Mimi channels kama Aljazeera, Ze Cinema, TVC news, Star Rise, ST baby ,hazitoi sauti. Nilitembelea ofisi zao kuuliza hawakuwa na majibu ila wakawasiliana na makao makuu wakadai eti wameboresha tech ya urushaji wa matangazo kwa hiyo ving'amuzi vya zamani ndio maana baadhi ya channel zinasumbua kutoa sauti.
Suluhisho; Eti ninunue kinga'amuzi cha kisasa zaidi ndio zitatoa sauti.
Sasa maswali ni haya;
1. Hicho kinga'muzi nilitengeneza mimi?
2. Kwa nini wasitoe taarifa kuwa wenye ving'amuzi aina fulani wanapaswa ku update ili wapate huduma nzuri?
3.Je hizo gharama za ku upadate ziwe za mteja wakati ving'amuzi ni vya kwao?
Walichonichefua zaid ni kuondoa channelsle zenye akili kama Nat Geo Wild, Nat Geo Explorer, Fox Movies, na Fox News na kutuachia matakataka. Yaani sina hamu na Startimes.