sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Ni mara chache sana mtu atapost facebook na instagram, inaweza kuwa mara 1 kwa mwezi lakini huku status za whatsapp mtu anaweza kupost kila siku maana hata watu wanaoziona ni wale aliowasevu na anaweza kuwachuja zaidi, pia hata watu watao like ama ku comment ni siri yake sio wazi wazi.
Imekuwa ni njia nzuri sana ya kuhabarishana, kuburudishana, kuelimishana, n.k na ni ngumu kukuta mtu anapost upuuzi maana kwenye namba alizosevu wapo hata wazazi wake.
- Mtu akifiwa tutajua kwa haraka kupitia status
- Mtu akipanadishwa cheo hupendelea zaidi status kupost.
- Mtu akipata mtoto atapendelea kutumia WhatsApp status kutufahamisha kwa picha
- Mtu akioa tutaziona video kwa status watu wake tunaomjua
- Tunawajua hata watoto wa wenzetu wa mbali kupitia status
- Marafiki wa zamani kam wa shule ya msingi pia inakuwa burudani kuona status zao
Imekuwa ni njia nzuri sana ya kuhabarishana, kuburudishana, kuelimishana, n.k na ni ngumu kukuta mtu anapost upuuzi maana kwenye namba alizosevu wapo hata wazazi wake.