SI KWELI Stendi ya Mabasi ya Magufuli (Mbezi Luis) Imebadilishwa Jina

SI KWELI Stendi ya Mabasi ya Magufuli (Mbezi Luis) Imebadilishwa Jina

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mlioko hapo Karibu embu mtujuze iwapo hizi habari ni za kweli.

Wengine wanasema kuna kikundi kimepewa kazi maalum ya kushughulikia legacy. Kimeona umati mwingi wa wageni unafika hapo Toka mikoa mbalimbali na hivyo Jina la Magufuli linaweza lisifutike.

1702990351854.png
 
Tunachokijua
Stendi ya Mabasi ya Magufuli ni kituo kikuu cha Mabasi ya masafa marefu kinachopatikana katika Jiji la Dar es Salaam. Kituo hiki kilizinduliwa na Hayati Magufuli mnamo Februari 21, 2021 aliyekuwa Rais wakati huo na kituo kikapewa jina lake kama heshima kwake.

Tangu Desemba 16 kumeibuka uvumi unaodai kuwa Stendi ya Mabasi ya Magufuli imebadilishwa jina na kuwa na kuitwa Dar es Salaam Bus Terminal. Uvumi huu ulianza kutokana na picha iliyotumiwa na Habari Leo wakieleza mapato ya kituo hicho kwa siku. Tazama hapa chini:

img_9962-jpeg.2846494

Picha inayosambaa ikihusishwa na kubadilika jina kwa Kituo cha Magufuli
Picha hiyo ilisambaa zaidi na kuibua mijadala katika mitandao mingine. Mathalani, katika Jukwaa la JamiiForums.com ikiwamo mleta mada hii (JF Member) na Mirindimo waliibuka na kuhoji kwa lengo la kutaka kujua uhalisia wa uvumi huo.

Je, kuna ukweli kwenye uvumi huo?
JamiiCheck imepitia vyanzo vya mbalimbali ikiwamo Google image Search na kufika kituoni hapo imebaini kuwa uvumi wa kituo cha Magufuli kubadili jina hauna ukweli wowote.

Kupitia Google image Search JamiiCheck imebaini kwamba picha hizo zinazovumi zilikuwapo mtandaoni tangu Februari mwaka 2021 na zilipigwa kabla ya kituo hicho hakijabadiliwa jina kutoka kuwa Dar es Salaam Bus Terminal na kupewa jina la Magufuli.

Zaidi ya hayo, JamiiCheck imefika eneo la kituo hicho ili kuhakiki kama jina la kituo hicho kimebadilika lakini imekuta bado kituo hicho kinaitwa Magufuli Bus Terminal kama ilivyokuwa tangu kituo hicho kilipopewa jina hilo mwaka 2021. Hizi hapa chini ni baadhi ya picha ambazo zimepigwa leo Desemba 19, 2023:

1702969669112-jpeg.2846856

Picha ya kituo cha Mabasi ya magufuli iliyopigwa Desemba 19, 2023
Ccm hawategemei kura kukaa madarakani, na udhibitisho ni pale dhalimu magu alipofanya siasa peke yake na chama lake la majizi, lakini ilipofika wakati wa uchaguzi na alichokiona kwenye kampeni zile ilibidi apore mchakato wa uchaguzi.
👍👏
 
Ubungo Interchange
Tazara interchange
Mwenge interchange
Chang'ombe interchange
..,.......etc
Kwa kweli hii itapendeza kuita majina ya sehemu husika ili kutokuleta mchanganyo hasa kwa wageni na ramani.

Nafikiri ni vizuri majina ya watu yakatafutiwa vitu vingine km viwanja vya michezo, majengo nk, ili kutopotosha ramani/locations.
 
Sio rahisi hilo jambo kufanyika, kumbe wengi hata hamjui matukio ya Kisiasa kulingana na nyakati.

Ina maana hamjui yule Mzee ameacha wafuasi zaidi ya 10M plus Nchini? Zile ni Kura

Na CCM inajua kitendo cha kufanya huo upuuzi kunaweza kuwanyima kura 2024 na 2025.

Nitakuwa wa mwisho kukubaliana na hii Propaganda.

