Stendi kuu ya Magufuli sio rafiki, ni laana kwa wasafiri na wasafirishaji jijini

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Inaonekena kuwa ujenzi wa stendi ya mabasi ya magufuli jijini Dar ilijengwa bila kuwashirikisha wadau. Haizingatii desturi, mazoea, utamaduni, uchumi na utaratibu wa wadau.

Ninapotaka kusafiri kwenda au kutoka mikoani hofu yangu kuu ni nitafikaje au nitatokaje stendi ya Magufuli, maana hakuna mabasi yanayofika na kutoka moja kwa moja kwenye stendi ile jambo linalolazimisha nipande bodaboda au nitembee kwa miguu umbali mrefu kutoka pale zilipo daladala za kutoka na kwenda mtaani kwangu. Kama nikiwa na mizigo hali inakuwa mbaya zaidi; itakulazimu uingie mfukoni kukodi usafiri kwenda stendi au kutoka stendi. Ni kero kubwa kwa wasafiri.

Pili, stendi ile ni kama vile haiko Dar es Salaam; iko Kibaha, ni ngumu sana kutoka Chanika, Temeke, Kigamboni, mbagala au katikati ya jiji kwenda stendi ya magufuli. Stendi iko pembeni sana mwa jiji. Kama natoka Arusha kwenda Mbagala na kushushiwa stendi ya magufuli ni kama vile nimepewa adhabu kubwa ya kwenda Mbagala au Temeke.

Tatu, wenye mabasi pia wanakereka sana na stendi ile. Mfano, basi linatoka Mtwara na abiria wote wameshuka Mbagala na temeke Sudan lakini basi linatakiwa liende hadi Mbezi Stendi ya magufuli ni kama vile unawapa adhabu ya kufika Mbezi basi likiwa tupu kwenye foleni.

Jiji ni kubwa sana, haiwezekani mabasi yoooooote yafike Stendi ya magufuli.
Inabidi madaladala yashushe abiria wao karibu kabisa na stendi ya Magufuli
Inabidi kuwe na routes za kwenda Stend ya magufuli kutoka mitaa yote ya jiji.
Kama hakuna abiria wa kushuka stendi ya magufuli kwanini basi lifike stendi ya magufuli

Kila huduma lazima ilenge kutatua changamoto za watu na sio watu walazimike kutatua changamoto za huduma inayotolewa.
 
tatizo ni jiografia ya stendi au uendeshaji wa stendi? i mean, kwa ukubwa wa dar (> 1500 sqr km) ulitaka stendi ijengwe wapi labda ili isilete ''kero'' ambazo umezitaja? haya tuseme ingebakia kisutu au ubungo, malalamiko ulioyaweka hapa yasingekuwepo kwa wengine? kwa ukubwa wa dar hizo stendi zilipaswa kuwepo zaidi ya 5 na ambazo zinaunganishwa kwa mwendokasi i.e ukishuka ktk kwenye basi unapanda mwendo kasi na kuunganisha mbele kwa mbele ...
 
Watu wa Dar ni walalamishi hatari

Sijui mmelewa chips yai....?

Siwaelewagi kwa kweli,

Stendi ya Magufuli, lengo lake ni zuri na litaendelea kuwa zuri mpaka mtakaoisha walalamishi

Watu wa Dar, sjui kama atatokea mtu wa kuwaweza baada ya Magufuli kuondoka..

Ilikuwa hivyo hivyo kwenye vivuko vya Kigamboni, mzee akamwambia mpige mbizi, sisi wa mikoani, huduma za huku ni za hovyo na bei yake juu mara dufu unapolinganisha na Watu wa Dar

Stendi ya Magufuli Mbezi, imekosa usimamizi na maamzi magumu ya serikali basi
 
Inaonekena kuwa ujenzi wa stendi ya mabasi ya magufuli jijini Dar ilijengwa bila kuwashirikisha wadau. Haizingatii desturi, mazoea, utamaduni, uchumi na utaratibu wa wadau.

Ninapotaka kusafiri kwenda au kutoka mikoani hofu yangu kuu ni nitafikaje au nitatokaje stendi ya Magufuli, maana hakuna mabasi yanayofika na kutoka moja kwa moja kwenye stendi ile jambo linalolazimisha nipande bodaboda au nitembee kwa miguu umbali mrefu kutoka pale zilipo daladala za kutoka na kwenda mtaani kwangu. Kama nikiwa na mizigo hali inakuwa mbaya zaidi; itakulazimu uingie mfukoni kukodi usafiri kwenda stendi au kutoka stendi. Ni kero kubwa kwa wasafiri.

Pili, stendi ile ni kama vile haiko Dar es Salaam; iko Kibaha, ni ngumu sana kutoka Chanika, Temeke, Kigamboni, mbagala au katikati ya jiji kwenda stendi ya magufuli. Stendi iko pembeni sana mwa jiji. Kama natoka Arusha kwenda Mbagala na kushushiwa stendi ya magufuli ni kama vile nimepewa adhabu kubwa ya kwenda Mbagala au Temeke.

