Stendi kuu ya Magufuli sio rafiki, ni laana kwa wasafiri na wasafirishaji jijini

Stendi kuu ya Magufuli sio rafiki, ni laana kwa wasafiri na wasafirishaji jijini

Huyu yeye anachokitaka pale Magufuli stendi kuwe na Stendi nyingi ya karibu zaidi au tuseme stendi ya Mwendokasi iwekwe pale nje yaan mtu akitoka ndani anakwea Mwendokasi kapotea mpaka Mbagala kakwea kupotea na Mwendokasi mpaka Tegeta, kakwea Mwendokasi kapotea mpaka Gongolamboto sijui Chanika huko, hivyo ndivyo anavyotaka huyu kijana yaan maisha mbilinge mbilinge hayawezi anataka maisha mseleleleko
Tatizo lake amekariri kusafiri na mizigo
 
Yaani wangeplan kwa wakati mmoja wakati wanajenga stendi ya magufuli wajenge na stendi ya dalala/mwendokasi/rele za kufikisha na kutoa abiria stendi kuu. Kila wilaya (Temeke, Ilala, Kinondoni) ingekuwa na stendi yake kuu inayounganishwa na stendi ya magufuli kwa barabara za mwendo wa haraka au treni.
Mbona Ma-bus ya Mwendokasi yana kituo hapo hapo kwenye mlango wakuingilia Stendi ya Magufuli?? Mkuu ulishafika Stendi ya Magufuli kweli?

Pia kituo cha daladala kipo karibu tu unavuka barabara ya Morogoro kwa kupitia flyover ya watembea kwa miguu na unapata Daladala za routes mbalimbali za Dar!!?

Nafikiri wewe utakuwa na matatizo ya akili siyo bure!!
 
Inaonekena kuwa ujenzi wa stendi ya mabasi ya magufuli jijini Dar ilijengwa bila kuwashirikisha wadau. Haizingatii desturi, mazoea, utamaduni, uchumi na utaratibu wa wadau.

Ninapotaka kusafiri kwenda au kutoka mikoani hofu yangu kuu ni nitafikaje au nitatokaje stendi ya Magufuli, maana hakuna mabasi yanayofika na kutoka moja kwa moja kwenye stendi ile jambo linalolazimisha nipande bodaboda au nitembee kwa miguu umbali mrefu kutoka pale zilipo daladala za kutoka na kwenda mtaani kwangu. Kama nikiwa na mizigo hali inakuwa mbaya zaidi; itakulazimu uingie mfukoni kukodi usafiri kwenda stendi au kutoka stendi. Ni kero kubwa kwa wasafiri.

Pili, stendi ile ni kama vile haiko Dar es Salaam; iko Kibaha, ni ngumu sana kutoka Chanika, Temeke, Kigamboni, mbagala au katikati ya jiji kwenda stendi ya magufuli. Stendi iko pembeni sana mwa jiji. Kama natoka Arusha kwenda Mbagala na kushushiwa stendi ya magufuli ni kama vile nimepewa adhabu kubwa ya kwenda Mbagala au Temeke.

Tatu, wenye mabasi pia wanakereka sana na stendi ile. Mfano, basi linatoka Mtwara na abiria wote wameshuka Mbagala na temeke Sudan lakini basi linatakiwa liende hadi Mbezi Stendi ya magufuli ni kama vile unawapa adhabu ya kufika Mbezi basi likiwa tupu kwenye foleni.

Jiji ni kubwa sana, haiwezekani mabasi yoooooote yafike Stendi ya magufuli.
Inabidi madaladala yashushe abiria wao karibu kabisa na stendi ya Magufuli
Inabidi kuwe na routes za kwenda Stend ya magufuli kutoka mitaa yote ya jiji.
Kama hakuna abiria wa kushuka stendi ya magufuli kwanini basi lifike stendi ya magufuli

Kila huduma lazima ilenge kutatua changamoto za watu na sio watu walazimike kutatua changamoto za huduma inayotolewa.
Usafiri mbona upo mzee ukishuka magufuli uliza stand za daladala za unakoenda au huwa unakutana na wajanja wa jiji wanakudqnganya unapigwa pesa kutoka hapo magufuli hadi stand ya daladala ni chini ya dakika 10 tu tena kwa mguu.
 