Kama mnadhani masihara ajitokeze mtu tuweke 500k kila mmoja tufanye betting
CCM sio wajinga kufanya ujinga kama huu! Magufuli amekufa lakini bado anao ushawishi mkubwa sana kwa wananchi …kati ya kosa CCM hawawezi fanya ni hili..! Hiyo ni picha ya zamani kabla ya kupewa jina la Magufuli
 
Inawezekana kuna ukweli Ila watakuwa wajinga sana legacy ya Magufuli haifutwi na kuondoa jina lake stendi NEVER

Yale yale ya kuzuia wajawazito kuingia wodini na simu wakihofia huduma zao mbovu zitaandikqa mitandaoni

Viongozi wetu badilikeni msifanye kazi kwa kukariri
 
Sasa mkuu hapa umeongea nini na unakubali na kupinga nini? Magufuli hakulazimisha hilo jina bhana kila mtu anajua
Wewe ulikuwa humjui DIKTETA anavyo operate!! Angekuwa hataki ANGEKATAA kama Mkapa alivyokataa alipokuwa hai, na uwanja ukapewa jina lake baada ya yeye kufa.

Lile DUBWASHA lilikuwa linapenda sifa sana na ndiyo maana likawa linawadanganya nyie WAJINGA kuwa bila lenyewe miundombinu haitajengwa na kwamba linajenga kwa fedha za ndani. Mlivyo wajinga MUKAAMINI.
 
Vilaza FC inaundwa na Mbowe form four failure, Msigwa babantilie la Tatu aliyeacha shule, Lema mwizi wa magari form two failure,sugu bwana mitepesho matakoni la 3D failure alizungusha Hisabati na masomo ya akapata wastani wa F
Pole ndiyo hivo ishabadilishwa jina
Mwendazake alikua muhun sana

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wewe ulikuwa humjui DIKTETA anavyo operate!! Angekuwa hataki ANGEKATAA kama Mkapa alivyokataa alipokuwa hai, na uwanja ukapewa jina lake baada ya yeye kufa.

Lile DUBWASHA lilikuwa linapenda sifa sana na ndiyo maana likawa linawadanganya nyie WAJINGA kuwa bila lenyewe miundombinu haitajengwa na kwamba linajenga kwa fedha za ndani. Mlivyo wajinga MUKAAMINI.
Hata plan ya ujenzi wa ofisi mpya ya makao makuu ya chadema ipo muda mrefu lakini hela za ruzuku ya chama zinaliwa na Joyce Mukya tu.

Hongera Halima Mdee kwa kukomesha udikteta wa Mbowe.
 
Bora waliondoe maana yule hakuwa binadamu bali shetani muuaji akishirikiana na jambazi Makonda
Vilaza FC inaundwa na Mbowe form four failure, Msigwa babantilie la Tatu aliyeacha shule, Lema mwizi wa magari form two failure,sugu bwana mitepesho matakoni la 3D failure alizungusha Hisabati na masomo ya akapata wastani wa F
 
Vijana punguzeni bangi mbichi. Msije mkawa Kama huyu. Mada inaongelewa jina stendi ya mabasi mtu anawashambulia Viongozi wa CHADEMA. Utadhani ndio wamebadilisha jina.
Vilaza FC inaundwa na Mbowe form four failure, Msigwa babantilie la Tatu aliyeacha shule, Lema mwizi wa magari form two failure,sugu bwana mitepesho matakoni la 3D failure alizungusha Hisabati na masomo ya akapata wastani wa F
 
Wewe ulikuwa humjui DIKTETA anavyo operate!! Angekuwa hataki ANGEKATAA kama Mkapa alivyokataa alipokuwa hai, na uwanja ukapewa jina lake baada ya yeye kufa.

Lile DUBWASHA lilikuwa linapenda sifa sana na ndiyo maana likawa linawadanganya nyie WAJINGA kuwa bila lenyewe miundombinu haitajengwa na kwamba linajenga kwa fedha za ndani. Mlivyo wajinga MUKAAMINI.
Vilaza FC inaundwa na Mbowe form four failure, Msigwa babantilie la Tatu aliyeacha shule, Lema mwizi wa magari form two failure,sugu bwana mitepesho matakoni la 3D failure alizungusha Hisabati na masomo ya akapata wastani wa F
 
Mlioko hapo Karibu embu mtujuze iwapo hizi habari ni za kweli.

Wengine wanasema kuna kikundi kimepewa kazi maalum ya kushughulikia legacy . Kimeona umati mwingi wa wageni unafika hapo Toka mikoa mbalimbali na hivyo Jina la Magufuli linaweza lisifutike.
Endeleeni tu mkae kwa kutulia mpk majina yaliyopo katika madaraja Yale ya ubungo na buguruni yatabadirishwa tu wanadam haturidhiki na yaliyosiniwa
 
Hakulazimisha wakati nyuma ya pazia alikuwa anaagiza, kisha akitokea hadharani anajifanya hataki. Kama alikuwa anaita nchi Tanzania ya Magufuli, Nini stand?
Sasa uko nyuma ulikuwepo mkuu?
 
Back
Top Bottom