Tatu, wenye mabasi pia wanakereka sana na stendi ile. Mfano, basi linatoka Mtwara na abiria wote wameshuka Mbagala na temeke Sudan lakini basi linatakiwa liende hadi Mbezi Stendi ya magufuli ni kama vile unawapa adhabu ya kufika Mbezi basi likiwa tupu kwenye foleni.

Jiji ni kubwa sana, haiwezekani mabasi yoooooote yafike Stendi ya magufuli.
Inabidi madaladala yashushe abiria wao karibu kabisa na stendi ya Magufuli
Inabidi kuwe na routes za kwenda Stend ya magufuli kutoka mitaa yote ya jiji.
Kama hakuna abiria wa kushuka stendi ya magufuli kwanini basi lifike stendi ya magufuli?

Tatu, Wenye mabsi
Ukishakuwa na Rais kopo, wahuni watatumia vijisababu uchwara kwa kila namna kukwepa utaratibu.

Kila mtu akiwa na stand yake anakotaka mwenyewe maana yake hakuna nchi hapo.
 
tatizo ni jiografia ya stendi au uendeshaji wa stendi? i mean, kwa ukubwa wa dar (> 1500 sqr km) ulitaka stendi ijengwe wapi labda ili isilete ''kero'' ambazo umezitaja? haya tuseme ingebakia kisutu au ubungo, malalamiko ulioyaweka hapa yasingekuwepo kwa wengine? kwa ukubwa wa dar hizo stendi zilipaswa kuwepo zaidi ya 5 na ambazo zinaunganishwa kwa mwendokasi i.e ukishuka ktk kwenye basi unapanda mwendo kasi na kuunganisha mbele kwa mbele ...
Yaani wangeplan kwa wakati mmoja wakati wanajenga stendi ya magufuli wajenge na stendi ya dalala/mwendokasi/rele za kufikisha na kutoa abiria stendi kuu. Kila wilaya (Temeke, Ilala, Kinondoni) ingekuwa na stendi yake kuu inayounganishwa na stendi ya magufuli kwa barabara za mwendo wa haraka au treni.
 
Wangeweka usafiri wa Moja kwa Moja kutoka njia zote kuu hasa hasa mjini Katikati kuwapeleka na kutoa watu isingekuwa tatizo kubwa
Kuna watu ili kufika stendi ya magufuli lazima waunge daladala mbili hadi tatu; na wakifika Mbezi lazima wakodi pikipiki kuwafikisha ilipi stendi ya magufuli.
 
Watu wa Dar ni walalamishi hatari

Sijui mmelewa chips yai....?

Siwaelewagi kwa kweli,

Stendi ya Magufuli, lengo lake ni zuri na litaendelea kuwa zuri mpaka mtakaoisha walalamishi

Watu wa Dar, sjui kama atatokea mtu wa kuwaweza baada ya Magufuli kuondoka..

Ilikuwa hivyo hivyo kwenye vivuko vya Kigamboni, mzee akamwambia mpige mbizi, sisi wa mikoani, huduma za huku ni za hovyo na bei yake juu mara dufu unapolinganisha na Watu wa Dar

Stendi ya Magufuli Mbezi, imekosa usimamizi na maamzi magumu ya serikali basi
Mbona ile ya Ubungo ilikuwa ya serikali pia? Kulikuwa hakuna usumbufu kwakuwa daladala za aina zote zilikuwa zinashusha abiria karibu kabisa na stendi. Hii hapa wanashindwa nini kuzifanya daladala zote zipitie Stendi ya magufuli kushusha na kuchukua abiria kabla ya kwenda kupaki kwenye stendi za daladala ili kuwaondolea usumbufu wasaafiri?
 
Tatu mara mbili
Nne, wale wamiliki wa mabasi ambao wana vituo binafsi au wana mambasi ambayo yanaazia safari zao kwenye mitaa kama Chanika, magomeni, mbagala, shekilango, mabibo, gongo la mboto nk wana akili sana na wanapendwa sana na abiria wanaotoka au kwenda maeneo hayo. Wanawasaidia sana kuliko kama kila mtu angeanzia na kuishia safari yake stendi ya magufuli.

Kila huduma lazima ilenge kutatua changamoto za watu na sio watu watatue changamoto za huduma inayotolewa.
 
Mbona mwendokasi inashusha hapo hapo Magufuli stendi? Na kwanini unasafiri na mizigo? Kama huna mizigo unaweza kushuka kituo cha daladala cha Mbezi na ukatembea dakika kadhaa kwenda Magufuli stendi

Stendi ya Magufuli imesaidia sana kuondoa foleni maeneo ya ubungo
 
tatizo ni jiografia ya stendi au uendeshaji wa stendi? i mean, kwa ukubwa wa dar (> 1500 sqr km) ulitaka stendi ijengwe wapi labda ili isilete ''kero'' ambazo umezitaja? haya tuseme ingebakia kisutu au ubungo, malalamiko ulioyaweka hapa yasingekuwepo kwa wengine? kwa ukubwa wa dar hizo stendi zilipaswa kuwepo zaidi ya 5 na ambazo zinaunganishwa kwa mwendokasi i.e ukishuka ktk kwenye basi unapanda mwendo kasi na kuunganisha mbele kwa mbele ...
Kama Dar ilitakiwa kuwa na Stendi moja ya bus za mikoani mkoa ilipaswa iwe Posta, Kariakoo au Kigamboni. Hata hivyo Dar haipaswi kuwa na Stendi moja kubwa bali zaidi ya nne za ukubwa wa stendi ya Magufuli na bus pia ziruhusiwe kutumia ofisi zao binafsi kama stendi.
 
