KERO Stendi Ya Basi Msamvu Morogoro inalipisha pesa ya kuingia hata kama una tiketi

KERO Stendi Ya Basi Msamvu Morogoro inalipisha pesa ya kuingia hata kama una tiketi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
NCHI Ina ujinga mwingi sana hii! Mi siku nitajifanya Sina mia tatu zaidi ya ticket,nione itakuwaje! .....maana Moro ndio kitaa,nitamtoa mtu meno ya mbele!
Wewe utakua wa chamwino au sabasaba 😀
 
Watanzania ni kama tumerogwa hizo tozo za Stand zote wangetoa tu ni ujinga wa kiwango cha juu kuwachaji watu wanaosafiri kwa lundo la Tozo lililopo kwenye mafuta na hayo magari...
Walitamani waweke tozo viwanja vya ndege wameona aibu kwa sababu viwanja vinaenda na standard za Dunia..
Usemacho Ni Kweli Yaani Abiria Anakata Ticket Analipa Kodi Zote
Bado Muda Wa Safari Yake Haruhusiwi Kufanya, Hiyo Safari Mpaka Alipe Tzs 300/= Wakati Tuna Vyanzo Tele Nchini Vya Mapato Yasiyoudhi

Tenda Wanapeana Kijamaa Mbaya Ukiingia Choo Hakina Usafi Wowote
Viongozi Wetu Ubunifu Umeisha Sasa Wanawaza Vitu Vidogo Vidogo
 
Dodoma pia wanafanya hivi. Sijui wana shida gani
 
Morogoro ni mkoa wenye rushwa na ufisadi wa hali ya juu!
Pia ndio Halmashauri yenye watumishi mediocre kuliko zote Tz. Ubunifu F Ufanisi zero kabisa. Kuna Mzee aliwahi niambie kuwa, watumishi wengi Moro ni wale wa kupachikwa tu pasipo vigezo, watoto na vimada wa vigogo wazurulao Dom-Dar Kila siku.
"Nikikuweka Dar tutashtukiwa, Dom nako hivyohivyo, nitakuficha Moro uncle eeenh au baby enh"
Pumbavu!
 
Ile stendi ya msamvu ni ya kisasa sana sema inaendeshwa kizamani,
 
Hilo hata stendi kuu ya Mbeya lipo. Wanadai kama umekata tiketi online na hauna tiketi ya karatasi ili uingie ndani lazima ulipie pale getini.
 
Leo Nimeshangaa Sana Nilipofika Stendi Tajwa Baadaya
Mgeni Wangu Kumkatia Ticket Ya Basi Kuelekea Nyanda Za Juu Kusini.

Nilipofika Mgeni Aingie Stendi Naambiwa Pamoja Na Kukata Ticket Hawezi Kuingia Ndani Mpaka Alipie Tzs 300/= Kiingilio

Manispaa Ya Morogoro Hata Kama Mnakusanya Mapato Ila Hii Ni Dhuruma Kwa Watanzania Wote Wanaotumia Kituo Hicho
Tunachojua Msindikiza Abiria Ndiyo Anayepaswa Kulipa Ila Abiria Ameshalipia Kupitia Ticket Yake Ya Basi Husika

Mkurugenzi Ajitafakari Maana Hizi Tenda Mnazopeana Hamtaweza Kuongeza Mapato Kamwe Ni Vyanzo Kibudu /Dhuruma Kwa Wananchi.

Yaani Huu Siyo Ubunifu Ila Kero Kwa Abiria

Huwa najiuliza hiyo hela wanayocharge watu kuingia stand ni ya huduma gani sijapata majibu?
Fikiria hata kwenda msalani ukiwa ndani, inabidi ulipie tena... l
 
Back
Top Bottom