Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Habari zenu wanaJamiiForums

Je, una tatizo lolote unapotumia huduma zetu? Unaushauri wowote ili kuboresha huduma zetu?

Tafadhali tunaomba utumie thread hii, ili tukusaidie. Tafadhali tunaomba unapokuwa na tatizo ili tukusaidie kirahisi.

1. Utaje tatizo lako
2. Taja sehemu unayoishi
3. Pia kama unaweza tunaomba ututumie na namba yako ya smartcard!

STARTIMES tutajibu maoni, malalamiko na ushauri ule tu ambao utakuwa umejitosheleza na wenye nia ya kutusaidia kuboresha huduma zetu.

kumbuka namba zetu za huduma kwa wateja ni 0764700800 au 0677700800

Ahsanteni sana na karibuni nyote.
Waambieni channel ten channel yao inapiga kelele, warekebishe sauti, kwenye channel za watoto ongezeni boomerang na cartoon network
 
Kwa nn mlisema ITV TBC NA LOCAL channel zote ni bure leo nimechelewa kuweka vocha naambiwa smart cadi yako haingiiliani maana yake ya kwangu ni ya zamani to upgrade au ?
 
Kuna hili suala la kuhama kifurushi mf. toka smart kwenda nyota bado lipo? mwanzoni eti unapiga *150*63# ukitaka kulipia kifurushi kingine tofauti na ulichokuwa nacho sasa.
 
Startimes hamna majibu humu hivi kwanini msiwe specific mpaka kupigiana simu,mfano nataka kuunga kifurushi mpaka mpigiwe, nadhani kuwe na chaguo katika mfumo wa ulipaji kifurushi, mfano kwa m-pesa nikisha ingiza namba ya smart card ije viwango vya kulipia na majina ya vifurushi,mwisho naomba kufahamu kifurushi cha wiki cha smart ni shilingi ngapi.
 
Startimes nyie washenzi mmezuia chanel zote za Bure
Startimes channel za bure wamefuta mkuu hadi ulipie kwanza, wameshazoea kudanganya wateja- It's better uamie Dstv at least mkuu if possible, huko unaweza lipia kifurushi cha 9000 plus na uka-enjoy quality na vipindi tofauti.
 
Kwa nn mlisema ITV TBC NA LOCAL channel zote ni bure leo nimechelewa kuweka vocha naambiwa smart cadi yako haingiiliani maana yake ya kwangu ni ya zamani to upgrade au ?
Hongera sana na ahsanteni statimes.

Mmenitendea haki sana leo.

1. Jana nilifanya malipo ya kifurushi cha 21000 bahati mbaya nikakosea tarakimu ya mwisho ya smatcard. Kwa vile nililipia kwa nmb mobile niliona ujumbe wa nmb mobile kuwa nimelipia kifurushi cha ststimes ila bado chanels hazikufunguka.

Leo jumapili nikawapigia na wakapokea haraka. Baada ya kukagua akaunt yangu ikaonekana haijaingia pesa yoyote. Basi muhudumu akaniambia huenda nimelipia akaunti isioyenyewe, basi kweli ikabidi nirudi kwenye statement za malipo ya nmb na kugundu nilifanya kosa la namba moja ya mwisho haikuwa sahihi.

Kuwapigia mara ya pili nikapokelewa haraka, na kujibu maswali kadhaa na kuahidiwa kurudishiwa malipo kwenye akaunti yangu.

Haikupita dk 10 watoto wanachekelea wananiambia baba tayari!

Big up bazee ba statimes
 
Hongera sana kwa maboresho Big up ila nimehuzunika mbona Chanel ya ID mmeitowa/futa startimes?????
 
Habari wakuu,hv naweza kutumia dish la Dstv kwenye king'amuzi cha startimes??
 
Mimi Nina kingamuzi Cha antenna nimelipia lakini muda huu sipati ESPN zote, channel ten plus napata msg kuwa ni recharge vipi?sijawaelewa
 
Back
Top Bottom