Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

StarTimes Tanzania Kwanini mmeondoa local channels zote kwenye king'amuzi changu cha antena?. Kama mmeziondoa sio bure tena niachane na nyie kabisa. Decoder yangu ni Na. 02155934461
 
Ujumbe ni NO ACCESS NOT SUBSCRIBED ila hata hizo local channels zimefutwa yaani sizioni katika list
Kama channel haziko kwenye orodha ya channel inamaana zimetoka kutokana na antena/dish lako kupata shida. Jaribu kufanya automatic search; kama haujazipata rekebisha dishi/antena yako kabla ya kufanya automatic search.

Sent from my SM-N920C using JamiiForums mobile app
 
Hata kwangu hazipo kabisa.
Kumbe hili litakuwa tatizo la wengi,startimes mturejeshee local channels (FTA) kabla hamjakimbiza wateja maana hata bei za vifurushi vyenu ni za kibepari 15000 kwa 30000!!!! Angalau mpoze bei iwe kama zamani mtu ulikuwa na uwezo wa kununua kifurushi cha 6000 kwa mwezi
 
Hapana hakuna tatizo hili ni setup kwa mteja husika.

Karibu

Sent from my SM-N920C using JamiiForums mobile app
 
Habari yako. Suala la Bollywood lugha ya kiswahili tunalifanyia kazi. Unaweza endelea kutizama kwa lugha ya kiingereza au pia channel nyingine kwa lugha za lugha ya kiswahili

Sent from my SM-N920C using JamiiForums mobile app
Nilihama kutumia king'amuzi chenu sababu ya kuondoa Bollywood Bollywood swahili

Wengine hatujui kingereza

Kama hamrudishi basi
 
Hili zoezi nimelifanya ila hazijarudi bado. Mbona zingine zipo vizuri? Channel ninazozikosa ni ITV, EATV, STAT TV na CLOUDS TV.
 
Sipati channel ya capital tv.... Ni kwamba haipo kwenye kingamuzi chenu au shida ni nini?
 
Sipati channel ya capital tv.... Ni kwamba haipo kwenye kingamuzi chenu au shida ni nini?
Habari yako. Capital TV haipatatikani katika kisimbuzi cha StarTimes. Tafadhari fuatilia unaweza kuangalia channel kama eatv, tve, clouds, wasafitv zinamaudhui sawa.

Karibu

Sent from my SM-N920C using JamiiForums mobile app
 
Nilikuwa natumia antenna sasa nimehamia kwenye dish nilichogundua mvua inaponyesha au wingu zito huduma haipatikani sasa sielewi ni kawaida au mfungaji kafanya kazi chini ya kiwango

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Habari yako, mfumo wa DTT (antena) hauna shida kabisa kwenye hali ya hewa (hauhathiriwi kabisa) ukilinhanishwa na DTH (dish) ambao nao ni kwa kiasi kidogo.

Tunashauri ufunge vizuri dishi/antena yako

Sent from my SM-N920C using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…