SI KWELI Stendi ya Mabasi ya Magufuli (Mbezi Luis) Imebadilishwa Jina

SI KWELI Stendi ya Mabasi ya Magufuli (Mbezi Luis) Imebadilishwa Jina

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mlioko hapo Karibu embu mtujuze iwapo hizi habari ni za kweli.

Wengine wanasema kuna kikundi kimepewa kazi maalum ya kushughulikia legacy. Kimeona umati mwingi wa wageni unafika hapo Toka mikoa mbalimbali na hivyo Jina la Magufuli linaweza lisifutike.

1702990351854.png
 
Tunachokijua
Stendi ya Mabasi ya Magufuli ni kituo kikuu cha Mabasi ya masafa marefu kinachopatikana katika Jiji la Dar es Salaam. Kituo hiki kilizinduliwa na Hayati Magufuli mnamo Februari 21, 2021 aliyekuwa Rais wakati huo na kituo kikapewa jina lake kama heshima kwake.

Tangu Desemba 16 kumeibuka uvumi unaodai kuwa Stendi ya Mabasi ya Magufuli imebadilishwa jina na kuwa na kuitwa Dar es Salaam Bus Terminal. Uvumi huu ulianza kutokana na picha iliyotumiwa na Habari Leo wakieleza mapato ya kituo hicho kwa siku. Tazama hapa chini:

img_9962-jpeg.2846494

Picha inayosambaa ikihusishwa na kubadilika jina kwa Kituo cha Magufuli
Picha hiyo ilisambaa zaidi na kuibua mijadala katika mitandao mingine. Mathalani, katika Jukwaa la JamiiForums.com ikiwamo mleta mada hii (JF Member) na Mirindimo waliibuka na kuhoji kwa lengo la kutaka kujua uhalisia wa uvumi huo.

Je, kuna ukweli kwenye uvumi huo?
JamiiCheck imepitia vyanzo vya mbalimbali ikiwamo Google image Search na kufika kituoni hapo imebaini kuwa uvumi wa kituo cha Magufuli kubadili jina hauna ukweli wowote.

Kupitia Google image Search JamiiCheck imebaini kwamba picha hizo zinazovumi zilikuwapo mtandaoni tangu Februari mwaka 2021 na zilipigwa kabla ya kituo hicho hakijabadiliwa jina kutoka kuwa Dar es Salaam Bus Terminal na kupewa jina la Magufuli.

Zaidi ya hayo, JamiiCheck imefika eneo la kituo hicho ili kuhakiki kama jina la kituo hicho kimebadilika lakini imekuta bado kituo hicho kinaitwa Magufuli Bus Terminal kama ilivyokuwa tangu kituo hicho kilipopewa jina hilo mwaka 2021. Hizi hapa chini ni baadhi ya picha ambazo zimepigwa leo Desemba 19, 2023:

1702969669112-jpeg.2846856

Picha ya kituo cha Mabasi ya magufuli iliyopigwa Desemba 19, 2023
Ni
Sio kubadilisha jina haitoshi wavunje madaraja wafukie mabwawa wang'oe reli wazamishe vivuko meli wauze ndege bado atakumbukwa kwa moyo wake wa kizalendo na kuipigania nchi na wananchi dhidi ya wala rushwa na mafisadi!
MBona una hasira sana, angalia usije kuwa gaidi a
 
Jf kuna mijitu mipuuz sn .... Pia hta wakbadirisha majna wao hawafi? Unajua wanadamu huwa tunaweka Kibri sanaaaaa kana kwamba hatufi na tutaish milele ...

Wamejifunza kiburi kutoka kwa mwendazake. Baba wa uovu.
 
Vilaza FC inaundwa na Mbowe form four failure, Msigwa babantilie la Tatu aliyeacha shule, Lema mwizi wa magari form two failure,sugu bwana mitepesho matakoni la 3D failure alizungusha Hisabati na masomo ya akapata wastani wa F

Vijana punguzeni bangi mbichi. Msije mkawa Kama huyu. Mada inaongelewa jina stendi ya mabasi mtu anawashambulia Viongozi wa CHADEMA. Utadhani ndio wamebadilisha jina.
 
Mlioko hapo Karibu embu mtujuze iwapo hizi habari ni za kweli.

Wengine wanasema kuna kikundi kimepewa kazi maalum ya kushughulikia legacy . Kimeona umati mwingi wa wageni unafika hapo Toka mikoa mbalimbali na hivyo Jina la Magufuli linaweza lisifutike.
Futa jina la huyo kiongozi muovu.
 
Ni
Sio kubadilisha jina haitoshi wavunje madaraja wafukie mabwawa wang'oe reli wazamishe vivuko meli wauze ndege bado atakumbukwa kwa moyo wake wa kizalendo na kuipigania nchi na wananchi dhidi ya wala rushwa na mafisadi!

Jina linaweza kuondolewa ila hiyo miradi ni Mali ya Umma. Imejengwa kwa Kodi za wananchi sio pesa za mtu binafsi.
 
Ni
Sio kubadilisha jina haitoshi wavunje madaraja wafukie mabwawa wang'oe reli wazamishe vivuko meli wauze ndege bado atakumbukwa kwa moyo wake wa kizalendo na kuipigania nchi na wananchi dhidi ya wala rushwa na mafisadi!
Kwani hivyo vitu alifanya kwa fedha zake? Kukumbukwa sio issue maana hata Hitler, Iddy Amin and the likes tunawakumbuka.
 
Mkuu kapigania nchi kwenye vita ipi? Ya lini, iilipiganwa wapi?

Mkuu hao wala rushwa na mafisadi ni kina nani? Na alipigana nao lini? Wapi? Wapo gereza gani kama wafungwa wa kivita?

Angalau tutajie orodha yao kwa ushahidi, inaonekana ulimeza uongo na propaganda zake JPM bila kutafuna!

Mkuu unakoelekea, siku moja utasema vitambulisho vya machinga vilitumika kukopa!
 
Magufuli hawamuwezi, kile chuma...kanda ya ziwa huwaambii kitu

Kanda ya Ziwa ipi?. Mnajificha kwenye Kanda ya Ziwa kana kwamba hatukuwepo 2020 kwenye uchaguzi mkuu. Rais wa kwanza CCM kupata asilimia 57 ya kura. Akaona aijiongezee za wizi 2020. Yule jamaa alikuwa mwovu kupindukia, Bora aliondoka mapema na kiburi chake Cha uzima.
 
Utateseka sana lakini huwezi kubadili ukweli...
JPM alishinda kihalal na hata sasa kiwekwe kivuli chake, kitashinda
 
Kwani hivyo vitu alifanya kwa fedha zake? Kukumbukwa sio issue maana hata Hitler, Iddy Amin and the likes tunawakumbuka.
Nafikiri pasi na shaka ndio maana nimeandika hivyo kwa kujua sio pesa zake ni zenu!
 
Mkuu kapigania nchi kwenye vita ipi? Ya lini, iilipiganwa wapi?

Mkuu hao wala rushwa na mafisadi ni kina nani? Na alipigana nao lini? Wapi? Wapo gereza gani kama wafungwa wa kivita?

Angalau tutajie orodha yao kwa ushahidi, inaonekana ulimeza uongo na propaganda zake JPM bila kutafuna!

Mkuu unakoelekea, siku moja utasema vitambulisho vya machinga vilitumika kukopa!
Mimi kumbu kumbu yangu ni ile hasira ya vyeti feki!
 
Back
Top Bottom