Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Habari zenu wanaJamiiForums

Je, una tatizo lolote unapotumia huduma zetu? Unaushauri wowote ili kuboresha huduma zetu?

Tafadhali tunaomba utumie thread hii, ili tukusaidie. Tafadhali tunaomba unapokuwa na tatizo ili tukusaidie kirahisi.

1. Utaje tatizo lako
2. Taja sehemu unayoishi
3. Pia kama unaweza tunaomba ututumie na namba yako ya smartcard!

STARTIMES tutajibu maoni, malalamiko na ushauri ule tu ambao utakuwa umejitosheleza na wenye nia ya kutusaidia kuboresha huduma zetu.

kumbuka namba zetu za huduma kwa wateja ni 0764700800 au 0677700800

Ahsanteni sana na karibuni nyote.
Natumia king'amuzi cha antenna ni mwaka wa tatu sasa sipati Chanel kadhaa kama vile ETV, TABIBU, ATN, ARISE AND SHINE, HOPE nazingine. Naomba msaada. Naishi Tegeta MBWENI JKT.
 
Yaani takri bani week 2 sasa mchana kutwa Channel zote hakishiki ila ikifika saa 1 jioni zinafunguka zote.

Mbaya zaidi leo siku ya 3 ile channel ya Star Swahili ndo ina scratch sana na haionyeshi kitu.

Ukiwapigia cm wahudumu kila mtu na majibu yake.

Naomba wajuzi wa hizi mambo wanishauri.
 
Nina shida na remote control za TV za startimes zile za mwanzo kabisa, nikitumia hizi remote mpya ambazo si za TV hizo inasababisha nishindwe ku operate kwenye ku play USB

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu msaada king’amuzi changu cha star time dish kinanletea sms ifuatayo card problem check card please insert your smart card again & make sure the direction is correct nafata hayo maelekezo lakin ngoma imegoma any solution pls
 
Back
Top Bottom