Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Nimuziwa tv yenye built-in decoder utaratibu wa kujiunga na Star times ni upi?
 
Nilinunua kifurushi tar.31 July 2022 na kwamba kingeisha tar. 30 August 2022 lakini kimeisha tar.29 August 2022, naona kama nimepunjwa hiyo siku 1, na hili limetokea mara ya pili naomba ufafanuzi.
 
Naombeni kuuliza hivi Star times ving''amuzi vyao ni HD?
 
Reactions: Ok9
Mtoa comment nikujuze mimi nimeanza kutumia startimes early 2009 baada ya serikali kutangaza Rasmi kwamba Tanzania inahama analogue inaenda digital, mwaka 2017 nikaswitch nikatoka startimes antenna nimehamia dish, nipo startimes kwa miaka 13, ngoja nikurekebishe, hayo mashindano uliyotaja hapo kwa sasa hawaonyeshi zaidi ya Bundesliga tena sio mechi zote. Na ndio maana hata ukipita kwenye ukurasa wao wa Instagram hukuti wanapromote football kama huamini nenda kacheki, na nikujuze tu mtoa mada world cup IPO DSTV tu, hao ndio official broadcasting. Wengine wote hawataonyesha. Startimes kwenye football wamepotea. Sasa hivi mambo yapo AZAM.
 
Sasa hivi wanaonyesha Ndondo cup tu[emoji3][emoji1787][emoji1787]
 
Siyo kwelii Mkuu! Bundersliga game karibia zote jmos zile za saa 10 na nusu Jioni huwa zinaonyeshwa channel tofauti tofauti kuanzia channel 240,Anae bagua ni Azam anachagua mechi moja ya kuonesha Kwa upande wa bundesliga.Azam hawana inshu zaidi ya ligi ya bongo tuu. Hata hiyo Ligi ya Ufaransa haoneshi mechi zote.

Star times wanaonesha La Liga,Ligi ya Scotland,Ligi ya uholanzi,Ligi ya Marekani,Ligi ya Uingereza daraja la kwanza,Uefa nation league,Ligi ya china na Sasa hivi kuna Ligi ya Brazil.
 
Wazoefu mtujuze naweza pata tamthilia hizi kwasababu zingine zinagusa maisha yetu kabisa, kama ile ya walima uyoga... Zinafurahisha sana. Tusaidieni tutawalipeni jamani
 
Startime mna tatizo ghani mbona mlikuwa Bora na Sasa huduma dhaifu mfano mimi nipo Moro Leo ni siku ya Tano Toka nimelipia huduma zenu sipati Chanel ya Aljazira,AMC movie,E.ENG,,NGW E,CGTN DOC,ST SPORTT PREMIUM,ESPN,ESPN2,CGTN,BBC WORLD,TRACE MZIKI Chanel zingine zipo mara hupati tatizo ni kitu ghani zinadai please reachage wakati nimelipia full package Ina boa sana
 
startime customer care mnatapeli wateja juzi mlinipigia simu kuwa kuna ofa ya vifurushi nikalipia lakini imekuwa tofauti na mlichoniambia
 
Chanel nyingine ni bure kwenye antenna ila kwenye dish za kulipia
 
Jamani Startimes kuna tatizo gani leo siku ya nne kama sio tano, ikifika saa 8:50 hivi hadi saa 9:08 mchana kisimbusi chenu kina kata signal baada hapo signal inarudi,nimefanya auto search ,haisaidii,na hakuna mvua ni jua limewaka kawaida tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…