Stendi mpya ya mabasi ya Magufuli haikuwa tayari kuanza kutumika

Stendi mpya ya mabasi ya Magufuli haikuwa tayari kuanza kutumika

Kuna Hospital Moja Dodoma Nayo Itafuata Njia Ya Hiyo Stendi Yaani Itazinduliwa Wakati Haijakamilika,
 
1614490806277.png
 
Kwasisi wakazi wa kaskazini short cut ni barabara ya kimara mbezi via msitu wa pande kwenda kutokea Bunju ni rahisi lakini bado tunazungushwa tu mwenge ambapo ni mbali.

Hakukuwa na ulazima wa kufungua stand kama ilikuwa haijakamilika ,sasa kama maji hakuna,rough road si utopolo huo?
 
Upo sahihi, wamekurupuka kutokana na woga kwa Mfalme.

Changamoto nyingine kubwa zaidi itakayofuata ni UCHAFU, utashangaa siku si nyingi kuta zimeloa mikojo na chini kuna vichupa vya mikojo kila pahala.

Wabongo wengi wachafu, si wastaarabu na zaidi sio watunzaji wa vitu vizuri.
Uchafu ni jadi yenu nyie wa Mkoa wa Dar
 
Waacheni professionals wafanye kazi zao, msiingize siasa zenu chafu kwenye Miradi
Shida mzee hazingatii ubora anazingatia namba. Furaha yake ni kuona anazindua miradi kila siku. Mradi mzuri km huo hakukuwa na sababu za kuukimbiza kimbiza. Ndio maana JK alikataa nyumba yake kuharakishwa.
 
Tutaelewana tu maendeleo hayana chama. Watu wa jimbo la ubungo/kibamba mmekosa barabara za lami kutokana na mbunge aliyetoka upinzani ambaye alikuwa mbunge wenu.
 
Habari za muda huu na ni matumaini mko wazima wa afya...
Straight to the matter, hiki kituo kipya cha mabasi ya mikoani hapa Dar es Salaam yaani Magufuli Bus terminal hakikuwa tayari kuanza kutumika. Ilitakiwa kipewe muda kidogo ili kiwe sawa.

Leo nimefika toka Morogoro muda huu kwa mara ya kwanza ktk hicho kituo na kuna changamoto nyingi. Nafikiri kina Jafo walifanya maamuzi kumridhisha tu bwana mkubwa.
baadhi ya vitu niliyoviona;
1. Mabasi hayana sehemu maalum ya kupandia au kushushia, yaani anayewahi eneo ndio kwa muda huo anatumia hilo eneo hivyo ni ngumu kwa abiria kujua eneo sahihi la kupandia au kushushia kwa kampuni fulani ya basi.

2. Nimetafuta sehemu ya kula ndani hamna zaidi ya wamama lishe waliozagaa zagaa kwa kupanga meza zao maeneo hayo hayo ya karibu na yanaposhushia mabasi abiria.

3. Nimeenda msalani kuna changamoto ya maji.

4. Eneo sehemu kubwa ni giza na kibaya zaidi ukitoka tu nje ya kituo hamna taa, kuelekea kituo cha daladala yaani ni giza na unapishana na vijana kwa muonekano wanaweza kuwa vibaka na wakatumia faida ya hilo giza kuibia watu.

5. Barabara ya kuingia na kutoka mabasi haiko sawa bado, ya vumbi.

6. Ukifika stendi ya daladala ya Mbezi kuna taa zimewekwa ila zimezimwa sijui mbovu houo eneo ni giza mpaka zimewashwa taa 'vibatari'.

7. Mwendokasi hamna...

8. nk

Nilitegemea wangekua wameshafanya research na kujua walau basic issues ambazo ilitakiwa ziwe tayari kabla ya kuanza kutumika kwa kituo.

viongozi waache kukurupuka maana wanaopata tabu kutokana na mikurupuko yao ni raia watumiaji wa hiyo miundo mbinu.
Namba 2 sijapenda aisee, yaani meza zimepangwa tu
 
Binafsi nashangazwa Sana kutumika wakati ni just tu nilipelekakifusi Cha kambodia pale kumwaga hata week mbili haijaisha na ilikuwaa bado Sana mchina ananiambia kuwaa ni mpk labda mwakani ndio ingekuwa taayar sasa sasahv wanalipua tu ilimradi wamridhishe raisi magufuli
Heeeeeh?
 
Upo sahihi, wamekurupuka kutokana na woga kwa Mfalme.

Changamoto nyingine kubwa zaidi itakayofuata ni UCHAFU, utashangaa siku si nyingi kuta zimeloa mikojo na chini kuna vichupa vya mikojo kila pahala.

Wabongo wengi wachafu, si wastaarabu na zaidi sio watunzaji wa vitu vizuri.
hiyo tunasema ni unkwepao inshuuu 🤣
 
Back
Top Bottom