Yaani wangeplan kwa wakati mmoja wakati wanajenga stendi ya magufuli wajenge na stendi ya dalala/mwendokasi/rele za kufikisha na kutoa abiria stendi kuu. Kila wilaya (Temeke, Ilala, Kinondoni) ingekuwa na stendi yake kuu inayounganishwa na stendi ya magufuli kwa barabara za mwendo wa haraka au treni.
Hawana uwezo huo wa kufikiri hivyo.
 
Mbona mwendokasi inashusha hapo hapo Magufuli stendi?
Mwendokasi zinatokea maeneo yote Dar?
Na kwanini unasafiri na mizigo?
Uko serious kabisa mkuu? Kwa hiyo tusisafiri na mizigo?
Kama huna mizigo unaweza kushuka kituo cha daladala cha Mbezi na ukatembea dakika kadhaa kwenda Magufuli stendi
Kama una mizigo, kwa nini isiwepo namna daladala ziruhusiwe kushusha karibu kabisa na stendi, kama ilivyo kwa mwendokasi?
Stendi ya Magufuli imesaidia sana kuondoa foleni maeneo ya ubungo
Ni kweli.
 
Mwendokasi zinatokea maeneo yote Dar?

Uko serious kabisa mkuu? Kwa hiyo tusisafiri na mizigo?

Kama una mizigo, kwa nini isiwepo namna daladala ziruhusiwe kushusha karibu kabisa na stendi, kama ilivyo kwa mwendokasi?

Ni kweli.
Mwendokasi inaendeea kujengwa, tayari kuna mwendokasi kutoka mbagala, soon kutakuwa na mwendokasi kutoka gongolamboto na Tegeta

Hata sasa haijalishi unatokea wapi Ukifika Morogoro road lazima ukutane na mwendokasi

Huwa sioni ulazima wa kusafiri na mizigo
 
Yaani wangeplan kwa wakati mmoja wakati wanajenga stendi ya magufuli wajenge na stendi ya dalala/mwendokasi/rele za kufikisha na kutoa abiria stendi kuu. Kila wilaya (Temeke, Ilala, Kinondoni) ingekuwa na stendi yake kuu inayounganishwa na stendi ya magufuli kwa barabara za mwendo wa haraka au treni.

hata kama wangefanya bado isingekidhi mahitaji ya mji zaidi km za mraba 1500 na watu zaidi ya miloni 5, kwa kifupi dar haikupaswa kuruhisiwa kukuwa na kusambaa zaidi ya ilivyokuwa zamani bila ya pia kukuza miundo mbinu, stendi moja hakuna miujiza yoyote unayoweza kufanya zilitakiwa ziwe nyingi, dar unakwenda km zaidi 20 bado uko mji huo huo, uliona wapi?

na siyo kituo cha mabasi tu fire is same story kama unaishi tegeta kwa mfano nyumba ikishika moto fire inatakiwa isafiri zaidi ya km 20 kuja kuzima moto, na hiyo tegeta siyo mwisho wa chaos ya dar bali inakwenda zaidi mpaka boko, bunju na kuendelea wote hao wanategema fire moja isafiri kutokea upanga kuja kuzima motó, sasa hiyo ni akili au matope? ...
 
Yaani wangeplan kwa wakati mmoja wakati wanajenga stendi ya magufuli wajenge na stendi ya dalala/mwendokasi/rele za kufikisha na kutoa abiria stendi kuu. Kila wilaya (Temeke, Ilala, Kinondoni) ingekuwa na stendi yake kuu inayounganishwa na stendi ya magufuli kwa barabara za mwendo wa haraka au treni.
mwendokasi zilikuwepo pale, ngoja tuone zile za blue mpya zilizoletwa kama wataweka pale
 
Mbona mwendokasi inashusha hapo hapo Magufuli stendi? Na kwanini unasafiri na mizigo? Kama huna mizigo unaweza kushuka kituo cha daladala cha Mbezi na ukatembea dakika kadhaa kwenda Magufuli stendi

Stendi ya Magufuli imesaidia sana kuondoa foleni maeneo ya ubungo
Huyu yeye anachokitaka pale Magufuli stendi kuwe na Stendi nyingi ya karibu zaidi au tuseme stendi ya Mwendokasi iwekwe pale nje yaan mtu akitoka ndani anakwea Mwendokasi kapotea mpaka Mbagala kakwea kupotea na Mwendokasi mpaka Tegeta, kakwea Mwendokasi kapotea mpaka Gongolamboto sijui Chanika huko, hivyo ndivyo anavyotaka huyu kijana yaan maisha mbilinge mbilinge hayawezi anataka maisha mseleleleko
 
Back
Top Bottom