Stendi ya mabasi ya mikoani Ubungo kuhamishwa kupisha kituo cha mabasi ya Mwendo Kasi

Stendi ya mabasi ya mikoani Ubungo kuhamishwa kupisha kituo cha mabasi ya Mwendo Kasi

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha Mabasi Yaendayo Haraka (UDART), kilichopo Jangwani na kukipeleka kwenye kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo (UBT).

Hatua hiyo inatokana na eneo hilo la Jangwani kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hali inayosababisha kuharibika kwa magari hayo.

Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha madiwani jana, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, alisema uamuzi huo umefikiwa ili kunusuru magari hayo yasiendelee kuharibika.

Alisema Menejimenti ya Kampuni ya UDART na viongozi wa jiji wapo kwenye majadiliano kuhusu suala hilo ili waweze kufikia mwafaka.

“Kwa sasa tupo kwenye majadiliano kwa ajili ya kuhamisha kituo cha mabasi yaendayo kasi(UDART) cha Jangwani tuweze kukipeleka Ubungo kwa sababu eneo la Jangwani limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara mvua inaponyesha,”alisema Mwita.

Alisema suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi na Halmashauri ya Jiji hilo ipo kwenye mchakato wa kupanua Mto Msimbazi uweze kuwa na nafasi kubwa ya kusafirisha maji hadi baharini.

Meya alisema jambo hilo linaweza kupunguza mafuriko katika eneo la Jangwani na maeneo karibu na mto huo.

Alisema fedha za upanuzi huo zimekwisha kutolewa, kilichobaki ni utekelezaji wa mradi kuanzia daraja la Salendar hadi Pugu.

“Awamu ya kwanza ya mradi itaanzia Salendar hadi Kigogo, jambo ambalo linaweza kupunguza ukubwa wa tatizo la mafuriko kwa wakazi wa Jangwani na maeneo jirani ya mto Msimbazi,” alisema.

Vilevile, Meya Mwita alisema Serikali Kuu imetoa shilingi bilioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kisasa çha mabasi yaendayo mikoani, kitakachojengwa Mbezi Mwisho.

Alisema licha ya kutolewa kiasi hicho cha fedha, jiji limetoa shilingi bilioni nane kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi ambao maeneo yao yatachukuliwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

“Tunatarajia kupata ekari 24 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha Mbezi Mwisho, ujenzi ambao utaanza wakati wowote kuanzia sasa. Mkakati uliopo ni kuwalipa fidia wananchi wa eneo lile tuweze kuendeleza mradi,” alisema.

Alisema mradi huo utachukua miaka miwili kukamilika na ndani yake kutakua na maduka na nyumba za kulala wageni, jambo ambalo linaweza kuwasaidia kuongeza mapato.

Alisema mwaka huu katika makusanyo yake ya kila mwaka, halmashauri imeingiza shilingi bilioni 22 ambazo zitatumika kwa mambo mbalimbali yakiwamo uendelezaji wa miradi.

Chanzo: Swahili Times
========

Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha mabasi yaendayo haraka (UDART), kilichopo Jangwani na kupeleka kwenye kituo cha mabasi ya mikoani Ubungo UBT, kutokana na eneo hilo la Jangwani kujaa maji kila mara wakati mvua zinaponyesha.

Picha ya chini ni mchoro wa kituo kipya cha mabasi ya mikoani kitakachojengwa Mbezi Luois jijini Dar es salaam.
IMG_20180509_103132_308.jpg
IMG_20180509_104147_284.jpg
 
Inahamia wapi tena,isije ikawa Kibaha!,mi hata ile stendi ya Mwanza kule Nyegezi huwa naona ni mbali from town,sasa hii Ubungo tu inahama!
 
Wastage of money itawagharimu. Upuuzi gani walifanya kujenga Kituo pale shamba la mpunga Ifakara?
Mkuu wwe huoni kuna mianya inatengenezwa hapo watu waishi
Jiulize ujenzi wa huu mradi ulianza lini
Hawakuwa na uchambuz yakinifu juu ya eneo la jangwani
Nani aliizinisha ujengaji wa yard bila kufata ushauri

Hizi ni janja janja za upotevu wa pesa
 
Hivi wakati wanajenga ile ofisi pale jangwani kipindi chote cha ujenzi haijawahi kunyesha mvua wakaona mafuriko au ndio akili za wasomi ziliganda kama uji wa cement [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Maana unaweza kufikiri wakati wooote wa ujenzi wa zile ofisi na yard basi hapakuwahi kunyesha mvua zikafurisha eneo.

Watanzania ni viumbe wazito sana sijui tu. Hata na UDART wenyewe wamerudi kwenye ticket za vishina .

Saa nyingine unaamua kusahau kila kitu ila kuna kodi nilikatwa kwenye pato langu imechezewa pale ndio maana akili yangu haikubali kusahau kabisa. [emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25]
 
Inahamia wapi tena,isije ikawa Kibaha!,mi hata ile stendi ya Mwanza kule Nyegezi huwa naona ni mbali from town,sasa hii Ubungo tu inahama!
Mbezi Luois ndo stendi mpya na hiyo hapo pichani mchoro wake..!
 
Hivi wakati wanajenga ile ofisi pale jangwani kipindi chote cha ujenzi haijawahi kunyesha mvua wakaona mafuriko au ndio akili za wasomi ziliganda kama uji wa cement [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Maana unaweza kufikiri wakati wooote wa ujenzi wa zile ofisi na yard basi hapakuwahi kunyesha mvua zikafurisha eneo.

Watanzania ni viumbe wazito sana sijui tu. Hata na UDART wenyewe wamerudi kwenye ticket za vishina .

Saa nyingine unaamua kusahau kila kitu ila kuna kodi nilikatwa kwenye pato langu imechezewa pale ndio maana akili yangu haikubali kusahau kabisa. [emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25][emoji25]

Yaani kodi zetu zinapiga chenga kuliko siye wenye mpira...maamuzi Yao gharama kwetu mara mia...
 
Back
Top Bottom