Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Habari zenu wanaJamiiForums

Je una tatizo lolote unapotumia huduma zetu? Unaushauri wowote ili kuboresha huduma zetu?

Tafadhali tunaomba utumie thread hii, ili tukusaidie. Tafadhali tunaomba unapokuwa na tatizo ili tukusaidie kirahisi.

1. Utaje tatizo lako
2. Taja sehemu unayoishi
3. Pia kama unaweza tunaomba ututumie na namba yako ya smartcard!

STARTIMES tutajibu maoni, malalamiko na ushauri ule tu ambao utakuwa umejitosheleza na wenye nia ya kutusaidia kuboresha huduma zetu.

kumbuka namba zetu za huduma kwa wateja ni 0764700800 au 0677700800

Ahsanteni sana na karibuni nyote.
Tatizo lenu hamna chanels za maana mfano clouds tv, zbc nk. Mtakosa wateja msiposahihisha hili
 
DSTV wako vizuri sana hasa picture quality ni excellent! Azam na wenzie bei chee ila poor picture quality
 
Kusema ukweli natumia startimes toka 2013.
Lkn kwa sasa huduma ni mbovu sana.
Wametoa clouds tv na nageo world ya wanyama.Kila nikiwapigia simu braabraa tu.
Alafu mvua ikinyesha hata kama ni ndogo no signal.
Wife amenishawishi tununue diesi tivi.
Kifurushi kimeisha jana najichanga niingie kwa mabingwa wa soka.
 
Leo hakuna Huduma. Namba yangu 02035005630 nimelipa hadi December tarehe 9, 2019 iweje leo hakuna kitu kabisa?
 
Naombeni msaada wa frequency za Startimes nimekwama ndugu zangu.
 
Nenda jukwaa la habari mchanganyiko wana uzi wao, uko pinned pale juu.
 
Mimi nipo Dar nimelipia kifurushi cha 21,000 leo ni wiki ya pili sijaunganishwa naambiwa signal ziko chini,nimemtafuta fundi wao na yeye hadithi tu,nafikiria kuhama service ni poor sana.iweje ulipie kifurushi kuupdate iwe muda mrefu hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nipo Dar nimelipia kifurushi cha 21,000 leo ni wiki ya pili sijaunganishwa naambiwa signal ziko chini,nimemtafuta fundi wao na yeye hadithi tu,nafikiria kuhama service ni poor sana.iweje ulipie kifurushi kuupdate iwe muda mrefu hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app

habari yako Imapro, tafadhari tutumie namba yako ya mawasiliana pia namba ya kadi kwa msaada zaidi1
 
Wakuu za asubuhi.

Nipo hapa Ofisini kwangu nashangaa hamna channel yoyote inayopatikana Startimes. Ujumbe inaoandika ni "No service".

Anyone experiencing the same?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari,naomba kujuzwa kama mmebadirisha kulipia vifurushi maana wiki mbili nililipia Nyota elfu 7 leo kimekata mimi ninatumia Antenna sio dish

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wiki mbili nililipa elfu 7 Nyota leo hii naambiwa nilipie, mimi ninatumia Antenna sio dish. Je, kuna mabadiliko ya bei kununua hivi vifurushi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom