Startimes waoneshaji rasmi wa Kombe la Dunia 2018 Urusi

Hawa hawatakua na HD Channel kwenye hizi mechi maana Vingamuzi vyao haviko HD.

Habari yako Tissaphernes, tafadhari usipotoshe habari ambazo hauna uhakika nazo, chanel zetu za michezo ST WORLDFOOTBALL, STSPORTSPREMIUM ni HD, Pia vingamuzi vyetu combo ni HD! Tafadhari kuwa muangalifu unapotoa taarifa usizokuwa nazo!
 
Hilo neno.WAONESHAJI RASMI WA KOMBE LA DUNIA.limekaa kitapeli sanaaa.na linanikera kwa kweli.
aliyewachagua kuwa rasmi ni nani?kwani wenzenu sio waonyeshaji rasmi?


Habari yako mjingamimi tafadhari je unamaoni yoyote kuboresha huduma zetu!
 
Tunapenda kuwajulisha watanzania wote kuwa Startimes tumekuwa ni waonyeshaji rasmi wa michuano ya kombe la dunia Russia 2018 itakayo anza June 14 mpaka July 15 2018.
Kwa nini mmezibadilishia package baadhi ya channel?Mfano, Sports Arena ilikuwa katika kifurushi cha Mambo, sasa hivi ipo katika Uhuru. Channel nyingi sana zimepelekwa Uhuru package ambayo ni lazima ulipe zaidi ili kuiona au uione kwa bei ileile lakini kwa muda mfupi zaidi. Why?
 
Kweli watanzania ni walopokaji. .. Mimi natumia king'amuzi cha startimes chenye HD na tv yangu ya LG.... Nimeunganisha na HDMI cable... Kila mtu akifika lazima ashangae na aulizie hiki king'amuzi... .Picha ziko clear na mzuri sana.... Mnaosema picha mbaya mnatumia vipi? Au mnaunganisha HD decoder kwenye TV chogo? Startimes mko vizuri sana aisee...
 
Lazima utakuwa unalipwa!! Decorder gani ya StarTimes Tanzania ina slot ya HDMI? Kwanza ukiwa bondeni kidogo tu inakatakata,nimeanza kutumia startimes mwaka 2010 na sijawahi kuona tofauti yoyote hadi sasa,picha zinaganda vilevile,zina kivuli vilevile,Startimes bado wana safari ndefu ili kuwaridhisha watazamaji wenu! Msiishie tu kuangalia idadi ya wateja,ni lazima tu mngekuwa na wateja wengi maana muliwahi soko,tulitegemea mngekuwa mbadala wa DSTV kwenye issue ya bei na ubora ila mumeishia kwenye bei tu! Ubora bado sana!!
 
Hilo neno.WAONESHAJI RASMI WA KOMBE LA DUNIA.limekaa kitapeli sanaaa.na linanikera kwa kweli.
aliyewachagua kuwa rasmi ni nani?kwani wenzenu sio waonyeshaji rasmi?
Basi unajiona Meeesi kwa huu ukosoaji...unajiona mjanja sana
 

habari yako Faru kabula, chanel hizi za michezo zinapatikana kuanzia kifurushi cha mambo, mteja akilipia kifurushi cha mambo atapata chanel zote hizi za michezo!

[HASHTAG]#kombeladuniakiswazi2018startimes[/HASHTAG]
 
Unajitahidi kujibu kwa umakini, nilinunua ving'amuzi viwili 2010 vya antenna. Nikirudisha nikataka vya dish kuna punguzo?

habari yako Donnie Charlie, hapana, ila kwa sasa vingamuzi vyetu vya dishi tumetoa punguzo maalum kwa ajili ya kombe la dunia, bei yake ni sawa na kulipia package mwezi 1 unapata king'amuzi bure na unaangalia miezi mpaka mitatu!

[HASHTAG]#kombeladuniakiswazi2018startimes[/HASHTAG]
 

Ahsante sana! karibu ufurahie nasi, hivi karibuni tumeboresha zaid na zaid!
 
Mimi natumia startimes na ndani yake unaweza kutazama free TBC1 (Kituo cha luninga ambacho sikpendi kabisa) lakini nimesikia watatumia kodi yangu ninayolipa kila siku ili waoneshe kombe la dunia bure.
Je, hichi ndicho ambacho mleta mada unamaanisha hapa?
 

Habari yako Capt Tamar, startimes ya sasa sio startimes ya mwanzo, tuna decoder COMBO, ambazo ni 2 in 1 (satelite na telestrial) pia ni HD decoder (ndizo ziko sokoni sasa), pia tuna SMART Decoder (tembelea maduka yetu utajionea), pia startimes decoder tumeanza kufanyia 'OUTUPDATE' ambapo zinajiupdate directly huko!

pia nataka nikwambie mvua ikinyesha ni decoder ya startimes pekee kwa sasa ambayo huwa haiathiriwi na mvua ukilinganisha na decoder zingine!

Tafadhari kama decoder yako inakusumbua fika katika duka letu lilipo karibu nawe utabadilishiwa




 

Habari yako Zanzibar-ASP, startimes tutaonyesha kombe la dunia kupitia chanel zetu za Startimes
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…