Huyu yeye anachokitaka pale Magufuli stendi kuwe na Stendi nyingi ya karibu zaidi au tuseme stendi ya Mwendokasi iwekwe pale nje yaan mtu akitoka ndani anakwea Mwendokasi kapotea mpaka Mbagala kakwea kupotea na Mwendokasi mpaka Tegeta, kakwea Mwendokasi kapotea mpaka Gongolamboto sijui Chanika huko, hivyo ndivyo anavyotaka huyu kijana yaan maisha mbilinge mbilinge hayawezi anataka maisha mseleleleko
Mbona Stendi ya Mabus ya Mwendokasi ipo kwenye geti la kuingilia Stend ya Magufuli!!?
 
Stendi ya Mwendokasi iko karibu na Geti la kuingilia Stendi ya Magufuli
 
Mbona Stendi ya Mabus ya Mwendokasi ipo kwenye geti la kuingilia Stend ya Magufuli!!?
Yeye hataki hivyo yaan anataka stendi ya Mwendokasi iwe ndani ya stendi ya Magufuli, umemuelewa sijui yaan mtu asisogeze hata mguu kuvuka barabara stendi ya Mwendokasi iwe mule mule ndani ya stendi ya Magufuli ukishuka kutoka Kahama unalikuta bus la Mwendokasi linaloelekea Chanika sijui Temeke na Mbagala limekaa pale linakusubiri ndivyo anavyotaka yeye hivyo na Mwendokasi ya huko Temeke, Mbagala sijui Chanika iwe uelekeo ni Magufuli stendi ndani sio nje, ushamuelewa?
 
Uvivu tu , hapa sio ulaya bn
 
Achana na mwendokasi kuna stendi ya daladala hapo jmaa atakuwa mgeni ukivuka tu kafly over kale kwa chini apo kuna stendi
Kisingizio chake ni mizigo, kwamba akishuka Magufuli kwenda Mbezi daladala analazimika kutoa pesa kubebewa mizigo yake
 
Uvivu tu , hapa sio ulaya bn
Hivyo ndivyo anavyotaka yeye yaan hata asisogeze mguu na akifika Chanika sijui Temeke akishuka kwenye Mwendokasi akute pale kuna Tax zinamsubiri anachagua tu anayoitaka km ameshuka Airport anaweka bag anakwea huyooo mpaka huko kwao mafichoni anakojificha, hicho ndicho anachokitaka mleta mada sio usumbufu wa kukimbizana na daladala sijui bajaj sijui bodaboda hapana yeye anataka mseleleleko utelezi anateleza tu chwaaaa
 
Kisingizio chake ni mizigo, kwamba akishuka Magufuli kwenda Mbezi daladala analazimika kutoa pesa kubebewa mizigo yake
Lbd ni mgeni ila kwa wenyeji mapema tu
 
Kisingizio chake ni mizigo, kwamba akishuka Magufuli kwenda Mbezi daladala analazimika kutoa pesa kubebewa mizigo yake
Mabus ya Mwendokasi yanasimama hapo hapo Mlango wa kutokea Stendi ya Magufuli pia Taxi zipo hapo hapo mlangoni.
 
Watu wa Dar ni walalamishi hatari

Sijui mmelewa chips yai....?

Siwaelewagi kwa kweli,

Stendi ya Magufuli, lengo lake ni zuri na litaendelea kuwa zuri mpaka mtakaoisha walalamishi

Watu wa Dar, sjui kama atatokea mtu wa kuwaweza baada ya Magufuli kuondoka..

