Na Didas Tumaini
Majivu yanayotumika siku ya Jumatano ya majivu yanatokana na matawi ya mitende yaliyochomwa,matawi haya ni yale yaliyotumika katika jumapili ya matawi/mitende iliyopita.Matawi haya yalitumika kumlaki Yesu alipokuwa akiingia Yerusalemu kwa shangwe akijiandaa kufa kwa ajili yetu.
Majivu haya hubarikiwa katika ibada ya misa ya jumatano ya majivu na hupakwa katika paji la uso kwa wale waumini waliohudhuria ibada hiyo.Ni ishara ya majuto na hutukumbusha kuwa sisi hapa duniani ni wasafiri tu hivyo tujute dhambi zetu na tujiweke tayari.Majivu hayo yaliyobarikiwa sio sacraments bali ni vijisakraments kama ilivyo kwa rozali,scapulari n.k.
Biblia inaonesha pia hata wayahudi walipomkosea Mungu walijipaka majivu kama ishara ya toba na majuto.(Esta 4:1-3,Mathayo 11:21,Luka 10:13,Yeremia
6:26,Isaya 61:3.Ezekiel 27:30)
Labda utajiuliza ni kwa nini tunapakwa kwenye paji la uso na sio sehemu nyingine ya mwili,ni kwasababu ,ishara yoyote inayowekwa katika paji la uso inaonesha ni *'Muhuri wa Mungu' na 'umiliki wa Mungu juu yako'.*
Rejea Ufunuo 7:3;9:4;14:1,Ezekieli 9:4-6
Tunapochorwa alama yoyote ya ishara ya msalaba either siku ya ubatizo kwa mafuta matakatifu au katika ibada au sakramenti yoyote ile ina maanisha kwamba sisi tupo chini ya milki ya Mungu,tupo chini yake yeye aliyetufia msalabani.
Kwa wakatoliki,majivu yanatukumbusha kuwa kipindi cha kwaresma kinaanza,kipindi cha toba na mfungo kwa ajili ya maandalizi ya pasaka.Katika kipindi hiki wakatoliki tunakumbushwa tumrudie Mungu kwa mioyo yetu yote (Yoeli 2:12)
Sala inayotumika wakati wa kupakwa majivu ni “wewe ni mavumbi na mavumbini utarudi” (Mwanzo 3:19),maneno haya waliambiwa Adam na Eva baada ya kumwasi Mungu,ilikuwa ni adhabu ya kutomtii Mungu na kifo ndio kilichokuwa adhabu kwa dhambi waliyoifanya wazazi wetu wa kwanza.
Kumbe siku hii ya majivu ni siku ya kutukumbusha kuwa ipo siku tutakufa na lazima tujiweke tayari kwa kila wakati.
Ndimi
DidasTumaini
Sent using
Jamii Forums mobile app