Mimi ni mteja wenu tangu mwaka 2015. Nakumbuka kipindi hicho kifurushi cha chini kabisa kiliuzwa TSH 6,00/= kama sikosei. Ila leo mwaka 2021 kifurushi kinaanzia TSH 10,000/=. (Kifurushi cha nyota)
Swali langu, ni kwa nini kipindi kile mlikuwa mna wateja wachache lakini bei ya kifurushi ilikuwa chini, lakini leo wateja wengi halafu bei ya vifurushi ipo juu?
Mapendekezo;
Naomba mpitie bei ya vifurushi upya ili mumguse kila mteja.
Kwa mfano, ningependekeza, channeli za sports zile nne ziwe kwenye kifurushi cha nyota (TSH 10,000/=) kwa sababu, zinarusha ligi za Ulaya ila siyo England.
Niwaambiee tu ukweli, kule upande wa pili mtu analazimika kununua kifurushi kwa TSH 20,000/= kwa sababu ya ligi ya bongo (VPL), FA ya England, na baadhi ya mechi za EPL.
Sasa nyie mnaweka channeli za michezo kwenye kifurushi cha 20,000/= wakati hizo ligi ni nzuri ila siyo maarufu, binafsi siwezi kuzifuatilia. Kama nadanganya, hebu angalieni kwenye statistics zenu muone kifurushi cha Uhuru (20,000/=) kina wateja wangapi!
Punguzeni bei ya vifurushi mpate wateja wengi.