STEALTH (LOW OBSERVABLE) TECHNOLOGY | Teknolojia ya ndege kutoonekana/kutotambulika na rada (RADAR)

[emoji16][emoji16][emoji16] aisee na baadhi ya materials zinakuwa extracted hapa hapa..
 
[emoji16][emoji16][emoji16] aisee na baadhi ya materials zinakuwa extracted hapa hapa..
Yani nchi ambayo haina research and development itateseka sana kwenye teknolojia. Vyuo vyetu tunakaa sana library na kufungua nati, kuzifunga na tukizidi sana kuchomelea. Sasa hapo utoe mtu akagundue nini.
Kwenye afya kama Prof. wa UDSM nilimuona anapaki dawa feki ya corona kwenye chupa za tomato, barakoa kutengenezwa chuo ilioneshwa TBC. Hii inatosha kuonesha masuala ya radar na mengine magumu tuyaache kabisa maana hata madogo hatuyawezi.
 
Samahani mkuu mimi maamuma kabisa naomba msaada mdogo tu pengine nitaelewa mnabishania nini



Naomba kujua maana ya Bomber na Fighter tu
 
Awamu hii itatuthubutisha tuipe muda
 
Daaah
 
Samahani mkuu mimi maamuma kabisa naomba msaada mdogo tu pengine nitaelewa mnabishania nini



Naomba kujua maana ya Bomber na Fighter tu
Bomber ni ya kubebea mabomu mengi na kudondosha kwa adui. Hii hufanya hata carpet bombing (kudondosha mengi kwa mfurulizo, kwa distance fulani).
Bomber kuna long range na medium range, sijawahi sikia low range bombers. Bomber imetoka kwenye neno "bomb"-bomu.

Air fighter hii hupambana na ndege za adui kwenye anga, ukitaka kupiga bomber hutumii bomber mwenzake bali utatumia fighter. Hizi zinakuwa na air to air missiles kadhaa na speed kubwa. Hizi pia zinakuwepo air superiority fighter ambazo zinahakikisha hakuna ndege ya adui inatamba kwenye anga hilo.

Pia kuna tanker, inabeba mafuta na huweza kujaza ndege zingine angani.
Reconnaissance, inafanya uchunguzi wa anga na ardhi kujua adui yuko vipi.
Airborne early warning, hizi hutoa taarifa zozote za hatari angani au baharini.
Na nyingine nyingi tu.
Kwa Tanzania hatuna hata moja hapa.
 
Sasa haya yamekujaje kwenye masuala ya Stealth
 
Tutapunguza muda wa kutengeneza kwa kuiba tech kijasus ndan ya Iran na israel km mision ikiisha salama inshaaaallah.
 
Tutapunguza muda wa kutengeneza kwa kuiba tech kijasus ndan ya Iran na israel km mision ikiisha salama inshaaaallah.
Mkuu huwezi iba tech Israel wakati Mossad ndo wanakuja kutufundisha hapa. Kuiba tech hakuwezi fanywa na wasiojulikana hawa wanaotumia Noah, kunaitaji watu wenye akili zao na uwezo, waliopewa mafunzo hayo. Sisi hatuna priorities hizo, wala hatuna uwezo wa kukabiri mikiki ya aina hiyo.
Jambo jepesi ni kununua tech zinazouzwa au kufanya licence production. Wauzaji wa kila tech ni North Korea, wao kila tech waliyonayo ukitaka wanakuuzia lakini wana vikwazo ukikamatwa shauri yako.
Naona tusitoke zaidi kwenye mada, si sawa.
Tunajadiri stealth tech
 
Samahani mkuu mimi maamuma kabisa naomba msaada mdogo tu pengine nitaelewa mnabishania nini



Naomba kujua maana ya Bomber na Fighter tu
Nafikiri umekwisha kupata majibu ya swali lako kuhusiana na hilo. Labda pengine nami niongezee kidogo:

Bomber ni ndege ya kijeshi mahususi kwa ajili ya mashambulizi mazito na mepesi ya ardhini kutokea angani. Kwa maana ya kwamba ndege hizi hutumika katika kufanya mashambulizi katika mtindo wa kushusha ama kuangusha mabomu kutokea angani.

Bombers zimegawanyika hasa katika makundi mawili;

1) Strategic bombers
2) Tactical bombers

Strategic bombers:
Kundi hili hutumika katika majukumu ama missions za mbali (long-range) kwa ajili ya kuangusha mabomu katika maeneo ya kimkakati. Maeneo ama vituo vya kimkakati ni vile ambavyo ndio nyenzo ama msingi mkuu wa nchi katika kuendesha vita kama vile miundombinu za kiuchumi, viwanda n.k. ambavyo ndivyo chanzo cha rasilimali za kuiwezesha nchi kuingia vitani. Bombers hizi hufahamika zaidi kama 'heavy bombers' kutokana na uwezo wa kubeba idadi kubwa ya mabomu na kufanya mashambulizi mazito ardhini. Baadhi ya strategic bombers ni B-2 Spirit, B1B Lancer strategic bomber pamoja na Tupolev Tu-160 strategic bomber.

