Unatumia mfano wa City center ndio unasema karibu.
Mbona huzungumzii mtu wa Gongo la mboto, Temeke, Chanika.
Hili jambo liangaliwe tena tusije kujilaumu tena baadae.
Hii stand bora waigawe, nyingine iwe kule Temeke(nadhani hii ipo tayari) kwa magari yaendayo mikoa ya Mtwara na Lindi.
Nyingine iwe Tegeta kwa magari yaendayo Tanga, KLM, Arusha, Manyara via Moshi.
Halafu hii ndio wailete Mbezi Louis.
Lakini bado kutakuwa na adha pia ya mtu anayeishi mbezi(Goba) akitaka kusafiri kwenda Mtwara na pia anayeishi Chanika akitaka kusafiri kuelekea mikoa mingine ambapo inabidi akapande gari Mbezi Louis.