jogoo_dume
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 2,204
- 1,939
Habari za muda huu na ni matumaini mko wazima wa afya.
Straight to the matter, hiki kituo kipya cha mabasi ya mikoani hapa Dar es Salaam yaani Magufuli Bus terminal hakikuwa tayari kuanza kutumika. Ilitakiwa kipewe muda kidogo ili kiwe sawa.
Leo nimefika toka Morogoro muda huu kwa mara ya kwanza ktk hicho kituo na kuna changamoto nyingi. Nafikiri kina Jafo walifanya maamuzi kumridhisha tu bwana mkubwa.
Baadhi ya vitu niliyoviona;
1. Mabasi hayana sehemu maalum ya kupandia au kushushia, yaani anayewahi eneo ndio kwa muda huo anatumia hilo eneo hivyo ni ngumu kwa abiria kujua eneo sahihi la kupandia au kushushia kwa kampuni fulani ya basi.
2. Nimetafuta sehemu ya kula ndani hamna zaidi ya wamama lishe waliozagaa zagaa kwa kupanga meza zao maeneo hayo hayo ya karibu na yanaposhushia mabasi abiria.
3. Nimeenda msalani kuna changamoto ya maji.
4. Eneo sehemu kubwa ni giza na kibaya zaidi ukitoka tu nje ya kituo hamna taa, kuelekea kituo cha daladala yaani ni giza na unapishana na vijana kwa muonekano wanaweza kuwa vibaka na wakatumia faida ya hilo giza kuibia watu.
5. Barabara ya kuingia na kutoka mabasi haiko sawa bado, ya vumbi.
6. Ukifika stendi ya daladala ya Mbezi kuna taa zimewekwa ila zimezimwa sijui mbovu houo eneo ni giza mpaka zimewashwa taa 'vibatari'.
7. Mwendokasi hamna.
8. nk
Nilitegemea wangekua wameshafanya research na kujua walau basic issues ambazo ilitakiwa ziwe tayari kabla ya kuanza kutumika kwa kituo.
viongozi waache kukurupuka maana wanaopata tabu kutokana na mikurupuko yao ni raia watumiaji wa hiyo miundo mbinu.