Tactical bombers:
Hizi ni mahususi katika kushambulia miundombinu muhimu za kijeshi. Yaani, vituo vinavyotumika na majeshi ya nchi pekee pamoja na zana zake; kambi za kijeshi, mifumo ya kijeshi ya ulinzi wa anga (air defense systems) n.k.

Dhumuni kuu la tactical bombers ni kudhoofisha miundombinu za kijeshi za adui ili asiweze kuingia vitani. Katika upande huu wa tactical, ni jeshi tu la adui ambalo ndilo hulengwa na mashambulizi tofauti na upande wa strategic. Bomber za aina hii hasa ni ndege ndogo kama vile fighters tofauti na zile za strategic. Mfano: Fighters kama vile; Sukhoi SU-34 pia ndege nyinginezo zenye uwezo wa kufanya majukumu mengi (multi-role); F-35 Lightning II, Eurofighter Typhoon, F-16 Fighting Falcon n.k.

Nihitimishe hapo kuhusu bombers.

Fighter ni ndege ya kijeshi mahususi hasa kwa mashambulizi ya anga kwa anga (air-to-air) ama juu kwa juu dhidi ya ndege zingine pia operesheni mbalimbali za anga. Sifa kuu ya ndege hizi ni kasi kubwa na uwezo wa kubadili badili uelekeo kwa lugha nyingine (maneuverability).

Hizi nazo zimegawanyika kimakundi kuendana na majukumu tofauti tofauti. Baadhi tu ya makundi hayo ni kama ifuatavyo:

1) Air Superiority. Hizi ni mahususi kwa ajili ya kuteka anga la adui na kuzishambulia angani ndege zingine. Mfano, F-22 Raptor. (Hizi ni za kibabe zaidi)

2) Fighter-bomber. Hizi ni kwaajili ya mashambulizi ya anga kwenda ardhini. Hizi hutumika hasa kama tactical bombers kwa ajili ya kushambulia miundombinu za majeshi ya adui kama nilivyoeleza hapo awali.

3) Interceptor. Hizi ni kwa ajili ya ulinzi. Zenyewe ni mahususi katika kuzuia ndege zingine kuvuka ama kuingia katika eneo fulani la anga.

4) Reconnaissance. Hizi ni kwaajili ya ukusanyaji wa taarifa muhimu kupitia anga. Hizi ni mahusui zaidi katika masuala ya kiintelijensia.

5) Multi-role. Hizi hufanya majukumu mengi. Maana yake ni kwamba, zina uwezo wa kutumika katika majukumu tofauti tofauti kuendana na operesheni mbalimbali za kijeshi. Zinaweza kufanya kazi kama air superiority fighter, bomber, interceptor n.k. Mfano; F-35 Lightning II.

Na kadhalika!
 
Shukrani sana kwa elimu hii


Kwa majibu haya mawili ni wapi hamkuelewani?

Nafikiri ilikuwa rahisi kubishana hii ni fighter na hii ni bomber kuliko hii ni bomber/fighter na hii ni stealth
 
Uko vizuri sana nimekuelewa
 
Shukrani sana kwa elimu hii


Kwa majibu haya mawili ni wapi hamkuelewani?

Nafikiri ilikuwa rahisi kubishana hii ni fighter na hii ni bomber kuliko hii ni bomber/fighter na hii ni stealth
Majibu hayo hayana mahusiano ya moja kwa moja na mabishano yeyote bali yamelenga haswa katika zana hizo mbili (bomber & fighter) specifically, si nje ya hapo.

Unasema ilikuwa rahisi mabishano yangelenga kati ya fighter na bomber?

Mabishano yanaweza kutokea popote pale haijalishi ni hapo ama pengine. Pia, hayo mabishano yaliyokuwepo ni ya kawaida tu, naweza kuyaita majadiliano kama njia mojawapo ya kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala haya na yafananayo.
 
Haya maandishi uliyoyaandika yamenisikitisha sana kwani ndiyo ukweli halisi kutuhusu. Lakini mkuu tulikosea wapi na nini kifanyike? Kama mpaka Circuit boards mpaka tuagize kweli? Aisee
 
Daaah MiG 21, J-7 bado tupo 2nd Gen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…