STEALTH (LOW OBSERVABLE) TECHNOLOGY | Teknolojia ya ndege kutoonekana/kutotambulika na rada (RADAR)

Upo vizuri sana.
 
Naamini kila kitu umeweka clear kabisaaa.
 
Daaah MiG 21, J-7 bado tupo 2nd Gen
Hizo Mig-21 Fishbed sidhani kama ziko operational hapa Tanzania. Si ndio zile US walitutuhumu kuwatumia Wakorea (North) kutupatia parts zake. Tulizitumia tangu vita na Iddi Amin nadhani na yeye pia alikuwa nazo.
Hizo J-7G tulizonazo ni copycat ya Mig-21, kitu kilekile. Hata Nigeria wanazo.

Tanzania tunaweza afford angalau J-17 walizonazo Pakistan kutoka China. Hizo modern Mig, Sukhoi, Saab, F, etc tuwaachie Egypt, South Africa na Algeria.
 
Haya maandishi uliyoyaandika yamenisikitisha sana kwani ndiyo ukweli halisi kutuhusu. Lakini mkuu tulikosea wapi na nini kifanyike? Kama mpaka Circuit boards mpaka tuagize kweli? Aisee
Jibu la hili swali watu wenye exposure na nchi zinazoendelea/zilizoendelea kwa kasi wanalo.
Sisi tuna matatizo mengi mno, na hakuna wa kuyaondoa kirahisi. Watu wanaamini wanasiasa ndo wana shida kumbe sio wao tu, ni kwa vile wanaonekana. Jamii nzima matatizo matupu, nyuzi za mabilionea marehemu weusi walioacha mali zikagombewa na familia si unaziona kila siku. Mbona Waarabu na Wahindi hawana.
Civilization ndo inatangulia development yeyote including technological.
 
Hakuna ulazima wa kununua hiyo midege kwa sasa hiyo pesa inabd tufufue kiwanda cha matair Arusha
 
Kwahiyo majadiliano yalifaa kuwa hii ni bomber na hii ni fighter badala ya hii ni bomber/fighter na hii ni Stealth
 
Sahihi kabisa lakini MiG21 Lancer unazingumziaje? Yani unataka kuniambia hata Mirage 2000 hatuwezi?
 
Mkuu FRANC THE GREAT upo kimya tuliishia na RADAR ABSORBING, Kwa habari za RAM na RAM.

Naamini muda mzuri kuendelea
 


Haya hasa ndiyo maswala ya kujadili hapa na sio "stealth technology" au "low observable technology", teknolojia zilizotuzidi kimo, teknolojia rahisi hatuwezi huo ni msiba mkubwa kwetu.
 
Ni Mig-21 Fishbed (silaha zote za Urusi huwa zina NATO reporting names, Fishbed kwa hii).
Lancer ndo B1B, hawa Wamarekani hutoa majina ambayo ndo hutumika hivo hivo NATO. US military ni wazuri sana wa kutengeneza acronym, utakuta kifupisho kama THAAD, DARPA, OSINT, SIGINT, MANPAD, etc yani maneno matamu yanatamkika kabisa lakini ni vifupisho vya maelezo fulani. Sio unakuwa na vifupisho eti PCCB (bora ibaki TAKUKURU).

Hiyo Mirage 2000 za Dassault, Wafaransa ambao wametengeneza pia Rafale mojawapo ya 4+ generation fighter nzuri. Mirage 2000 ni nzuri sana lakini inaelekea mwisho wa utawala wake, tatizo la kumiliki silaha za zamani kuna muda utafika ukose spare parts (umeona nilipogusia 'tetesi' za North Korea kutupa parts za Mig-21). Silaha zinatakiwa kuwa serviceable. Mirage 2000 ni tangu 1978, sio zamani hata kidogo lakini kwa nini nimesema si best option?

•Tanzania tukinunua silaha, tukija kununua tena ni makumi ya miaka. Tafuta list ya vifaru tulivyonavyo uone vya mwaka gani. Sasa tukinunua ndege za 1970s kisha tunapanga kuishi nazo mpaka miaka 30 ijayo kweli zitakuwa na mashiko. Hizo Shenyang J-7G tulizipata around 2012 or 2014 lakini za zamani ingawa zina upgrades. Mirage wanazo India wanazitumia hasa kwenye ground attack.
Zipo ndege nyingi sana za 1970s muhimu kuwe na maintenance lakini tatizo moja kubwa kabisa, integration na silaha mpya utakosa.

•Mirage 2000 ni ya Wafaransa, hatuna mazoea ya kununua silaha kwao. Kuchanganya suppliers kuna shida zake hasa maintenance costs, kuoanisha mifumo ya silaha na training ingawa kuna faida pia.
•Muhimu kabisa kwa nini naona sio best option, operating costs za silaha za kizungu ni kubwa mno. Utauziwa e.g air-to-air missiles, spares kwa bei ndefu.
Mkuu mambo mengi nisichoshe watu na kuchanganya mada.
 
Ina maana hata Uganda inatushinda kwa uchumi?
 
Ina maana hata Uganda inatushinda kwa uchumi?View attachment 1502824
Hizo Su-30 ziko 6. Sijui katika groupings za jeshi ndege sita utaziweka group gani, squadron hazikai, wing hazikai, etc.
Kununua ndege na kuzioperate ni vitu viwili.
Unanunua utakachomudu tu, ukitafuta ndege walizokuwa nazo Indian Air force kwenye vita dhidi ya Pakistan utaona walishinda na ndege gani.
Israel alikuwa na silaha za kawaida lakini kumbe ndizo aliweza kumudu kufanyia training, Waarabu wakaja na silaha nzuri lakini training hawana kwa kuwa ni gharama wakawa wanashindwa mapigano.

Na hawanunui silaha kisa uchumi, wananunua kwa ajili ya ulinzi na wakilinganisha adui ana zana gani. Nchi kama Australia ina uchumi mzuri lakini haina mkazo sana kwenye usalama.
Egypt inanunua silaha nyingi sana kwa kuwa iko maeneo hatarishi, kama zingekuwa sababu za kiuchumi Nigeria na South Africa zingeizidi.
Switzerland ina uchumi lakini hainunui silaha kivile.

Sio hata silaha tu, nilikuwa natazama Bulgaria wana raia hawafiki 10M lakini wanajeshi 300,000. Sisi tuko 55M hata wanajeshi 50,000 hatuna.
Na ukumbuke Uganda ni nchi inayoongozwa kijeshi sijui niseme.
 
appreciation, ujasema tech hi wap
 
Mkuu nilimaanisha hii kitu....

Elbit MiG-21 Lancer

The MiG-21 "Lancer" is not a new plane, but the name given to one of the modifications to the MiG-21 has modernized after the collapse of industries in the former Soviet Union. Once the USSR was over, many users of these planes were practically without assistance, or with limited assistance for only part of the aircraft. The MiG-21 "Lancer", the company modernized ELBIT of Israel, in cooperation with the Romanian industry is one of those versions.
 
Nilikusudia kuquote hapo juu
Pamoja sana, nipe kidogo maelezo ya Suppression of Enemy Air Defence (SEAD) na Destruction of Enemy Air Defence (DEAD) na Electronic Warfare (EW) katika habari za Air defence huwa kidogo vinanichanganya mkuu.
 
Kwa Africa ukiwa na SU-30 6 tu ni nyingi sana ndugu, yani unahesabika kuwa una jeshi la Anga bora.sisi wenyewe tuna F-7 (11) na F-6 (3) tu na bado tunatamba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…