SI KWELI Stendi ya Mabasi ya Magufuli (Mbezi Luis) Imebadilishwa Jina

SI KWELI Stendi ya Mabasi ya Magufuli (Mbezi Luis) Imebadilishwa Jina

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mlioko hapo Karibu embu mtujuze iwapo hizi habari ni za kweli.

Wengine wanasema kuna kikundi kimepewa kazi maalum ya kushughulikia legacy. Kimeona umati mwingi wa wageni unafika hapo Toka mikoa mbalimbali na hivyo Jina la Magufuli linaweza lisifutike.

1702990351854.png
 
Tunachokijua
Stendi ya Mabasi ya Magufuli ni kituo kikuu cha Mabasi ya masafa marefu kinachopatikana katika Jiji la Dar es Salaam. Kituo hiki kilizinduliwa na Hayati Magufuli mnamo Februari 21, 2021 aliyekuwa Rais wakati huo na kituo kikapewa jina lake kama heshima kwake.

Tangu Desemba 16 kumeibuka uvumi unaodai kuwa Stendi ya Mabasi ya Magufuli imebadilishwa jina na kuwa na kuitwa Dar es Salaam Bus Terminal. Uvumi huu ulianza kutokana na picha iliyotumiwa na Habari Leo wakieleza mapato ya kituo hicho kwa siku. Tazama hapa chini:

img_9962-jpeg.2846494

Picha inayosambaa ikihusishwa na kubadilika jina kwa Kituo cha Magufuli
Picha hiyo ilisambaa zaidi na kuibua mijadala katika mitandao mingine. Mathalani, katika Jukwaa la JamiiForums.com ikiwamo mleta mada hii (JF Member) na Mirindimo waliibuka na kuhoji kwa lengo la kutaka kujua uhalisia wa uvumi huo.

Je, kuna ukweli kwenye uvumi huo?
JamiiCheck imepitia vyanzo vya mbalimbali ikiwamo Google image Search na kufika kituoni hapo imebaini kuwa uvumi wa kituo cha Magufuli kubadili jina hauna ukweli wowote.

Kupitia Google image Search JamiiCheck imebaini kwamba picha hizo zinazovumi zilikuwapo mtandaoni tangu Februari mwaka 2021 na zilipigwa kabla ya kituo hicho hakijabadiliwa jina kutoka kuwa Dar es Salaam Bus Terminal na kupewa jina la Magufuli.

Zaidi ya hayo, JamiiCheck imefika eneo la kituo hicho ili kuhakiki kama jina la kituo hicho kimebadilika lakini imekuta bado kituo hicho kinaitwa Magufuli Bus Terminal kama ilivyokuwa tangu kituo hicho kilipopewa jina hilo mwaka 2021. Hizi hapa chini ni baadhi ya picha ambazo zimepigwa leo Desemba 19, 2023:

1702969669112-jpeg.2846856

Picha ya kituo cha Mabasi ya magufuli iliyopigwa Desemba 19, 2023
...Vilaza FC inaundwa na Mbowe form four failure, Msigwa babantilie la Tatu aliyeacha shule, Lema mwizi wa magari form two failure,sugu bwana mitepesho matakoni la 3D failure alizungusha Hisabati na masomo ya akapata wastani wa F na majinga na kichaaa kama wewe
Jina limeng'olewa .
 
Hao waliokupa hiyo taarifa,, deal nao waendelee kukupa feedback pia ya nini kinachoendelea??
 
Sasa mkuu hapa umeongea nini na unakubali na kupinga nini? Magufuli hakulazimisha hilo jina bhana kila mtu anajua
Angekataa kwa kumaanisha lisingewekwa, hivi ni nani mwenye uthubutu wa kufanya Jambo ambalo rais amelikataza, tena rais mwenyewe Magu
 
Vilaza FC inaundwa na Mbowe form four failure, Msigwa babantilie la Tatu aliyeacha shule, Lema mwizi wa magari form two failure,sugu bwana mitepesho matakoni la 3D failure alizungusha Hisabati na masomo ya akapata wastani wa F
Wewe ulipata div 1 ila unaishi kwenye umaskini wa kutupwa unaowaita failure ni mabilionea
 
Mlioko hapo Karibu embu mtujuze iwapo hizi habari ni za kweli.

Wengine wanasema kuna kikundi kimepewa kazi maalum ya kushughulikia legacy . Kimeona umati mwingi wa wageni unafika hapo Toka mikoa mbalimbali na hivyo Jina la Magufuli linaweza lisifutike.
Wanajidanganya !! 😅🙏
 
Heee kweli? Vipi pesa za plea bargain mbona hazikufika hazina?

Vipi ripoti ya wezi wa mali za CCM ikafichwa na hakuna aliyewekwa ndani?

Takukuru waliambiwa wachunguze watoa rushwa kampeni ccm mbona sikuona aliyekamatwa?

Ripoti ya makinikia kuna mafisadi walitajwa mbona sijaona aliyewekwa selo?

Vipi mwanyika kesi ya Billion 2 mkampa ubunge bado?

Nitajie mahakama ya mafisadi iliwahi mfunga nani kwa kumkuta na hatia?

JPM alikua na wafuasi wajinga sana, mnadanganywa na maneno wakati matendo tofauti.
Alikuwa anaelekea kwenda kuwashighulikia wote na skendo zote ulizozitaja kama asingeondoka !!
Na ndio maana uchaguzi ulikuwa vile !!
Kuna watu wangejuta kuzaliwa !!
 
Duh 🙄 Asalaleee !!
Kumbe Kivuli chake bado kinaendelea kutesa baadhi ya watu ??! 🤣🤣
Wangemuachia tu hilo jina lake maana hata Mwalimu Nyerere pamoja na siasa ya ujamaa kutupiliwa mbali lakini jina lake bado linaishi sana tu !
Wengine wameshasahaulika kitambo !!🙏🙏
 
Duh 🙄 Asalaleee !!
Kumbe Kivuli chake bado kinaendelea kutesa baadhi ya watu ??! 🤣🤣
Wangemuachia tu hilo jina lake maana hata Mwalimu Nyerere pamoja na siasa ya ujamaa kutupiliwa mbali lakini jina lake bado linaishi sana tu !
Wengine wameshasahaulika kitambo !!🙏🙏
Kwenye system majangili yote yamerudi hivyo lazima washughulike na Magu sababu aliwatosa
 
Back
Top Bottom