uaminifu
 
Sijawahi ona usanii kama wa Startimes.

Channel kifurushi cha uhuru Tshs 18,000 World Football na Sports nyingine kwangu siku hizi hazionyeshi na nimelipia.

Na matangazo yenu mnajigamba kuwa zinaonekana kwa bei hiyo. Sasa nina kama mwezi na zaidi nilkuwa naangalia mmetoa.

Wametoa channels kama:
1. Nat Geo Wild
2. Clouds Tv
3. Fox Sports na nyinginezo kama 4 sizioni.

Sasa mateso ya nini? Mwezi huu nahamia Multichoice (DStv) au Azam Tv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…