Ilikuwa hivyo hivyo kwenye vivuko vya Kigamboni, mzee akamwambia mpige mbizi, sisi wa mikoani, huduma za huku ni za hovyo na bei yake juu mara dufu unapolinganisha na Watu wa Dar

Stendi ya Magufuli Mbezi, imekosa usimamizi na maamzi magumu ya serikali basi
Kwamba watu wasielezee changamoto za dar kisa mikoani kuna kubwa zaidi kwani wa mikoani wamekatazwa kuelezea zao, kwahiyo changamoto za mikoani ndio zinahalalisha kuwepo kwa changamoto za dar, hapo ukiuliza hakuna jibu la maana utaambiwa tu acheni wabeba mizigo nao wapate rizki.. halafu eti na sisi tunasema tunataka maendeleo wakati nchi nyingi zilizoendelea hazina huu ujinga
 
Hivyo ndivyo anavyotaka yeye yaan hata asisogeze mguu na akifika Chanika sijui Temeke akishuka kwenye Mwendokasi akute pale kuna Tax zinamsubiri anachagua tu anayoitaka km ameshuka Airport anaweka bag anakwea huyooo mpaka huko kwao mafichoni anakojificha, hicho ndicho anachokitaka mleta mada sio usumbufu wa kukimbizana na daladala sijui bajaj sijui bodaboda hapana yeye anataka mseleleleko utelezi anateleza tu chwaaaa
Naona mko na echo chamber yenu mnajazana ujinga.
Hicho unachosema ndo mleta mada amemaanisha?
 
Naona mko na echo chamber yenu mnajazana ujinga.
Hicho unachosema ndo mleta mada amemaanisha?
Yeah baba amemaanisha stendi ya Mwendokasi ijengwe mlangoni kwao anapoishi akitoka tu hatembei anaingia kwenye bus yupo Magufuli stendi, wewe ulifikiri alimaanisha nini?
 
hata kama wangefanya bado isingekidhi mahitaji ya mji zaidi km za mraba 1500 na watu zaidi ya miloni 5, kwa kifupi dar haikupaswa kuruhisiwa kukuwa na kusambaa zaidi ya ilivyokuwa zamani bila ya pia kukuza miundo mbinu, stendi moja hakuna miujiza yoyote unayoweza kufanya zilitakiwa ziwe nyingi, dar unakwenda km zaidi 20 bado uko mji huo huo, uliona wapi?

na siyo kituo cha mabasi tu fire is same story kama unaishi tegeta kwa mfano nyumba ikishika moto fire inatakiwa isafiri zaidi ya km 20 kuja kuzima moto, na hiyo tegeta siyo mwisho wa chaos ya dar bali inakwenda zaidi mpaka boko, bunju na kuendelea wote hao wanategema fire moja isafiri kutokea upanga kuja kuzima motó, sasa hiyo ni akili au matope? ...
Watu wetu wa mipango miji ni vilaza au viongozi wa serikali ndio vilaza?
 
Huyu yeye anachokitaka pale Magufuli stendi kuwe na Stendi nyingi ya karibu zaidi au tuseme stendi ya Mwendokasi iwekwe pale nje yaan mtu akitoka ndani anakwea Mwendokasi kapotea mpaka Mbagala kakwea kupotea na Mwendokasi mpaka Tegeta, kakwea Mwendokasi kapotea mpaka Gongolamboto sijui Chanika huko, hivyo ndivyo anavyotaka huyu kijana yaan maisha mbilinge mbilinge hayawezi anataka maisha mseleleleko
umenisoma kwelikweli, mifumo lazima isomane na ionane. Unapoona abiria kwenda stendi (lazima) washushwe na bodaboda au wamelowa jasho kwa kutembea au lazima waje kwa gari ndogo ujue kuna ukilaza pahala.
 
Yeah baba amemaanisha stendi ya Mwendokasi ijengwe mlangoni kwao anapoishi akitoka tu hatembei anaingia kwenye bus yupo Magufuli stendi, wewe ulifikiri alimaanisha nini?
Reading comprehension ni tatizo..
 
Back
Top Bottom